Tuesday, October 09, 2007

Walioigiza katika sinema ya Bongoland II






Kuona Actors wote waliocheza katika sinema yaBongoland II nenda:

http://www.kibirafilms.com/bongoland/cast.html

7 comments:

Anonymous said...

tunawatakia kila heri , hi sinema iwe kwenye wale watakaopata tuzo ya academy, kama siou tuzo angalau iwe kwenye orodha.
Je mna pesa ya kuitangaza hii sinema?? movie nyingine huwa sio nzuri lakii kutokana na promotion basi zinaaangaliwa na watu wengi zaidi au hata kupata "nomination"

Ila tunasubiri kwa hamu kununua hii movie, je itatoka lini??

Anonymous said...

Wa kati hapo juu anaonekana kama dada Joyce. Au nakosea? Kama ndiye nampa pongezi! Da Chemi tupe majina basi. Tupo ughaibuni miaka mingi ndugu zetu tumepotezana nao.

Chemi Che-Mponda said...

mlalahoi, asante sana kwa maoni yako. Ni kweli kutangaza sinema inachukua hela nyingi na kama unavyosema sinema enye pesa nyingi za kuitangaza inaweza kupata umaarufu hata kama ni sinema mbovu.

Mimi nimekwishapitia Academy Award experience na sinema ya Maangamizi the Ancient One. Iliteuliwa na Tanzania katika Foreign Language category mwaka 2001. Kwa kweli ingekuwa na budget kubwa ya kuitangaza huenda ingeingia katika Top Five. Halafu tatizo lingine ni kuwa washenzi wa Academy waliipanga siku na saa mbaya kuionyesha kwa wapiga kura. Hiyo ni muhimu maana ukipangiwa siku na saa nzuri una pata wapiga kura wengi. Na kuna mengine naona itabidi niandika kabisa blog kuhusu hiyo swala.

Pia njia nyingine ya kuitangaza ni kuionyesha kwenye Film Festivals.

Anonymous wa 6:19am, Hizo picha tatu ni Thecla Mjatta, Sabrina Rupia na Mimi.

Anonymous said...

pia kwa kuongezea tuu kwa kile chemi alichosema au kaka mlala hoi kweli promotion ni ghali sana
na hasa inapokuja ktk ukweli ulio wazi kwamba kwanza festivals nyingi siku hizi wanataka film yaani 35mm reel ili iweze kuwa projected kwa screening ingawa kuna baadhi chache sana tena saana wanachukua video kama hiyo sinema ni nzuri kweli kweli kwa sababu zingine wana zo high end digital projection facilities

sasa kwa sinema ya kaka kibira nihisi tu kwamba ni vigumu kupata slot ya festivals kubwa kubwa kama nilivyosema wanataka film 35 mm
ingawa kiufundi inawezekana kutransfer video kuwa film 35mm,16mm au hata super16mm lakini maandalizi yake kiufundi huanza mapema ktk hatua za upigaji picha yaani dop kiufundi anapaswa azingatie na a-seti viwango vya picha na lens na mwanga nk kwa ajili ya mahitaji transfer .sasa sijui kama kibira production walikuwa na hilo kichwani kabla ya kuanza production.
Lakini kama ukipata festivals wanzochukua video napao wana coplikesheni zake kwa sababu wengi wao watkuambia wantaka video yes lakini ni high end professional high def mfano ile sinema ya star wars ya george lucas aliyocheza leeam nielson ilkuwa shot kwa video ikfanyiwa transfer kuenda film mtu wa kawaida si rahisi kuliona hilo kiufundi ilwasave pesa nyingi sana

pia gharama nyingine ni publicity na fee za kuingia festivals mfano toronto film festivals wanadai hela nyingi ktk fee ya kuingia festival

lakini tusikate tamaa tuendelee tuu ipo siku mambo yatakuwa.
wenzetu south africa walianza cheza na film miaka mingi na hata hivyo huko napo si wengi wanauwezo wa film wengi wanashoot video kisha wanatransfer pale capetown au joburg

mimi nasema hilo si tatizo saana ni suala la muda tuu kama tutaendelea kusapoti watengenezaji sinema wenye muelekeo sio mambo ya "the fake pasters" au dilema au sijui "girl friend" kwa muenendo huo wa kinaijeria hatutaweza fika kwenye hizo academy
kibira kaka usihofu tuko nyuma yako ninakuadimaya kwa kuwa umethubutu na umeseti mfano wa kiprofessional hapa nyumbani natamani serikali yetu pia ingekuwa na kitu kama GRANTS kwa ajili ya kuziwezesha sinema za kiprofessional zenye theme halisi ya nyumbani ili walau ziingie ktk festivals tuu hata tusipoata award
chemi kwani una info zozote kama kuna grants pale MFUKO tanzania ?
vitu kama hivyo vingeweza kusaidia ktk tranfer gharama za transfer na kutoa copy za reels chache tuu ajili ya festivals za maana
asante
Raceznobar

Chemi Che-Mponda said...

Raceznbar,

Asante kwa maoni yako. Sinema ya Bongoland II imepigwa kwa Hi-Def. Na ni kweli festivals nyingi wanataka hiyo 35mm reel. Nimeabiwa kuwa South Africa wana transfer kwa bei nafuu kuliko hapa USA kama kwa $5,000.

Nadhani na Bwana Kibira atatoa jibu lake.

Anonymous said...

Kibira hapa,

Kwanza kabisa namshukuru dada Chemi kwa jitihada zako za kurusha habari hizi mtandaoni kwa ujumla.

Pili nashukuru sana kwa comment nyingi na nzuri kwa sababu zinatia moyo na kunifanya kuwa na nia ya kuendelea kupigana kuleta picha zenye maana kwa watu wa Afrika ya Mashariki lakini hasa nyumbani.

Garama ni kitu kikubwa sana na kukosa mtaji, production huwa hafifu. Kama alivyosema Chemi, picha hii ilipigwa katika HD na hii ni rahisi kufanya transfer kuweka katika 35mm. Hata hivyo ikibaki ilivyo, quality yake ni ya juu kulinganisha na digital video. DVD zitakazotoka zitakuwa na clarity ambayo ni ya aina pekee kulinganisha na sinema nyingi hata za kimarekani.

Lakini lengo letu ni kuonyesha kuwa sisi nasi tuna uwezo wa kutoa sinema za hali ya juu. Watu wote walio katika sinema hii wamenidhirishia kuwa uwezo tunao. Labda Chemi anaweza kuwa shahidi wangu. Msaada ukipatikana ni vizuri, lakini tunajitahidi hata ukikosa, kubuni njia za kuendeleza production zetu. Lakini support ipo kwa kiasi Fulani na tegemeo letu ni kwamba baada ya matunda ya sinema kama hii, labda na ufadhili utaongezeka.

Quality ya sinema hii itasema mengi kuhusu uwezo wa wabongo katika fani hii na itasaidia kututofautisha na sinema za Afrika Magharibi.

Promotion tutafanya, hasa uzinduzi huko Bongo na pengine. Mungu akitujalia labda November au December mwaka huu…labda!

Tunashukuru support yenu! Tunaomba muendelee kutupigia debe na sisi kwa kweli hatutawaangusha.

Ahsante!

Josiah

Anonymous said...

Hello Josiah,Chemi na wadau wengi
nashukuru sana kwa maelezo yenu ya haya mambo ya movie production, promotion etc. kwa mimi ambaye sijui kitu juu ya haya maswala, inanisaidia kuelewa nini kinaendelea "behind the scenes".

Kuhusu kuitangaza hii sinema, hasa kuweza kuiingiza kwenye orodha ya academy-je wanasiasa wetu wanaweza kuchangia?? Maana kama mtu huna pesa unatakiwa kutumia kujuana au "influence". Hawa wanasiasa mfano Raisi Kikwete, balozi Ombeni n.k, sasa hivi wanapenda kuitangaza nchi hasa katika maswala ya utalii, nafikiri sinema inaweza kutumika katika kusaidia kutangaza nchi. Kwa hiyo, pande zote mbili yaani nchi na ma-producer wa hii sinema- wanaweza kufaidika.

Nakumbuka Waganda wametumia sana sinema ya "the last king of scotland" kwa ajili ya kuongeza utalii-hasa baada ya yule muigizaji mkuu wa hiyo sinema kushinda oscar.

Haya ni mawazo tu , je wengine mnasemaje??