Tuesday, June 12, 2007

Marudio - OmbaOmba


Leo nimeona nirudie topiki ya ombaomba hapa Boston. Nikitokea South Station kwenye subway leo asubuhi kuna ombaimba fulani anaitwa Gus, alikasirika na kutupa hela kwenye sidewalk. (Kisa alipewa pennies (senti moja moja). Huyo Gus amekaa pale miaka na miaka zaidi ya miaka 15. Kila siku hakosi, wakati wa Lunch makao yake ni Federal Street. Wikiendi anazunuguka kwenye subway siku nzima, kula kwake ni pale Food Court ya South Station. Hizo pennies alizopewa na huyo mzungu mwanamke zilikuwa anyingi kidogo, basi kazitupa chini kwa hasira. Kazoea noti.

Nashangaa sana. Hao si wanasema wanataka spare change? Lakini ukiwapa na hazitoshi wanatupa chini kama kukutukana. Hao ombaomba wana viwango vyao na kama huna usiwape chochote. Mara nyingi wanakuwa na hela kuliko wewe mfukoni.

****************************************************************
From: December 31, 2005

Hapa Boston kuna ombaomba kibao! Tena wengi ni wazungu. Hao ombaomba wengi wao ni walevi na watumia madawa y kulevya na wenye ugonjwa wa akili. Miaka nenda, miaka rudi, ombaomba ni hao hao!Unapita njiani, unasikia “Spare Change”! Utaona mtu kasimama na kikombe chake anakitikisa. Kuna wengine usipowapa kitu wanakutukana matusi ya nguoni.

Halafu kuna wale wakali wanakufuata mpaka ndani ya ATM. Basi watu kwa uoga wanatoa walichonacho na kuwapa kwa kuhofiwa kupigwa au kuibiwa. Haya, lakini ni lazima niongelee kitu ambacho nimeona, na labda wengine hapa USA mmeona. Kuna ubaguzi katika kile watu wanachotoa kwa ombaomba. Tuseme mtoaji ni mzungu, na ombaomba ni mweusi, basi kama atampa kitu anampa vichenji. Huyo huyo mzungu atatoa noti kwa ombaomba mzungu. Nimeshuhudia mara nyingi tu.

Nimeona ombaomba wa kizungu wakipewa noti za $1, $5, $10 na hata $20! Lakini mweusi atapewa vichenji, kwa nini? Je, ni kwa vile mzungu anajisikia vibaya kuona mzungu mwenzake katika hali hiyo, hivyo ni jitihada ya kumwinua? Je, ni kwa vile anaona kuwa mweusi ni hali ya kawaida kuwa maskini? Sijui kama tutaelewa sababu. Halafu utaona weusi wako tayari kutoa kwa yeyote. Atampa mzungu, atampa mweusi lakini mara nyingi nimeona weusi wakisaidia weusi wenzao kuliko mzungu. Kisa, anajua kuwa yule mzungu anaweza kuishi maisha mazuri akitaka maana Marekani maana bado kuna ubaguzi Marekani.

Lakini nisiseme kuwa wazungu wote ni wabaguzi, maana mwaka juzi kuna ombaomba Cambridge, anaitwa Ramsey, alikuwa amesimama pale Memorial Drive. Basi Mzungu jike tajiri kapita ndani ya gari yake ya fahari na kampa noti ya $100. Ndiyo kampa dola mia moja! Halafu mzungu kamwambia Merry Christmas, maana ilikuwa Christmas Eve. Lakini jambo kama hiyo kutokea ni bahati nasibu.Utaona wazungu wana jaribu kusaidia wazungu wenzao kupata public housing na huduma zingine. Lakini mweusi anaweza kupitwa. Kuna magari ya kuwasaidia zinapita mitaani, lakini hebu cheki, hao ‘volunteers’ wataenda kwa wazungu kwanza halafu mweusi ataambulia kilichobaki.

Ajabu na si kitu cha kushangaza sana ni kuwa hao ombaomba wa kizungu wakienda kuoga, ku-shave, kuchana nywele na kuvaa vizuri, anaweza kupata kazi kabla ya wewe mweusi na digrii zako!Na kama hamniamini ukipita barbarani tazama mwenyewe. Ngoja niishie kwa leo, na kwa maksudi sijaongelea habari ya welfare, na shelters maana hii blogu ingekuwa ndefu mno!

Nairobi Red Eye umeingia Tanzania Tena!




Nasikia ule ugonjwa wa 'Nairobi Red Eyes' (Conjuncivitis) umeingia tena Tanzania. Huo ugonjwa mbaya kweli maana unasambaa kirahisi sana. Wagonjwa walalamika kuwa ni kama vile kuwa kwenye michanga kwenye macho. Pia macho yanatoa machozi na tongotongo kwa wingi. Waznungu wanaiita 'pink eye'.
Jinsi pekee ya kuepukana nayo ni kunawa mikono kila mara, na usifikiche jicho/macho. Ukishake hands na mtu vijidiudu vinasambaa ukigusa alipogusa mwenye nacho pia unaweza kuambukizwa. Pia usi-share dawa ya macho ya mgonjwa.

Huo ugonjwa ulianza kuitwa Nairobi Red Eyes baada ya kuwa epidemic miaka ya 80. Haikukawia na ugonjwa huo ukaingia Dar es Salaam na kuwa epidemic. Ndo watu wakaanza kuita Nairobi Red Eyes kwa sababu waliona ilianzia Nairobi. Wakati ule maji shida, basi ilikuwa vigumu watu wanawe mikono kila mara, ndo ulikuta kila kona mtu mgonjwa, unamkwepa.
Kaeni Macho!

Monday, June 11, 2007

Kwa Heri Sopranos!



Sijui kama mlikuwa mashabiki wa Sopranos. Jana ilikuwa mwisho wa hiyo show. Na watengenezaji waliacha watazamaji kwenye mataa iliishia vipi. Walitumia Njia ya 'Fade to Black' kumaliza show. Kwa hiyo sisi watazamaji tubakie kujadili Sopranos iliisha vipi.

Mimi nimekuwa mshabiki wa Sopranos kama mwaka moja hivi. Nilikuwa nasikia watu wakiongea kuhusu Sopranos lakini wala sikutazama miaka yote hii. Ila nilianza kutazama kwenye reruns. Comcast wana On Demand, na uliweza kuonza Seasons zote. Kwa muda mfupi nilijua habari za Big Pussy, Christopher, akina Aprile na wengine.

Basi nikaanza kuzitama na kugundua kumbe Sopranos ni nzuri. Huyo Tony Soprano, japo ni mobster ana maisha na familia, na marafiki na watu wanaomwabuud na wanaomwogopa, na pia alikuwa amejaa ashki ya uzeeni. Episodes nyingi walimownyesha Tony akifanya mapenzi na wanawake wasio mke wake. Wengine waliweza kuwa hata umri wa binti yake, wazungu wanaiita 'mid life crisis'.

Lakini ilikuwa kila ukimzoea character, huyo anauliwa! Kifo nilichofurahia ni cha mshenzi Ralph, aliyeua fariai wa Tony Soprano. Ralph alikuwa kichaa anaua watu kwa kufurahia kweli. Kifo nilichosikitika kuona ni cha Bobby Bacala, wiki iliyopita. Huyo baba, alikuwa mpole na alikuwa anajali watu, lakini Tony alimlazimisha kwenda Canada kuua mtu. Bobbby aliuliwa kwenye Toy store.

Yule Baba mdogo wa Tony, Uncle Jr. jana walimwonyesha hana akili kabisa, zimefyatuka shauri ya ugonjwa wa Alzheimers. Na Silivio aliyekuwa concilieri (mshauri) wa Tony alipigwa risasi wiki iliyopita na sasa yuko kwenye coma.

Mtoto wa Tony A.J. maskini ya mungu, show ingendelea nadhani anefanikiwa kujiua. Tokea yule binti mDominica amwache amekuwa kama mwehu hivi. Na hata siku moja atakuwa katili kama baba yake.

Binti yake Tony, Meadow, naona atafanikiwa kimaisha. Anasomea sheria. Na inaelekea ataolewa na rafiki aliyekuwa anatembea naye kisirisiri.
Dada yake Tony, Janice, kawa binadamu alikuwa anajadili ataishaje na watoto wa marehemu mume wake, Bobby Bacala. Hao watoto wa Bobby ni yatima, maana mama yao alikufa kwenye ajali ya gari, ndo Bobby kamwoa Janice.
Paulie, yule mzee rafiki yake Tony mwenye nywele kama vampire, haachi kuchekesha. Jana kasema eti paka ni nyoka mwenye manyoya (fur). Kisa Tony katokea kumpenda paka wa mitaani. Ajabu huyo paka alipena kukaa na kulia mbele ya picha ya Christopher, aliyeuliwa na Tony. Je, roho ya Christopher imo ndani ya huyo paka?
Kuna mengi ya kusema kuhusu Sopranos, nadhani kwa vile imekuwa na washabiki wengi huenda wakatengeneza sinema za Sopranos. Na wakitengeneza mtasikia kuna Sopranos Movies hata 20!

Asante HBO kwa hadithi tamu ya The Sopranos.

Saturday, June 09, 2007

African Americans Remember their Slave Ancestors



Siku ya jumamozi, 6/9/07) waMarekani weusi walikumbuka mabibi na mababu zao walioibwa kutoka Afrika na kulazimishwa kuingia utumwani. Japo ni wachache waatakaohudhuria ni vizuri kuona wapo wenye moyo wa kukumbuka wahenga.

Watumwa waliteswa na kusihi maisha duni sana huko wakijenga taifa la Marekani. Shukurani yao ilikuwa ubaguzi ambao mapak leo weusi wanaiona Marekani.

Mungu awape nguvu na umoja.

****************************************************
June 9, 2007 CHARLESTON, S.C. (AP) -- Eighteen years ago, Tony Akeem organized a ceremony in New York City to honor the millions of Africans who died crossing the Atlantic during the slave trade. Similar observances have since spread around the world.

Today , offerings of water, honey and rum were to be poured along the shores of South Carolina and elsewhere for Middle Passage Remembrance Day. The remembrance is held the second Saturday in June.

"We must, we must, honor our ancestors," said Tony Akeem, who has been organizing an observance at Coney Island, N.Y., ever since a 1989 conference on the slave's brutal trip was held at Medgar Evers College in Brooklyn, N.Y., where he works as a photographer.

The observances have spread from Philadelphia to San Francisco and from Brazil to Ghana. Most were started by people who have attended the New York event, Akeem said.

Saturday marked the 10th year South Carolina was participating in the remembrance. As many as 100 people were expected at a Fort Moultrie dock on Sullivans Island near Charleston.
The first slaves arrived in Charleston in 1670, the same year the Carolina colony was created. Historians estimate nearly 40 percent of the millions of slaves brought to what became the United States passed through Charleston. Many others died at sea.

"The stories run pretty strong that there were people who realized they were enslaved and would rather drown than be enslaved and when allowed up on the decks, would just jump into the water," said Fran Norton of the Fort Sumter National Monument, which includes Fort Moultrie. "It commemorates those people who gave up their lives for freedom."

Just how many perished in the slave trade will never be known.

"We know that many died of disease because they were packed in the ships like sardines," said Osei Terry Chandler, a project director at a Charleston education facility who is helping organize the South Carolina memorial.

Participants at the ceremonies in New York and South Carolina planned to drizzle water, rum and honey into the waves Saturday. Some were to toss flowers into the coastal waters. Some were to beat drums.

"Pouring libations is simply to venerate your ancestors," said Bill Jones, who helps organize the Coney Island ceremony. "It gives the ancestors a cool drink of water, or a little bit of gin or a little bit of rum, whatever you pour the libation with.

"In African spirituality we believe we are in constant contact with our ancestors. They are not someplace in heaven, they are right here with us."

Mkenya yuko jela New Hampshire baada ya kutarisha maisha ya Mtoto!


MKenya Esther Ngari (20)anshsikiliwa na polisi, wa Nashua New Hampshire, kwa dhamana ya $50,000 baada ya kuhatarisha maisha ya mtoto aliyekuwa anamwangalia.
Esther alikuwa ana babysit watoto wadogo wawili, moja alikuwa na miezi 18 and mwenzake alikuwa na miezi sita tu. Hakujuana nao mpaka jana hiyo hiyo.
Sasa huyo mwenye miezi kumi na nane alienda chumbani kwake na kula vidoge vya Esther vya ugonjwa wa kifafa. Wakati huo Esther kalala. Angetoa taarifa mapema kuhusu tukio isingekuwa shida sana. Tatizo ni kuwa Esther alijua kuwa mtoto alimeza vidonge lakini hakusema kitu.
Baba wa watoto alikuja kuchukua wanae. Aliona kuwa mtoto anapata shida kukaa macho na pia alikuwa anashindwa kunyayua kichwa. Walivyofika nyumbani mtoto alianza kutapika ndo kapiga simu 9-11. Mtoto alikuwa hoi kiasi kuwa ilibidi apate MedFlight (ndege) hadi Children's Hospital Boston.

Madakatari wana wasiwasi kuwa huenda, ubongo, ini ,na moyo wa mtoto zimehairibiwa. Anasema kama Esther angesema mapema mtoto asingeugua kiasi hicho.
Polisi wanasema kisheria ilikuwa jukumu la esther kuhakisha kuwa mtoto hawezi kupata hizo dawa.
Kesi itakuwa mahakamani wiki ijayo, lakini kwa sasa vyombo vya habari vimerukia habari hizo. Esther amekuwa nchini Marekani kwa miezi mitano tu. Alikuja kama mwanafunzi. Aliwaambia polisi kuwa aliaacha mfuniko wa chupa ya dawa wazi kwa vile ilikuwa shida kuifungua. Hapa wanatengeneza vifuniko vya dawa, 'childproof' kusudi watoto washindwe kufungua.

Kwa habari zaidi someni:

Friday, June 08, 2007

Paris Hilton alie tu!








Binti tajiri na aliyeharibiwa kwa unasa, Paris Hilton, (26)amerudishwa jela huko Los Angeles, California.

Binti huyo anyejiona mrembo kuliko binadamu yeyote duniani na aliyezaliwa katika utajiri wa ukoo wa Hilton (Hilton Hotels), alitoka jela ghalfa siku ya Alhamisi, baada ya kukaa siku mbili tu alisababisha mzozo mkubwa kwenye vyombo vya habari Marekani.

Mchungaji Al Sharpton alisema, "Paris angekuwa ni mtu maskini, au mwanamke mweusi angekuwa bado yuko jela!" Ajabu watu wengi wanaopingana na mawazo ya Sharpton walikubaliana naye. Mweusi au maskini asingeweza kutoka jela Marekani kwa kusingizia atapata kichaa. Lazima pesa zilitembea.

Leo, Paris huko mahakamani kamlilia mama yake kama mtoto mdogo. Kama vile kusema "mama hebu walipe hao wapuuzi waniachie".

Alivyotoka jela Alhamisi ilikuwa amalizie kifungo chake nyumbani kwake. Nyumba enyewe ni ya kifahari kweli kweli. Na ilikuwa avae bangili kwenye mguu kusudi polisi wajue yuko wapi wakati wote. Ilikuwa akae siku 23, lakini hata tau hakufisha, huyooo, nyumbani!

Kisa cha Paris kuonja jela ni hivi, Septemba mwaka jana alikamtwa akiendesha gari amelewa. Alipewa probation ya miezi 36 and fine ya $1,500. Baada ya hapo alikamatwa mara mbili akiendesha gari bila leseni. Alisema eti hakujua kuwa leseni yake imesimamishwa kwa muda.

Jumatatu alivyoenda jela baada ya kwenda kwenye party ya matajiri, wanasema alikataa kula chakula cha jela na alikataa kulala. Haya yeye kazoea kula kweli mahoteli na restaurants za bei mbaya, chakula cha jela hakiwezi kwa sasa. Lakini nasema akishikwa na njaa atakula tu.

Jaji amemrudisha jela leo na atakaa sentensi yake ya awali ya siku 45. Alikuwa amepunguziwa hadi siku 23, lakini baada ya upuuzi huo kutoea jana Jaji kasema apate fundisho. Awe mfano kwa matajiri wengine Marekani, maana inaelekea matajiri wana sheria yao na maskini wana sheria yao!

Thursday, June 07, 2007

Mheshimiwa Sumaye Atoa Shukrani kwa WaTanzania New England



Mheshimiwa Sumaye na mke wake Esther wakifungua densi.

Leo aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi, mheshimwa Frederick Sumaye, amemaliza masomo yake na kuhutimu shahada ya juu ya Masters of Public Administration kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, John F. Kennedy School of Government mjini Cambridge, Massachusetts, USA.

Mheshimiwa Sumaye alitoa shukurani kwa WaTanzania waliomsaidia akiwa masomoni. Alisema kuwa maisha yake chuoni Marekani yamekuwa tofauti na maisha aliyozoea Tanzania ya kuwa na wahudumu, walinzi, wapishi nk. Alisema alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na alikuwa anajipikia, kujifulia, kufanya usafi na kubeba backpack ya vitabu kwenda darasani. Pia alikuwa na homework kibao na mwanzo aliona ni kazi kweli lakini alizoea.

Alicheskesha watu alivyosema kuwa Tanzania alizoea kuitwa 'Mheshimiwa' lakini hapa USA hata mtoto mdogo anamwita, Fred.

Alitoa shukurani kwa waKenya pia waliomsaidia.

Sherehe kabambe iliandaliwa na waTanzania chuoni Harvard ya kumpongeza mhesimiwa Sumaye kwa kuhitimu masomo yake. Sherehe ilihudhuriwa na waKenya, waGanda, waGhana, na waNigeria, na wazungu kadhaa pia.

Mhesmiwa Sumaye anatarajia kurejea Tanzania hivi karibuni.

Wednesday, June 06, 2007

Mjue Mtunzi Sandra A. Mushi



Sandra A. Mushi, ni mwandishi na mtunzi wa kiTanzania. Anajitahidi sana kuandika mashairi, na hadithi za kusisimua. Pia ameandika novels.


Hii ni moja ya mashairi yake:

THE MOMENTS
Remember all the moments for two ...
Attraction
Relaxation
Communication
Stimulation
You used to be my masseuse
You used to be my boo
And much more
But after the diamond ring
You stopped lighting candles and using oils too
Can’t remember the last time we had a hot thing
You used to be my fashion model
You used to be my beauty queen
And much more
But after the white veil on the aisle
You just wear a bath robe and drinking Gin
Can’t remember when you last used a nail file
You used to be my madam
You used to be my whore
And much more
But after the baby
You locked away the toys
and I’ve become a bore
Can’t remember when we last touched, now an ice cold lady
You used to be my dance partner
You used to be my date
And much more
But after the buying the house
You now only get me a beer, TV dinner and a cold plate
Can't remember the last time we went out, a subject I can't rouse
You had that feminine thing going,
Smelt like wild flowers from the Serengeti,

It would turn me on just to see you
Walk into a room
Across the room
Out of the room
Soft, round and proud

You had that serene thing going

Tasted like nectar from the Zanzibar,

It would put a smile on my face just to hear your voice
Speaking
Laughing
Smiling
Fiery, sweet and exotic

The girl next door, with me she has been flirting
My secretary, to me sexy jokes she has been emailing
Your best friend, to me she has been listening
Your sister, with me she has been smiling
The girls next door, wears black like you used to
My secretary, has ginger dreadlocks like you used to
Your best friend, wears the perfume you used to
Your sister, wears the ethnic jewel that you don’t wear
no more
Remember the moments for more than two ...
Hesitation
Attention
Temptation
Situations


Copyright © Sandra A. Mushi All Rights Reserved



http://www.authorsden.com/sandraamushi


http://authorsden.com/visit/viewpoetry_all.asp?Authorid=28003

Tuesday, June 05, 2007

Tangazo


Naomba wasomaji wa blog hii waelewe kuwa blogu yangu siyo journalism, Hakuna editor (Mhariri), na wala si hoji interview na kuandika habari hapa, sina ratiba maalum ya kuandika na wala silipwi. Hii Blogu ni maoni yangu na naandika na kuposti kwa wakati wangu. Na wala habari zinazoandikwa hapa haziwezi ku-qualify kupata award ya journalism, bali zinaweza kupata award ya blogging. Mtu yeyote anaweza kuanzisha blogu yake mwenyewe… hakuna qualifications zaidi ya kujua kuandikia, kusoma na kutumia internet. Asanteni.

Ukiumwa malaria Marekani!


Umewahi kuugua malaria Marekani? Usiombe maana ugonjwa ambao unatibika Bongo, inaweza kukuua hapa. Bora uje na dawa kutoka Bongo kabisa.

Hapa USA hawaelewi kabisa malaria ni ugonjwa wa aina gani. Nawambia huwezi kuipata kupitia kwenye hewa. Nikawaambia kuwa Afrika, m ugonjwa wa malaria ni common vile ugonjwa wa mafua hapa. Watu wengi tu wanapata. Nawaambia inaambukizwa na mbu, tena anopheles mosquito. Hapa Marekani hamna. Kuna siku niliwaambia watu weusi na wazungu wa hapa kuwa niliuugua malaria sana nikiwa Tanzania, wakanitazama kwa mshangao na woga. Utadhani walikuwa wanamtazama Frankenstein yule monster wa kwenye masinema!

Nafahamu wazungu kama wanne ambao wamekufa nao hapa. Kisa madaktari hawakujua wanaumwa nini. Wali safiri nchi zenye malaria na kuugua baada ya kurudi. Pia mara nyingi madatari wa Marekani hawa uzoefu na huo ugonjwa ambao Tanzania ni kama kuugua mafua hapa.

Kuna MBongo kanisimulia kuhusu alivyokuja tu kutoka Bongo miaka ya 80, New York. Anasema alianza kujisikia vibaya na akaenda clinic. Kamwambia daktari kuwa anadhani ana malaria, maana katoka Tanzania hivi karibuni. Heh! Kosa kubwa. Kajaza fomu kwenda CDC (Center for Disease Control). Anasema manesi walikuwa wanamwogopa. Wakawa wanauliza kama wanaweza kuambukizwa. Anasema daktari hakuwahi kutibu malaria na ilibidi angalie kwenye kitabu na kumwandikia prescription ya quinine! Damu ilipimwa na ilichukua siku tatu kupata majibu. Haikuisha hapo, anasema alivyofika nyumbani katembelewa na health officer wa serikali. Wakamwuliza maswali mia kidogo mpaka kaogopa kuwa atarudiishwa Tanzania.

Bahati nzuri haikuwa na malaria wakaacha kumsumbua.

Lakini hivi karibuni kuna jamaa alienda Tanzania, karudi na malaria. Akashindwa kwenda kazini , alichukua siku mbili off na kupiga simu kuwa amerudi kutoka safari lakini anaumwa. Alivyoenda kazini, bosi kamwuliza alikuwa anaumwa nini, jamaa kamwambia, alikuwa na malaria. Heh! Utadhani jamaa alimwambia anaumwa Ebola virus. Jamaa alifukuzwa kazi. Nikamwambia bora ungemwambia unflu au UKIMWI, kulikoni umwambie kuwa una malaria.

Na kuna dada fulani naye aliuugua, tena alipata attack ya kusikia baridi na kutetemeka akiwa kazini. Kazi aliyokuwa anafanya ni ya kuangalia wazee. Huyo alikuwa na bahati walimpa paid leave ya wiki tatu! Lakini aliniambia kuwa alijuta kwa nini aliwaambia maana watu walikuwa kama wanamwogopa.

Naona siku hizi mambo kidogo afadhali, maana kuna tropical disease experts wengi. Wengine walifanya practicals kwenye mahospitali za Afrika na hata Tanzania. Lakini ukimkosa mtaalamu wa kukutibu, Mungu akulinde.

Karibuni mtoe maoni yenu au story zenu za malaria Marekani.

Saturday, June 02, 2007

Marudio - Ulafi wa bia Haipendezi Marekani


Orignally Posted: Tuesday, March 28, 2006


*************************************************************************

Ulafi wa Bia Haipendezi Marekani!Hivi majuzi nilienda kwenye ‘Party’ ya waBongo hapa Boston. Party ilifanyika kwenye basement ya nyumba. Na kama kawaida waBongo walijaa. Na kama kawaida chakula kilikuwa kingi na vinywaji tele. Kwa ‘Party’ waBongo ndo wenyewe maana wanachanga bia na chakula bia shida. Huyo anakuja na kesi ya bia, yule anakuja na kesi, yule anakuja na tray ya mapochopocho, mambo swafi kabisa!

Basi kuna MBongo kashuka kwenye ndege juzi juzi, alikuwa kalala kwenye Lawn Chair ndefu anastarehe huko akipunga upepo wa USA. Jamaa kalala kwenye hiyo lawn chair tena bila wasiwasi wowote, huko anaongea na watu. Nikamcheki, jamaa kalegea kabisa na kikofia kichwani anakula maisha ya USA. Basi chini ya hiyo Lawn Chair alikusanya kama chupa kumi za Heineken.

Nikasogea kwa huyo jamaa kumcheki, kama ni mzima au taira au nini, au labda mtu hajiwezi, ndo maana kalala hivyo. Kuongea na jamaa nikakukuta ni mzima kabisa. Basi nikamwuliza sababu ya kulundika mabia chini ya kiti wakati ziko tele jikoni. Na nikamwuliza kama hapendi bia baridi maana kuziweka chini ya kiti zinapata joto. Nikamwambia jamaa kuwa ni mshamba na anajiaibisha.

Jamaa kabisha kasema yeye ana bia tele chini ya kiti atakuwaje mshamba na hawezi kujiaibisha. Hakuwa na habari kabisa kuwa wageni waliokuwepo walikuwa wanamsema chini chini. Lakini jamaa hakujali maana kajiona kafika! Tena kafika USA.

Nadhani watu wangemwona kafika kama hizo bia kununua yeye, na hiyo nyumba ilikuwa yake.

Kwa kweli tabia zingine za Bongo tunaweza kuziacha Bongo. Maana nakumbuka kwenda kwenye shughuli mbalimbali Bongo, na kuona watu wanakusanya bia chini ya kiti. Hiyo kukusanya bia chini ya kiti watu walikuwa wanafanya wakidhania bia zitaisha. At least walikuwa na akiba na rafiki akija wana kitu cha kumpa. Halafu ilikuwa ni sifa kuonyesha kuwa una hela ya kununua bia zote hizo.
Hapa USA karibu kila mahala kuna liquor store na kuna bia tele. Hela yako tu. Na kwenye party za waBongo hata siku moja sijawahi kusikia bia zimeisha, au zikiisha basi watu wanaenda kununua zingine.Jamani eh, tabisa zingine zinafaa ziachwe huko Bongo. Mnasemaje?

Designer Mustafa Hassanali ajibu hoja za Michuzi blog


Wapendwa wasomaji, kule kwa Michuzi, watu walikuwa wanaongelea sana juu ya nguo alizovaa Flaviana Matata, kwenye mashindao ya Miss Universe. Hasa designer Mustafa Hassanali alitajwa sana.


Sasa kampuni yake imefanya Public Relations na kujibu hoja waliozotoa wasomaji kule. Kweli blogu ya Michuzi imekuwa nzito kuliko site yoyote ya waTanzania.

Photo (Designer Mustafa Hassanali poses with model and Former Miss Tanzania, Nancy Sumary pic from Michuzi Blog)
***********************************************************************************

PRESS RELEASE Dated 1 June 2007
FLAVIANA'S WARDROBE SAGA


First and foremost, we at Mustafa Hassanali Couture would like to congratulate Ms Flaviana Matata for performing well at the Miss Universe Pageant which is attributed to the young girl’s zeal, zest and support from her organisers, sponsors and the people who voted for her. Flaviana prior to being a Miss Universe Tanzania 2007 had an opportunity to be cast to showcase our “Namaste” Collection in January 2007.

Pictures of that Show were published in Issa Michuzi Blog amongst many others. Since May 28 2007, the finals of the Miss Universe pageant, The Issa Michuzi Blog has been flooded with comments, remarks, feedbacks and allegation in regards to the Her Wardrobe, this has been intensified more so, since her arrival back from Mexico.

Mustafa Hassanali would like to clarify, refute and abstain from the following remarks:“bora wangempa deal hassanali ila waliogopa bei si unajua these stingy idiots hu just think of themselves....”
we Appreciate that, the Anonymous, thought of us…. But we would want to make clear, we design, create, construct and embellish as per the clients budget. All good and quality product does come with a price tag. “The biggest hindrance to creativity is budgets” Mustafa Hassanali“

Hivi kaka Michu,gauni lile"jeupe"ambalo hasa ndilo lilitukosesha sisi watz ushindi kwa"mwanamke wetu Flaviana"lilitengenezwa na"designer"wa kitz Hassanali au?? Kama Hassanali ndiye alilitengeneza gauni lile"baya"adhabu yake ni kupigwa bakora hadharani,manake halikutoa kabisa dada yetulets me know kaka Michu,nani hasa alitupokonya ubingwa huu kwa kutumia hila ya kumpa auni baya"jeupe "dada yetu?”

We hereby attest that Ms Flaviana Matata On stage evening gown, Official National Costume, Bikini, Pre-final rehearsal segment gown and her welcome home gown were NOT A MUSTAFA HASSANALI CREATION. Each designer has its own creative IQ which makes that their selling point. We respect it.

As they say “one mans meat is another mans poison” Kwa Kiswahili “Mkia was Nguruwe………….”“michuzi hakuna uzalendo wa kijinga tena la sivyo tutaacha kufagilia, wabunifu wa kibongo hawajafikia viwango kwa hiyo hakuna kuvaa nguo zao kwenye mashindano ya kimataifa la sivyo itakuwa aibu tu, vaeni nguo zao hukohuko bongo mkishatoka mnavaa nguo zenye mvuto zilizo kwenye international standardkwa lile gauni hata kumi bora wamempa sababu alikuwa unique and creative on her own beauty”

we @ Mustafa Hassanali would like to inform the person who wrote this comment, That fashion designers just like other professionals have their Identity. I would like to enlighten the said person that its passion for our work, just like the rest of you, drives us for our daily livelihood. As they Say Charity Begins at Home, Ailinda Sawe of Afrika Sana is a Professional Designer and one of the first in Tanzania with a Degree.

Ally Rhemtullah is another qualified designer from USA whilst Elly Mlaki studied in UK. The Late Kiiza Kahama studied in Paris. We Have So many professional DESIGNERS in Tanzania some who are trained and others are Qualified by Experience.

“Hivi ni nani aliye-design Night Gown yake?? Lile Gown lilikuwa baya kusema ukweli. Jamani Tanzania Designers wengi wabovu sana yaani hata tungemnunulia nguo kutoka Walmart angependeza sana kuliko lile gown baya. Angekuwa na Gown bomba angeweza kushinda. Lakini hata hivyo hongera sana Flaviana Matata.”

As stated Earlier that it was NOT A MUSTAFA HASSANALI.What Ms Flaviana Matata Wore during the pageant, had nothing to do with the Qualification status of designers in “Bongo” but its entire her own judgement, she is above 18yrs old, and that of her Organisation Miss Tanzania Universe.Mustafa Hassanali did design two over the Top Evening Gowns for Miss Flaviana Matata as her personal wardrobe which was commissioned and paid for by Flaviana personally.

ABOUT MUSTAFA HASSANALI COUTURE

Mustafa Hassanali Couture is renowned for its elegance, style, flamboyancy, glamour and glitz that has made it one of the most sought after fashion house in TanzaniaHaving been showcased throughout South, Central, Eastern Africa and Italy, this has influenced his cosmopolitan approach to the world of Fashion in Tanzania. It is his exquisite handwork, detailed beadwork and creative ensemble embellishments that make its designs alive. Whether it’s the corporate wear, Traditional costumes or a Wedding Ensemble… Mustafa Hassanali handles each piece with great care and gives the utmost attention to whole outfit right from first client contact to delivery, a personal touch all through.

True to its policy, each design and Outfit is a masterpiece of work…. A duplicate is NEVER created.That is what makes it unique, a Truly Mustafa Hassanali Affair.
Issued By:press@mustafahassanali.netTel: +255-71-5303880
P.O.BOX 10684 DAR ES SALAAMTANZANIATel: +255-78-4303880+255-22-2668555E-mail: press@mustafahassanali.netURL: http://www.mustafahassanali.net

Thursday, May 31, 2007

Jeff Koinange afukuzwa kazi CNN


Photo from CNN.com

Leo nimesikia habari za kusikitisha kweli. Jeff Koinange, amefukuzwa kazi CNN. Wanasema kuwa mwanamke aliyemtaka kamfanyia mbaya. Haya. Kweli wamepoteza mwandishi aliyejua Africa, na aliyetoa habari za kuaminika. Ni vizuri kuona mwafrika mweusi anaongelea habari za Africa na siyo mzungu. Kweli wamepata hasara na kama kafukuzwa shauri ya mwanamke ni hasara kwa CNN.
Huyo mwanamke anakataa kuwa yeye ndiye alisababisha afukuzwe. Soma habari zake na e-mail walizokuwa wanatumana hapa:

Monday, May 28, 2007

Flaviana afika Top Ten - Miss Japan ashinda!






Kwanza nampongeza Miss Tanzania, Flaviana, Matata kwa kufika katika Top Ten (kumi bora) ya mashindano ya Miss Universe. Ingawa hakufika katika Top 5 atafika mbali maana mabilioni ya watu wamemwona. Pole zake Miss USA, alianguka jukwaani kwenye evening gown segment.

Nilijua Miss Japan atashinda. Alivyopita na swimsuit yake alivyokuwa anatingisha matako, kwa swing, macho yote yalikuwa kwake. Flaviana alivyovaa ili bikini niliona kama ana aibu fulani, bora angetembea kama anacheza ngoma watu wangemshangilia. Flaviana alijitahidi sana lakini kuna wakati niliona kama alikuwa nervous hasa pale kwenye Evening gown, na hata mwanzo walivyokuwa 77 na alikuwa jukwaani.

Lakini kunyoa kipara kilimsaidia kwa kiasi fulani, ila ingekuwa vigumu ashinde awe Miss universe maana moja wa wadhamini wakuu ni kampuni inayotengeneza manukato ya nywele. Miss Jamaica naye alishindana na nywele za rasta.

Lakini leo jioni waTanzania tuliweza kujivunia si mchezo, maana ni mara ya kwanza kuona Miss Tanzani anafika mbali kiasi hicho katika hayo mashindano. Naomba Flaviana akirudi Tanzania afundishe na atoe ushauri kwa wasichana wengine kuhusu jinsi ya kushiriki katika hayo mashindao na kushinda.

Natumaini Trump Model Agency watampa contract.

Good Luck Flaviana! -

(Miss Tanzania Flaviana Matata akipiga pozi na Miss Italy na Miss Nigeria. Photo from Michuzi Blog)

Msisahau kutazama mashindano ya Miss Universe leo jioni. Flaviana anasifiwa kweli, hasa kwa vile amenyoa kipara na anajiita 'natural African woman'.

Kwa habari na picha zaidi nenda:

http://tv.yahoo.com/miss-universe-2007/show/41744/photos/1

http://www.elpasotimes.com/entertainment/ci_6006480

Saturday, May 26, 2007

Umecheza Slots?


Hivi karibuni nilienda kwenye Casino cha Foxwoods, huko Connecticut na nilicheza na hizo slots. Usipokuwa mwangalifu inakula hela yako. Kama unabahati unarudi na kibunda. Niliona watu wakipata vibunda lakini wanarudishia casino!

Kila mtu na bahati yake lakini!

Bongowood





Katika dunia ya sinema, mfalme na wa kuiga ni Hollywood. Maelfu ya sinema zimetengenezwa na Hollywood tokea miaka ya 1910's. Lakini siku kila kona ya dunia sinema zinatengeneawa. Wahindi wana Bollywood na waNigeria wana Nollywood. Sasa sisi waTanzania tuna Bongowood.

Ndiyo, tuna BONGOWOOD! Sinema zinaanza kutengenezwa kwa wingi Tanzania, na watu wana hamu ya kujifunza namna ya kuzitengeneza. Si muda mrefu iliyopita, enzi Ujamaa utengenezaji sinema ilikuwa si kitu muhimu kwetu. Wakati huo kutenegeza sinema ilikuwa ghali na serikali ya Ujamaa ilikuwa na kazi muhimu kama kuwapatia wananchi maji safi, elimu na huduma ya afya.

Lakini ziku hizi asante 'digital technology' bei ya kutengeneza sinema imeshuka sana.

Kama makao makuu ya Hollywood iko Los Angeles, California USA, ninapendekeza studio kubwa iwe Bagamoyo. Bagamoyo ni penyewe kwa mambo ya usanii. Kuna Chuo cha wasanii huko Bagamoyo, na mambo mengi.

Baadhi ya Sinema za KiTanzania, zilizotengenezwa Tanzania ni:


1. Simu ya Kifo (2007)
2. Tusamehe (2005) http://www.kibirafilms.com/tusamehe
3. Bongoland (2003) http://www.kibirafilms.com/bongoland
4. Maangamizi the Ancient One (2001) http://www.grisgrisfilms.com/html/maangamizi_-the_ancient_one.html
5.Arusi ya Mariamu (1985) http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
6. Mama Tumaini (1987)
7. Mogambo (1953) http://www.imdb.com/title/tt0046085/
8. YombaYomba (1985)
9. Darwin’s Nightmare (2005) http://www.imdb.com/title/tt0424024/
10. Surrender (2000) http://www.newsreel.org/nav/title.asp?tc=CN0132&s
10. These Hands (1992)
11. Gubu la Wifi
12. Four Weeks in Tanzania (2004) http://www.studentfilms.com/film/get.do?id=978
13. These Hands (1992)13. Girlfriend (2004)
14. Fimbo ya Mnyonge (1974)
15. Tumaini -Childhood Robbed (2005) http://www.abantuvisions.com/StoryPage.php?StoryID=3

Thursday, May 24, 2007

Postcard from Bagamoyo


Nimeona hii POSTCARD ya Bagamoyo Beach, kwenye neti.

Kuna picha zingine hapa: http://www.rlw-photography.com/blog/category/contests/

Mshindi wa American Idol 6 ni Jordin


Natoa pongezi kwa Jordin Sparks aliyeshinda American Idol 6 jana. Ana miaka 17 tu na anasoma darasa la 11 (Form 3). Ni mshindi mwenye umri mdogo kuliko wote waliowahi kushinda.

Baba yake ni mcheza footbal (American style) mweusi, na mama ya ni mzungu. Huyo Jordin ni mrefu na ana mwili. Alifmfanya Ryan Seacrest aonekane kama pygmy kwake.

Kwa uimbaji, sijamfurahia sana. Ila aliimba vizuri kuliko aliyebaki, Blake, kijana wa kizungu aliyependa kutia ma beatbox kwenye nyimbo zake.

Wenye sauti nzuri Melinda na Lakisha walitolewa wiki kadhaa zilizopita. Wanasema watazamaji wa America Idol walipungua kwa vile show mwak huu haikuwa nzuri. Nsiyohaikuwa nzuri, maana walitoa waliojua kuimba mapema. Wengi walikuwa wanaume weusi. Tungojea January 2008, kuona American Idol y itakuaje.

Tuesday, May 22, 2007

Kama Huoni Blog

Wapendwa wasomaji blog sizifuti. Hapana zinaingia Archives, na kila mtu anaweza kuziona. Kama kuna blog uliyopenda na kwa sasa huoni, uangalie upande wa kushoto wa blog, halafu u-clik kwenye Archives. Kama unakumbuka mwezi ulioiona u-click kwenye mwezi na mwaka. Pia, unaweza kufanya Search hapo juu kwenye upande wa kushoto.