Wednesday, October 24, 2007

Nyumba za Matajiri zaungua moto California!


Jamani mnakumbuka Hurricane Katrina. Ile kimbunga iliyoleta balaa mji wa New Orleans na kusambaza watu wake. Wengi waliathirika kule New Orleans walikuwa ni weusi maskini.

Sasa moto mkali unateketeza maeneo ya matajiri huko California. Misaada ya kila aina wamepatiwa mara moja. Hata kwenye shelters zao wanafanyiwa catering na Legal Seafoods na Au Bon Pain, na kulalia magodoro na siyo cots!

Watu wawili wamekufa, zaidi ya 50 wako mahututi hiospitalini na zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia! Nyumba kadhaa za ma celebrity zimeungua na pia Hollywood wamesimamisha kupiga filamu na show za TV kwa vile wafanyakazi wengi wameathirika au sehemu walizotaka kupigia zimeathirika.

Ajabu kwa sasa sehemu ziliathirika zaidi kule California ni maeneo ya wapiga kura Republicans!

Kwa habari zaidi someni:

No comments: