Sunday, August 11, 2013

Sheikh Ponda Yuko Muhimbili Kwa Matibabu

Video Kwa Hisani ya Imma Mbuguni
Sheikh Ponda Akitibwa Jereha la Kupigwa Risasi Begani MuhimbiliKutoka: MICHARAZO MITUPU BLOG

Sheikh Ponda Issa Ponda ameletwa Dar na kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu na tayari kuna habari kwamba Polisi wakiwa kwenye madifenda yao wameshatimba hospitalini hapo.

MICHARAZO inafuatilia taarifa hizo zilizopenyezwa hivi punde kujua ukweli na ikiwezekana kuwatupia na picha kama ni kweli Sheikh huyo machachari na kiongozi wa umma wa waislam walio wengi amepelekwa hospitalini hapo.
Pia taarifa rasmi kuhusu hali ya Sheikh Ponda inatarajiwa kutolewa Alasiri hii katika Msikiti wa Mtambani na Amir wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha baada ya kuwepo kwa mkanganyiko juu ya hali ya kiongozi huyo wa umma wa waislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda juu ya tukio la kujeruhiwa kwa risasi begani na Polisi wakati alipotaka kukamatwa, japo Polisi wanaendelea kukomaa kwamba hawajui lolote.

Picha Kutoka Daily Mirror

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

17 comments:

JM said...

Muda si mrefu nimetoka kuongea na shuhuda mmoja aliyekuwepo Morogoro. Ni kweli kuwa Sheikh PONDA amejeruhiwa vibaya kwa RISASI.

Huu ni mwendelezo wa matukio ya kuwawinda viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari na wanaharakati ambao serikali inaamini ni watu hatari.
Hivi karibuni, taarifa za ndani za serikali zimekuwa zikimuonesha Sheikh Ponda kama mtu hatari kwa usalama wa taifa, huu ni upuuzi na ujinga mkuu ambao utatupeleka pabaya.

Ikiwa kuna mtu ni hatari sana kwa taifa, na serikali ina ushahidi, kwa nini isimfungulie mashtaka mtu huyo na ipeleke ushahidi huo mahakamani ili mahakama ipime na kuamua au la!

Serikali inayotumia “approach” (mbinu) ya kushambulia, kujeruhi kwa nia ya kuwaua watu wenye msimamo tofauti na serikali hiyo, hii inakuwa “serikali hatari, ya kijinga, dhaifu na iliyoshindwa kuongoza”, serikali ya namna hii “is more dangerous to the peace of the nation than the dangerous persons themselves” (serikali ya namna hii ni serikali hatari mno kwa amani ya taifa kuliko watu inaowadhania kuwa hatari”.

Mimi nachojua, Sheikh Ponda ni mwanaharakati wa kiislamu anayebeba matumaini, hoja na visheni ya waislamu walio wengi. Kwa upande mwingine serikali ya CCM inamuona Sheikh PONDA kama mtu hatari kwa sababu hoja na visheni zake vikifanikiwa vitawatoa waislamu chini ya BAKWATA ambayo inatumiwa na serikali ya CCM kama nyenzo ya kuwadhibiti waislamu katika masuala yao ya msingi na hata baadhi ya haki zao muhimu za kiimani.

Serikali yoyote ya kipuuzi na iliyokufa “a failed state” haifikiri namna ya kutafakari hoja zinazokinzana na serikali na kuzitafutia ufumbuzi mezani. Hufikiri kutumia nguvu, kuwatisha watoa hoja husika na hata kuwaua pale nafasi inapopatikana, ilimradi udhibiti “sensorship” uendelee.

Serikali mfu kama ya CCM huwasha kiberiti yenyewe na baadaye huhaha kuzima moto ikiwalaumu watu wengine kwa matatizo yaliyoanzishwa na serikali yenyewe.

Ikiwa viongozi tutachekelea unyama huu na kuacha fulani atambuliwe kama “mtu hatari sana” ATI kwa sababu tu yeye ni dini fulani, ni kweli mhusika atashughulikiwa ipasavyo, atateswa tutachekelea, ataumizwa tutasheherekea na atauawa tutapiga nderemo na vifijo.

Serikali mfu haitaishia hapo, ikimaliza kumshughulikia yeye kwa dini yake itahamia kwako, itakuita “mtu hatari sana” kwa sababu ya chama chako, kwa sababu ya uanaharakati wako, kwa sababu ya uandishi wako na kwa sababu ya msimamo na mtizamo wako ambao unapingana na serikali. Nani atabaki salama?

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “ukinywa damu ya mtu, utaendelea kunywa tu”. Nami nasema, tukichekelea na kukubali propaganda za CCM kuwa Sheikh Ponda ni mtu hatari sana, akishamalizwa watahamia kwetu(kwangu na kwako), mimi na wewe tutapewa “uhatari” na tutasakwa kwa mtutu wa bunduki tuuawe haraka ili taifa libaki kuwa salama.

JM said...

Serikali ya CCM iache mbinu hizi ambazo tulishazijua. Serikali ikatatue tatizo la msingi la MZOZO WA MIONGO KADHAA KATI YAKE NA WAISLAMU. CCM iwaache waislamu watafute uongozi wao huru kabisa, wanaouamini. Kufikiri ATI maoni ya waislamu yataendelea kusimamiwa, kuratibiwa na kuongozwa na BAKWATA ni kupoteza muda na kijidanganya. Mbona sisi wakristu tuna taasisi zetu muhimu na imara za kidini na tunaziamini? Kwa nini serikali ya CCM inaendelea kuwashika waislamu na kuwadhibiti kwa kuitumia taasisi ambayo waislamu hawaiamini?

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, pamekuwa na marais wawili ambao ni waumini wa dini ya kiislamu, Mzee Mwinyi na sasa Mhe. Kikwete, hawa ni waislamu kabisa, ina maana hawajui malalamiko ya waislamu ya miaka nenda rudi? Kama Kikwete na wenzie walichoshwa na mauaji yaliyokuwa yanaendelea Zanzibar na wakaamua kuwaacha wazanzibari waamue hatima yao na Leo imeundwa SUK. Kina Kikwete haohao wanashindwaje kusema matatizo ya waislamu sasa basi na wakawaachia waislamu huru waamue hatima yao, wawe na vyombo wanavyoviamini visimamie maslahi yao. Mwinyi na sasa Kikwete siyo waislamu? CCM ina maslahi gani BAKWATA?

Mtizamo wangu pia ni kwamba, waislamu wanaweza kuwa wanamalizana wao kwa wao bila kujua.

Pale Marekani kulikuwa na tatizo la msingi kwa wamarekani wengi wa kipato cha chini, huduma za afya zilikuwa kuzungumkuti. Sehemu kubwa ya waathirika wa jambo hili walikuwa wamarekani weusi. Marais wote wazungu waliopita hawakuwahi kufikiri kulitatua, alipopata nafasi Obama akalibainisha Suala la afya kwa wamarekani wa kipato cha chini kama tatizo la msingi linalohitaji utatuzi wa haraka. Obama akatengeneza muswada wa bima ya afya, akambana hadi ukawa sheria, Leo wamarekani wa kipato cha chini ambao wengi ni weusi wanafaidika na mpango huo. Obama alipigwa vijembe kuwa analeta muswada wa kuwapendelea watu weusi lakini aliwapuuza wapinzani wake, alijua anafanya jambo ambalo litaondoa mgawanyiko na ukosefu wa haki muhimu ambalo lingeisumbua Marekani ya baadaye.

Hapa kwetu tuna marais wanaonea haya dini zao na wanashindwa kutatua matatizo ya msingi ya kundi ambalo wameliishi na kuonja adha ya kero zao. Kuwaacha waislamu wajichagulie vyombo huru vya kujiongoza ni kuongeza na kupanua wigo wa demokrasia na uhuru muhimu kwa watanzania wote, hili halitakuwa na faida kwa waislamu peke yao, lina faida kwa nchi nzima. Ni bora rais uitwe mdini kwa kuondoa udhibiti wa chama chako kwa taasisi ya kidini na kuiacha huru kuliko kuacha mifarakano na malalamiko ya kundi linalodhaniwa linaonewa kwa miongo kadhaa yaendelee.

Mimi nadhani waislamu wana matatizo ya msingi kati yao, panahitajika viongozi imara wanaoliona hilo. Ikiwa yataachwa au kushughulikiwa kwa mtindo huu wa kuvizia na kupiga RISASI wale wanaotetea maslahi halisi ya waislamu, hayatakwisha.

Ikiwa atauawa Ponda mmoja eti kwa sababu anadhaniwa kuwa “mtu hatari”, in the next morning watazaliwa Ponda wengine hatari zaidi wapatao 1000. Uhuru wa Dokta hauzimwi kwa RISASI.
Sote bila kujali itikadi zetu za kidini, kisiasa na kimtizamo, TULAANI KWA NGUVU UNYAMA ALIOFANYIWA SHEIKH PONDA.

Shuhuda said...

Kweli nimeshindwa kuamini kilichotoke, sheikh ponda kubigwa risasi. Nilikuwepo pale uwanjani tena nilikuja mapema kabisa na hivyo kushuhudia kila kitu kilichotokea.

Kimsingi sikuona sababu ya Sheikh Ponda kutokewa na tukio baya kiasi kileambacho hakionyeshi ubinaadamu kabisa, utu wetu, uhuru wetu na hata heshima tuliyonayo watanzania kwenye jumuia za kimataifa. Mpaka sasa haieleweki ni nani hasa kampiga risasi Sheikh Ponda, lakini minong'ono ya watu wanasema ni polisi wamehusika. Binafsi pamoja na kufuatilia kwa ukaribu sikuona ilikotokea risasi hata aliyepiga na nilikuwa mbali kidogo na tukio. Ila nilimwona wakati anapandishwa kwenye pikipiki akiwa tayari amekwisha kupigwa risasi. Imewahuzunisha wengi!

Jamaa ameongea kwa muda mfupi sana ni takribani dakika 18, kwani alianza kuongea saa 11:54 na alimaliza kuongea saa 12:12 jioni. Hali ya uwanjani kwakweli ilikuwa shwari sana, hata polisi hawakuonekana jirani walikuwa kwa nyuma kabisa huku wakiwa wamejisheheni kwa zana zote za kazi.

Mara baada ya ponda kukaribia kumaliza kuongea alisema kuwa muda hautoshi isipokuwa ilitangaza kuwa kesho baada ya swala ya adhuhuri atakuwa kwenye msikiti wa mkoa wa morogoro wa Boma road ambapo ataongea kwa kirefu hivyo kuwataka waislamu kesho kuhudhuria Boma road.

Inavyooneka polisi walipanga wamkamate hata kabla ya kuongea katika ule mkutano na ndio maana walitega sehemu kana kwamba walikuwa wakimsubiri aingie wamkate. Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi Sheikh Ponda iliingia uwanjani kupitia upande wa pili ambapo msafara wake ulikuwa na gari moja tu na taksi mbayambaya kiasi kwamba wala huwezi kudhania. Mara tunashangaa gari imesimaa na Sheikh Ponda na Amiri wa wahadhiri Tanzania Sheikh Kondo Bungo wakashuka,wakapita kwenye kundi la waislam kwa nyuma ghafla kivumo cha shangwe na Takbir kikavuma huku umati wa waislam waliohudhuria hapo ukiitia allahu akbar, allahu akbar nk.

Sheikh Ponda mara baada ya kumaliza kuongea, watu wakaanza kutawanyika, lkn ghafla mwendesha shughuli akatangaza waislam wasitawanyike kwanza kwa kuwa kulikuwa na matangazo.Wakati matangazo yanendelea ambayo sikuweza kuyasikia , ghafla tukaona defenda moja ya polisi inaingia ambayo ilikuwa imejaza polisi walio tayari kwa mapambano. Waislam wakawa wanawashanga kulikoni tena ilhali mkutano ulifanyika na kuisha kwa amani kabisa.

Basi Sheikh Ponda akaingizwa kwenye taxi iliyokuja kumfuata akiambatana na Sheikh Kondo Bonge. Polisi walitaka kumkamata sheikh Ponda lakini waumini wakamkinga kwa kulizingira gari alilopanda sheikh Ponda huku likiondoka taratibu. Huku nyuma gari la polisi likawa linafuata taratibu bila kubiga risasi hewani wala kupiga mabomu ya machozi. Gari ya polisi ilipofika barabara ya lami maeneo ya karibu na jengo la Fire ilionekana kusima kwa muda huko gari iliyombeba sheikh Ponda kukunja kushoto kueleke kwenye msikiti wa Mungu mmoja dini moja. Kabla msafara wa Ponda haujafika kokote gari nne za polisi zilikuja kwa kasi sana na kuanza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya waumini, watu walitawanyika na Sheikh Ponda akashuka na kuelekea kwenye Gereji moja hivi kabla ya kufika idara ya maji ambako ndiko alikopigwa risasi. Kwakweli sijui ilikotoke risasi iliyompiga Ponda, nadhani kamanda wa polisi atalitolea ufafanuzi zaidi. Mimi nimeandika kile nilichoona kwa macho yangu!

Mi nilidhani ingekuwa busara kwa jeshi la polisi kama walimuhitaji sheikh ponda wangemwambia anahitajika polisi na hivyo ajisalimishe.

Anonymous said...

Japo namchukia Issa Ponda sifurahii hata kidogo kama amepigwa risasi na polisi. Huyu mtu ilitosha kumuweka lupango kwani alipatikana na kosa la uchochezi ila dola ikamuachia na yeye kuendelea na kile asichoweza kuacha..."uchochezi wa kidini'

Anonymous said...

serikali inaimba kila siku amani amani tudumishe amani lakini kwa umbande wa pili serikali ndo ya kwanza kuvuruga amani!

Anonymous said...

Hivi huyu ponda ni nani hasa tanzania na anamwakilisha mwislamu gani huyu hata adekezwe namna hii. anapata umaarufu wa bure kwa kuachwa huru wakati akitenda jinai. polisi acheni utani na amani ya nchi mtu kama ni wanted anaachiwaje apande jukwaani kisha ajichome kisu mwenyewe aseme kapigwa risasi. huyu ana ajenda toka rwanda ambako inasemekana ni kwao na pia wanahabari wa kimataifa wote ni wanyarwanda ndio maana kila baya wanalishobokea. anayebisha afuatilie kazi za mwandishi wa AFP aliyeko arusha anayeandika kwa kifaransa na kutupakazia sana. asipotupiwa macho tumeumia. na kama hana work permit na aondoke zake kama wenzie wa karagwe

Anonymous said...

kwao Burundi kwani siri si wamezoea kuwana kule kwani nani asiyejua, wamekimbilia nchi mbali mbali kuomba hifadhi sas antataka ayalete mambo ya kwao hapa, hatutaki kwa kupitia udini this is so bad! Serikali Wamvue uraia wa Tanzania na arudishwa kwao! Fujo zake hatutaki tunataka Amani!

Anonymous said...

Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana kumchukia yule anayetuelekeza tufanye mambo mema. Lakini swali linabakia, inakuwaje apewe hukumu mbaya namna hii kwa kuwa na malengo mazuri hivi? Inawezekana malengo mazuri namna hii ya Sheikh Ponda yanakinzana SANA na yale ya Bakwata? Kwa nini basi Sheikh Ponda asisajili taasisi tuiite labda 'Sheikh Ponda Foundation' ili shughuli zake ziwe wazi zaidi? Of course msururu wa maswali ni mrefu hasa hasa kufuatia utetezi anaopewa Sheikh Ponda dhidi ya shutuma mbaya dhidi yake. Mashaka niliyonayo ni huenda Sheikh Ponda ana sura zaidi ya moja kiasi kwamba anaonekana ni hatari kwa dola. Basi wanahabari (ambao baadhi yao Ludo hawakubali) wafanye uchunguzi huru kuhusu Sheikh Ponda ili hatimaye watueleweshe Watanzania kuhusu Sheikh Ponda ni nani, anafanya nini na ndoto zake kuhusu Tanzania na Watanzania ni nini. Pengine tuanzie hapo

Anonymous said...

,mimi nimeishi na hyu mtu,wewe unasema una rekodi zake.watuhumiwa wa kesi ya kuchoma makanisa mbagala pia nimeishi nao pale segerea.Ponda binafsi aliguswa na tatizo la maji kwa wafungwa na mahabusu,na alipotoka akatoa msaada wa kujenga kisima cha maji safi.nakuuliza tena sisi watetezi wa wanyonge na tunaopiga kelele juu ya haki za mahabusu,kiasi cha kuitwa au kujiita prison graduate,tumefanya nini zaidi ya kusifia magereza kuwa ni mahala pazuri kabisa kwa maisha.ni kama nchi fulani.kwa hili moja sisi na shehe ponda ni nani mwenye maana kwa jamii ya wateseka kama magereza?

Anonymous said...


Nazidi kuchanganyikiwa, chanzo cha mkasa huu ni vurugu kwenye mhadhara Morogoro au kuhusika na tukio la Zanzibar?

Anonymous said...

Tukio hili limenikumbusha mauaji ya kikatili ya Sheikh Abou Rogo yaliyotokea Mombasa, Kenya mwaka jana. Sheikh Rogo alipigwa risasi kadhaa wakati akiendesha gari kumpeleka baba mkwe wake hospitali akiambatana na mkewe. Rogo alikuwa anahusishwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la al qaeda na al shabaab pia alikuwa ni muhimili muhimu katika madai ya Jamhuri ya Mombasa.

Anonymous said...

Kwani nini kitu kinachofanyika hapa nchini kinahusishwa na CCM? Kila tukio linakua politicized hata bila kujua background ya kilichotokea jamani!!!! Bwn. Julius mm sio mwanasiasa wala mwanaharakati wa aina yoyote kwa hiyo napenda tujaribu kupata taarifa ambazo hazina upendeleo wa upande wwt ili tulaani au vinginevyo. Pia tungeacha siasa katika kila tukio

Anonymous said...

Huenda Sheikh Ponda katembea na mke wa mtu! Labda hii haihusiani na siasa.

Jerry Springer said...

Serikali ijue kwamba serikali zote za kibabe hazijanufaisha wananchi wake na hazidumu,kama ponda ana makosa afunguliwe mashitaka sio kumpiga risasi,polisi wasiseme walipiga risasi juu kama wangepiga juu isingeweza kujeruhi mtu na kwa nini watumie risasi ya moto badala ya kutumia mabomu yao ya mchozi ingawa ya siku hizi yanaua,
lakini la msingi serikali jueni kuwa waislamu wanatakiwa kuwa na chombo chao huru sio kuwalazimisha waongozwe na Bakwata hata kama wenyewe wanaona hakuna maslahi kwa misingi ya dini yao,huwezi kuleta amani kwa kutumia bakwata jumuia ambao haina ridhaa ya waislamu ni chombo kinachotumiwa na serikali kuwabana waislamu kama wakristo wana jumia zao ambao wameridhika nazo kwa nini waislamu wasipewe nafasi ya kuunda jumuia yao kwa ajili ya maslahi yao.leo ponda kesho mwingine lakini tatizo haliwezi kwisha mpaka waislam wapate nafasi ya kuwa na umoja wao kwa maslahi yao!

Anonymous said...

SHEIKH ISSA PONDA NI MTU MBAYA YA NCHI YETU.

WANAVYOZIDI KUMWACHA ITAWAGHARIMU SANA SERIKALI NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA.

HAKUNA SIRI KABISA HUYU NI ANAENEZA CHUKI ZA KIDINI

ANAFAA AKAMATWE NA ASIACHILIWE KABISA

Anonymous said...

Watanzania jamani tusifuate mikumbo ambayo haina faida kwenye nchi yetu,naiomba serikali imchunguze huyu PONDA na kama ci raia wa Tanzania basi apewe masaa 24 ili atoke kwenye hii nchi,nakama atakua Mtanzania bc serikali imzibiti vilivyo huyu PONDA la sivyo mtu huyu atasababisha mauwaji ya wanachi wasio na hatia,why mtu mmoja tu atuponze sisi sote,na kama alikua katika KIFUNGO cha NNJE kwann afanye haya yote? Hii nikuonyesha ameidharau MAHAKAMA,POLISI,USARAMA WA TAIFA na SERIKALI kiujumla,jamani hivi serikali wapi inatupeleka? Nakuombeni wadau wenzangu mnisaidie kwahilo,,naitwa mdudu KAKAKUONA mm nailinda nchi yangu na kuipenda pia je vipi? Wenzangu nyie,asanteni nawapendeni wote watz,

Anonymous said...

Tory MP Bill Cash, who sits on the All-Party Parliamentary Group for Tanzania, has urged the Foreign Office to further upgrade its travel warning for tourists visiting both Zanzibar and Tanzania because it was 'more than just an ordinary criminal event'.
The Foreign Office updated its Tanzania travel advice page on Friday with details of the attack and warns British nationals to 'take care' and read its travel advice.