Tuesday, January 08, 2008

Alicia Keys atakuwa Lena Horne!


Habari kutoka Hollywood zinasema kuwa Oprah, amemchagua mwimbaji maarufu, Alicia Keys, kuigiza kama mcheza sinema na mwimbaji maarufu wa Marekani, Lena Horne. Sinema hiyo itaitwa The Lena Horne Story.

Watu wamengojea miaka mingi hii sinema. Production bado haijaanza.

Lena Horne alikuwa maarufu miaka ya 1940' na 1950's. Alikuwa pia ni moja wa masex symbol wa wakati huo. Ana miaka 90 sasa.

Kwa wasiojua, Lena Horne, alikuwa mmarekani mweusi wa kwanza kupata studio contract Hollywood, 1940. Alicheza katika sinema kadhaa kama Cabin in the Sky (1943), Stormy Weather na Panama Hattie. Alikuwa mwimbaji maarufu mpaka miaka ya 80 alivyostaafu. Weusi wametoka mbali katika Hollywood na ubaguzi bado upo. Enzi hizo kama ni mweusi unaingia mlango wa nyuma, hakuna ushirikiano na wazungu, mnatumia choo duni, unakula chakula nje, hakuna kulala hotelini na mengine mabaya.

Bi Horne alimtaka Janet Jackson, amwigize. Baada ya ile kasheshe ya Superbowl mwaka 2004, (Janet Jackson kuonyesha umati chuchu), Horne alisema hana habari na Janet Jackson tena wala hataki kusikia habari zake.

Oprah ameanza kutengeneza sinema za weusi tena. Alikuwa amepumzika kwa sababu ile sinema ya Beloved , ilikuwa bomu. Watu wengi wanasema Beloved isingekuwa bomu, kama mtu mwingine angeigiza kama mhusika mkuu, Sethe. Oprah aliigiza kama Sethe na alikuwa na Scenes za mapenzi pamoja na scene ambayo ananyanyua gauni na kukojoa. Pia watu wanasema kama wangesema ni sinema ya matishio (horror) ingefika mbali zaidi. Sinema nyingine ambayo Oprah ame produce hivi karibuni ni The Great Debaters starring Denzel Washington.

3 comments:

Anonymous said...

I saw beloved recently kwa kweli haikuwa nzuri. Janet angefaa kuigiza kama lena ila hana sauti nzito kama alicia. She was beutiful pua imechongoka bila nose job siku hizi watu wengi wa hollywood ni feki. Talking of holywood Dachemi mbona huja tupa habari yoyote ya movie star wetu kanumba au hukufahamu au uko busy sana?

Chemi Che-Mponda said...

Hi Anonymous wa 3:21PM,

Asante kwa maoni. Nina habari za Kanumba na utaziona hivi karibuni.

Anonymous said...

tutashukuru kweli ukituwekea habari za kanumba da chemi..god bless