Thursday, October 04, 2007

Britney Spears Anyang'anwa Watoto Wake na Serikali



Mwimbaji Britney Spears amenyang’anywa watoto wake na Serikali. Kisa wanaona kuwa hafai kulea watoto. Kwanza anashindwa muda gani na hao watoto, maana anakuwa amelewa. Mara alipigwa picha hajavaa chupi na dunia yote iliona hao watoto walitoka wapi. Nadhani alichoka na hao watoto maana jana ilikuwa awe mahakamani kujitetea na hakutokea. Badala yake paparazzi walimwona anatembea na gari yake barabarani.

WaTanzania walioko hapa USA wengi wanajua sheria za hapa. Hakuna kumchapa mtoto. Hapa Boston mtoto wa MBongo aliulizwa kama anapigwa na wazazi wake. Alijibu ndiyo. Mbona karibu serikali wamchukue huyo mtoto. Mwisho walikimbia mji.

Sasa huyo Britney na mapesa yake yote anaweza kulipa maaya wa kuwalea lakini bado walioona kuwa hafai kulea. Watu wa karibu naye walidai kuwa anatumia madawa ya kulevya mbele ya watoto, anatembea uchi mbele ya watoto na mengine. Pia walidai anawalisha ‘junk food’ kama soda na chips.

Sasa hivi watoto wanalelewa na baba yao, mcheza densi, Kevin Federline, ambaye ana watoto wengine wawili zaidi aliyezaa na mwanamke mweusi na mcheza sinema, Shar Jackson.

Watu wanadai kuwa huenda Kevin, alimshitaki Britney kwa sababu mwisho wa mwezi huu ndo mwisho wake kupokea posho ya dola $20,000 kutoka kwa Britney. Wanasheria wanasema kuwa Kevin ataweza kuendelea kupokea hizo $20,000 na zingine kila mwezi kama akiweza kutunza watoto vizuri.

Maisha ya Britney ni ya ajabu. Miaka Mingi alidai ni bikira na alikuwa mfano wa kuigwa. Mara kasema alishavunjwa huo ubikira siku nyingi. Mara Aliolewa kwa muda wa siku tatu tu na kijana aliyesoma naye shule ya msingi. Baada ya hiyo ndo kunvunjwa ndo tulisikia kuwa amemwibia Shar Jackson, baba watoto wake. Britney ana vituko.

1 comment:

Anonymous said...

kuporomoka kwa huyu binti kunasikitisha sana. Sasa wale vijana waliokuwa wanamuona kama "idol" wao sijui inakuwaje. Magazeti ya "tabloid" yatanufaika sana na hii habari kwa muda mrefu ujao.