Saturday, October 27, 2007

Alifungwa miaka kumi gerezani - Kisa Ngono. Sasa ameachiwa huru.


Kijana Genarlow Wilson (21) ameachiwa huru baada ya kukaa gerezani mkoani Georgia kwa miaka miwili. Wilson alipewa kifungo cha miaka 10 ...kisa akiwa na miaka 17, msichana wa miaka 15 alikutwa anamnyonya ume wake!

Kwa kweli naona ni vizuri hao vijana wakifanya ngono wenyewe kwa wenyewe kulikoni huyo binti wa miaka 15 angekutwa na jibaba wa miaka 40! Lakini sheria za kule kusini mwa Marekani ni kali hasa mahakama wakiamua kuzitekeleza.

Kesi ya Wilson ilikuwa machoni mwa waMarekani toka itokeee. Na sasa Georgia wamebadilisha sheria. Kama vijana wamepishana umri hadi miaka minne hakuna kosa. Yaani tuseme moja awe na miaka 20 mwingine miaka 16.

Hapa Marekani lazima watu wawe waangalifu na sheria. Vijana wa miaka 18 wanaweza kufungwa wakikutwa wanafanya ngono na wasichana chini ya miaka 15 na states zingine hata miaka 16! Pia wanaitwa 'Sex Offender' daima.

Je, Afrika hizo sheria zingekuwepo ingekuwa balaa!

1 comment:

Anonymous said...

Msichana wana miaka 15 anajua nini. Alionewa huyo kijana!