Monday, November 12, 2007

Mama yake mzazi Kanye West Amefariki


Kanye West na mama yake, Dr. Donda West

Kuna habari ya kusikitisha na ya kushangaza....mama yake mzazi, mwimba rap, Kanye West, amefariki dunia ghafla siku ya jumamosi.

Mama yake, Dr. Donda West, alikuwa na miaka 58. Habari za kuaminikia zinasema alikufa baada ya kufanyiwa opresheni ya urembo, lakini hawakusema ilikuwa ni opresheni ya aina gani.

Huenda ilikuwa ya kupunguza matiti, matako, uso, liposuction (kupunguza mafuta).

Mama yake alikuwa meneja wake. Alistaafu kazi ya kufundisha kiingereza Chuo Kikuu cha Chicago kusudi awe na mwanae.
Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni:4 comments:

Anonymous said...

DOH! Pole sana Kanye.

Nauliza. Mtoto anaita Kanye, mama anaitwa Donda. Hao majina walipata wapi.

Anonymous said...

Shule ya sekondari tulikuwa wavulana watupu, sasa vituko vilikuwa vinatokea wakati wanapokuja wasichana kucheza muziki, hii ilikuwa inatokea mara 1 katika miezi 3, siku nyingine huoni binadamu wa kike zaidi ya walimu (mimama) na sekretari wa headmaster. Disco likianza kila mvulana anachangamkia nafasi anayopata ya kuongea na msichana huko ukumbini, vinginevyo disko likiisha mabinti wanaunga foleni hadi kwenye basi ambalo linawasubiri nje kwenye mlango wa ukumbi. Kama msichana hakutaki ukimuuliza unaitwa nani, anakujibu "Sikuta". Basi mvulana anazidi kujigonga "Jina lako zuri! Sasa nikikuandikia barua, niandike Sikuta nani?" Anajibiwa "Kiwewe". "Basi nitakuandikia" mvulana anasema. Wakati muziki unaisha msichana anamkumbusha jina, "Sikuta Kiwewe, usisahau, bye".

Anonymous said...

Maskini! Sasa alitaka hiyo plastic surgery ya nini na yeye ni mzee wa miaka 58.

REST IN PEACE MAMA KANYE.

Anonymous said...

Donda West's Doctor Comes Forward, Kanye Releases Statement, Doctor Has DUI Convictions
Huffington Post
November 13, 2007 08:08 AM


Two days after Donda West's untimely death following cosmetic surgery, the doctor who performed the procedures stepped forward late Monday night to proclaim his innocence to website TMZ. Dr. Jan Adams, who claims to have performed a tummy tuck and breast reduction on singer Kanye West's 58-year-old mom said he did not cause her death. Rather, Dr. Adams hypothesized Donda may have died from a heart attack, pulmonary embolism, or massive vomiting.
Monday a coroner's official said Donda may have died from surgical complications and an autopsy is set to begin.
Donda was reportedly at home Saturday evening when she stopped breathing and someone phoned 911. She was pronounced dead about hour later at the Centinela Freeman Hospital in Marina del Rey.
Hours before Dr. Adams came forward, Kanye West released a statement. It thanked fans for their outpouring of support and asked for donations in Donda's name to Kanye's charity, which she cofounded and which focuses on reducing the high school dropout rate.

Update:
TMZ reports that the medical board wanted to suspend Dr. Adams' license this past April following multiple DUI convictions.