Saturday, January 19, 2008

WaTanzania Wengi Hatujikubali! - Maoni ya Mdau


Kuna Dada fulani (jina ameomba nihifadhi) amenilietea maoni yake. Nazishea na wadau....

***********************************************************************

Dada Chemi ngoja leo nikudondoshee mtazamo wangu,mi nimpezi sana wa blog hii,na sababu kubwa iliyonifanya nipapende humu ni uandishi wako,na mimi nipe fulsa nikuandikie leo mtazamo wangu maana na mimi napenda saana kuandika.

Kitu ninachotaka kuwaeleza watanzania wenzangu,majirani au marafiki zetu hii leo ni kwamba tujijengee utamaduni wa kukubali kama tunaweza kufika kimaendeleo kama wenzetu waliotutangulia.

Mfano wangu nautoa humu humu kwenye pita yangu blogini mwako nikakuta picha mbalimbali za muigizaji maarufu wa Tanzania Steven Kanumba ,ambaye kajipatia umaarufu mkubwa katika sekta ya uigizaji hapa nchini akiwa ziarani Hollywood na uliandika Kanumba au kwa watu wanaomkubali humwita Denzel Washington wa bongo.

Sasa Dada Chemi ulileta mzozo pale ulivyosema Denzel Washington wa bongo,nilivyoona mimi nilifurahi na kusema “yes” siku moja Kanumba anaweza kufika hapo Denzel alipo lakini wasiwasi wangu ulikuwa kwenye maoni,nikasema sasa asubiri kushushuliwa na wabongo (maana ni kawaida yetu kutokukubali).

Nilifurahi sana kuona watu mbali mbali wakimpongeza na kukubali kazi yake,lakini kilichonisikitisha kuna wengi wadau hawakumkubali yeye afananishwe na denzel hata siku moja.Kwa kweli nilishwangazwa sana na kauli hizo.

Na huo ni mfano mmoja tu,kuna vitu vingi tu vinafanyika miongoni mwetu na uwa tunakatishana tamaa sana,wewe tu thubutu kumwambia mtu mipangilio yako ya baabae utaona ishu yake itakavyokuwa,”oh wewe utaweza kweli au walishafanya wakina fulani wakashindwa sembuse wewe” .

Sasa mi nilikuwa najiuliza wenzetu (Nchi nyingine) wakipiga hatua fulani ya juu,uwa wanawathamini na kuwaunga mkono kwa hatua waliyopiga,kwa nini na sisi tusibadilishe mioyo yetu na tujipende,kama mtu kafanya vibaya basi mshauri kama mtu kajitahidi kwenye maendeleo basi mpongeze,na kama ni mazuri yaige na wewe uwe na maendeleo kama hayo yake.

Kujikubali ni kukubali kwamba unaweza kufanya kitu chochote cha maendeleo ulichopanga na ukafanikiwa na hata zaidi yake,na hayo ndo maendeleo yenyewe,kama huo mfano wangu hapo juu wa Kanumba kuitwa Denzel Washington wa Bongo, sasa kwani Kanumba hawezi kuwa kama Denzel au zaidi?.

Nakumbuka mimi nilikuwa nataka kuanza biashara fulani hivi,nikamwaga aidia yangu kwa jamaa zangu fulani,unajua waliniambia nini,eti hiyo biashara ni ngumu sana na sitaweza kufika popote na nitapoteza muda na nguvu.

Kwa kweli niliumia na kuvunjika moyo kabisa,na mimi naye nikawaamini kwa kweli hata kasi ya kufanya hiyo biashara nikaacha kabisa,basi angalia yaliyofuata,baada ya mienzi kadhaa nikashangaa kuona hao hao walioniambia haiwezekani wakianzisha ishu iyo iyo niliyowapa kuomba ushauri kwao na hao hao ndo waliniambia haifai.

Kitu ninachotaka kusema hapa ,tujiamini kwa kila kitu tunachotaka kufanya,hakuna mtu anaweza kuondosha ndoto yako kwenye Dunia hii ila wewe mwenyewe, Kama mtu hakuamini basi wewe jiamini na unaweza.

Hivi unajua maendeleo mengine yanakuja pale wewe ukimuona mwenzio kafanya vizuri na wewe unataka kufanya kama yeye,lakini inaelekea wabongo wengi hatujui hilo na wanaoona ni wachache labda.

Zaidi ya yote tunatakiwa kukaza buti kisawasawa tusiruhu kukatishwa tamaa na wengine,tuamini kama kila mtu anauwezo na nafasi ya kufanya jambo la maendeleo bila kukatishwa tamaa,Lakini wabongo tubadilike tusiwasifie wenzetu tu na sisi tujikandamize kuwa ni dhaifu sana,au haujui mtu akisifia ndo bichwa linapanda na kufanya zaidi ili asikuangushe uliyemsifia(ha ha ni mawazo yangu tu).

Je unajua ni kwanini duniani wazungu wanajiona ni bora zaidi ya wengine?na wamejitangaza kwa kujisifia na kujikubali kwamba wao ni zaidi,na ngozi yao ni bora kuliko zingine?.Na hapo ndo maana kimaendeleo acha tu ya kiuchumi tunaiga kutoka kwao,na hata baadhi ya dada zetu wameamini hilo na kujibadilisha nao wawe weupee kama wazungu.

Mi siku nilijiuliza eti kama sisi weusi,tungekuwa wazungu na wazungu wangekuwa kama sisi,nywele rangi nk,Nafikiri tungelazimika kujibadili kama sasa tunavyotaka nywele ndefu laini nk.Hapo mi nafikiri wamefanya tuwaamini hivyo kwa sababu wanadhamini vito vyao zaidi na kuwaeleza wengine umuhimu wake hata kama si vizuri na vyakuigwa.

16 comments:

Anonymous said...

nawee umepoteza muda mwingi kuandika kumfagilia kanumba,kanumba awezi ata kupata kazi za ndani kwa denzel achilia mbali kumfikia kuna gap kubwa sana.

Anonymous said...

Hawezi kuwa Denzel kwa kutudanganya kama watoto! Ati tuzo! Tuzo gani zisizotangazwa toka mapema!?

Anonymous said...

Ndio maana hatuendelei, kama huamini utawaze basihutaweza ni bora u aim higher ukapata high kuliko jkujikatia tamaa kabisa. ni bora kujaribu kuliko kushia kusema laiti unge...Kanumba kajitahidi kama mapungufu anayo ajinoe ajifunze english, asome vitabu kama vya kina sydney poiter ajifunze mwenzie alivyo struggle mapka akafikia hapo alipo. Nayie wakatisha tamaa hata kujiigiza wenyewe hamuwezi mwacheni asongembele kijana wetu. Tunatakiwa tubadilike tuwe kama wahindi na waarabu. Huwezi kuwaona wakifa njaa kwa sababu wanasaidiana sana na kuinuana. Da chemi unatakiwa umpe darasa kijana huyo kwa vile wewe ni muigizaji uliyepiga hatua kuliko yeye kiasi cha kuwa extra kwenyefilamu kubwa. Kuna somethings kachemsha ndio kama kujipiga picha akipokea tuzo ya dukani lakini sisi ndio tutakao mjenga ama kumbomoa

Anonymous said...

Kujikubali pasipo kujikosoa ni kujidanganya.Umesifia tuu lakini hajagusia "Awards" za Kanumba.Suala sio kucheza filamu nyingi bali pia ubora wa filamu hizo.Lakini kikubwa zaidi ni tabia ya msanii husika.Think of Denzel alipokuwa star-in-the making,unadhani alikuwa anafanya upuuzi wa kununua suveniours za $5 na kudai amepewa Award Hollywood?Endeleeni kulewesha sifa kijana wa watu,lakini as usual,tunajua mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza,sio kumhurumia,bali kumcheka.

Anonymous said...

I won't even bother explaining why Kanumba will have to personally contact Jesus Christ to achieve the amount of success Denzel has,but what I will do is post a picture that sums up the reality of the situation:

http://img408.imageshack.us/img408/3302/denzelvskanumbapk9.jpg

Chemi Che-Mponda said...

Naweza kusema hivi...kufikia standard ya Denzel yaani A list ni kazi ngumu hapa Marekani. Inabidi uwe unafanya training kila mara, kama hufanyi acting basi inabidi ufanye michezo ya kuigiza. Hao A- list actors wengi ni wataalamu wa Shakespeare hata Will Smith na mke Jada. Unaona walipofika? Kujifunza hakuna mwisho hata katika uigizaji. Wazungu wanasema 'practice makes perfect'.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa Steven Kanumba ni hivi endelea kuigiza katika hizo sinema za waNigeria na waBongo. Hata siku moja usiseme kuwa nimefika, endelea kuwa na moyo wa kujifunza. Usione haya kuuliza maswali kwa wataalamu, tena Tanzania wako akina Prof. Lihamba na Prof. Mlama. Tengeneza resume ya acting, uwe na headshot safi. Uwe na copy kadhaa wakati wote maana huwezi kujua utakutana na mteneneza filamu lini.

Tuzo zitakuja, kazi nzuri zitakupatia tuzo.

Wikedzi said...

Binti, umenikuna sana ulipowataja Prof. Mlama na Prof Lihamba, ingawa inabidi ujue kuwa film industry ya Tanzania inawachukia sana wataalamu wasomi. Producers wanaona wanaharibiwa bajeti, actors wanaona watakosolewa, hivyo fani inabaki ikiongozwa na vipofu kuwaongoza vipofu wenzao.

Anonymous said...

Nyongeza ni kwamba watu wote duniani hukutana na vipingamizi kuhusu hali walizonazo au vitu wanavyofanya. Ukiwa na viwango vya juu sana vya kazi unazofanya usidhani kila mtu atakukubali, wapo wengi tu watakaokupinga na "kuponda". Na hata ukiwa duni sana katika kazi unayofanya, usidhani kila mtu atakupuuza, wako wengi pia watakaokusifu, sanasana kutokana na ujinga wao wa kutokujua ni kipi kinachostahili sifa wanazotoa. Cha maana ni kuwa na malengo na kuwa na viwango sahihi vya kujilinganisha nayo, ili hata unaposifiwa wakati unajua kiwango chako ni duni "usivimbishe" kichwa, badala yake uongeze bidii kufikia malengo yale. Kadhalika ukipata wanaokupuuza ilhali una uhakika hatua uliyofikia ni nzuri katika malengo yako, bado usikatishwe tamaa na maoni hayo, badala yake uyachukulie kama changamoto katika safari yako.

Na mwisho namtakia kila la heri huyu mwanangu Steve Kanumba(huo mwaka aliozaliwa nilikuwa na umri wa miaka 20, kidato cha sita).

Brian Kithuku

Anonymous said...

Nampongeza Kanumba kwa kazi nzuri na kujituma. Mimi ninafikiri kama ifuatavyo;
1. Nafikiri mtu anayemuongoza katika kutoa matangazo binafsi inabidi abadili muulekeo kwa sababu picha zilizotolewa na chemi haziendani na maelezo kwani zinatoa maswali mengi kuliko majibu. Nina maana anaonekana kama mtalii wa kawaida. kwa mfano angetoa picha ambazo zinaonyesha amekutana na waongozaji (producer).

2. Hiyo award aliyopata hajafananuliwa ilikuwa ni award ya nini na ilitolewa kwa sababu zipi?

3. Ni mapema sana kusema lolote wakati huu kwani sidhani kama kuna mkataba au makubalino yoyote amepata, (labda hajatuambia).

Ninafikiri inabidi kubadilisha mkakati wa kumtangaza ndugu yetu (Kanumba), hizo picha zilizoonyeshwa lazima atapata negative feedback.

Pia ningewaomba Watanzania wenzangu nafikiri umefika wakati wa kukubali kazi nzuri za waigizaji wetu. nafikiri maoni yenye changamoto yatasaidia zaidi kutoa muongozo na muelekeo kwa Kanumba ili nasi tuwe kwenye ramani ya dunia ya uingizija.

Napenda kuwakilisha

Anonymous said...

chemi you should be whisked in a court of law for crimes against the people of tanzania,for knowingly,that its not true,yet using inept jounalism,you feed us this kanumba crap

Anonymous said...

Kumfananisha Kanumba na Denzel ni kumvunjia hadhi kubwa sana Denzel Washington, yaani Kanumba hamfikii hata kwa 1%. Ila kama anataka kuwa Denzel wa Tz basi namshauri aongeze jitihada, aache majungu na ubi-shoo basi anaweza akafanikwa japo 5%

Anonymous said...

Huyu Anony wa January 19, 2008 7:07 AM ni sehemu tu ya wale wengi ambao wamezungumzwa kwenye makala hii.

Mi namuunga mkono mwandika makala hii "WATWANZANIA HATUJIKUBALI" Lakini mi nadhani sasa watanzania wenyewe tuichukue hali hii kama changamoto na tuangalie tunaweza kutoa mchango gani katika kuhakikisha tunaondokana na Kasumba hii mbaya kuliko kuendelea kuandika makala za kulaumu au kulalamika kuhusu changamoto hii.
Mi nadhani umefika muda sasa wakuanza kufanya Talk the Talk.

Nami nitaanza kwa kutoa changamoto kwa wadau wote wa kijiji hiki na wengine popote.

Lakini nianze kwa kutoa mfano. Hivi karibuni shirika la utnagazaji la Taifa (TBC) kupitia Televisheni yetu ya Taifa wamekua wakionyesha mfululizo wa vipindi vya Kijapani vikienda kwa jina la "The Project X". Katika vipindi hivi wamekua wakionyesha mashujaa wa kizalendo wa Kijapani waliotoa michango katika nyanja mbalimbali katika maendeleo ya Taifa lao.

Kwa kweli kipindi hiki kimejaribu kumgusa kila mjapani Shujaa, Kuanzia aliyejenga mnara wa Kwanza mrefu kupita yote wamawasiliano mpaka kwa wajapani waliojitoa mhanga kwenye kuhahakisha wanastumia elimu na ujuzi wao wa Afya ya wazazi na uzazi hatari ili kuokoa maisha ya maelfu ya ndugu zao.

Mi nadhani hapa tunaweza kuanzia, kuna watanzania wengi walioifanyia Nchi yao makubwa ambao hawajulikani licha wale waliotoa michango midogo lakini iliyoikuna Dunia.
Hapa nitatoa mfano wa wachache ninao wafahamu na si vibaya wengine wakatukumbusha.

Mzee Abdulwahid Sykes aliyekua mpambanaji na miongoni wa waanzilishi na mfadhili mkubwa wa Vuguvugu la Uhuru wa nchi hii,

Mzee Moris Nyunyusa Mpiga Ngoma hodari mlemavu wa macho aliyeipata heshima kubwa nchi hii katika fani yake.

Mzee Lipangile
Alievumbua matumizi ya Mianzi miti kama technolojia mbadala na rahisi katika usambazaji wa maji vijijini.

Shaaban Robert
Mwanamashairi na muasisi mkubwa wa lugha yetu adhimu ya kiswahili.

Abdala "king" kibane (Mputa) mwanasoka Nguli aliyetetea taifa lake na hadi sasa anaendeleza shule ya Vipaji vya watoto wadogo.

Juma Ikangaa, Leodger Tenga,Amina Mongi,Mzee Nyirenda na wengi wengi wengineo.

Hivi Dada Chemi hatuwezi tukawa na siku moja katika kijiji hiki mabacho tutakua tunatoa makala ya Mtu aliyeiletea heshima nchi yake/ shujaa katika nchi hii. Labda watu watajitambua na Kujiheshimu

Anonymous said...

Mosi, Suala la kumfikia/kutomfikia Denzel W'ton (DW) sio issue sana! Issue ni kwamba kwa resources za Tz, age ya film industry Tz, ukubwa wa market ya film Tz na actors wenzake, anajitahidi!
Pili, sina hakika wanaosema moja kwa moja hamfikii DW, kama walishaangalia hizo filamu alzocheza Kanumba as many kama walivyoangalia za DW. Nina hakika wangekuwa wameangalia kungekuwa na kitu +ve cha ku-mention.
Tatu, DW sio "unit" i.e kwamba wengine ni "fraction" ya DW!
Nne, ku-appreciate ni "culture"! Mtu anaweza rewind life yake na kukuta hajawahi ku-appreciate ila kushabikia! Anaweza kutokuwa mtu wa ku-appreciate kwasababu ndivyo alivyokuwa/alivyolelewa. Mwana karudi home na 90% kapasi, ndo kwaanza mzazi anasema "mimi nilikuwa nabanjua hizo kibao'. Hakika huyo kuwa na culture ya ku-appreciate ni vigumu sana!

Anonymous said...

Eheeeee hapo sasa! Hadithi kasema ukweli. Wasanii Tanzania hawako tayari kujifunza kutoka kwa wataalam. Eti wasomi! Mama Lihamba ana ujuzi sana katika filamu msimwone hivyo. Kuna ubaya gani kuwaomba ushauri. Mnasem Oh Nigerians ndo wataalam. Akina Kanumba mnapotoshwa!

Na wewe Kanumba umeniangusha. Kichwa kimevimba mno mwisho kitapasuka!

Anonymous said...

mimi sikubaliani na huyo aliyeandika hii issue ya kwamba watanzania hatujikubali, atleast partially.sikubalaine naye na simwungi mkono si kwa kila kitu alichosema no! bali ktk suala hili la kanumba na hata katk issue hii ya kanumba sio kila kitu nakubaliana naye kimsingi wa kwamba kanumba ni msanii anayejitahidi sana hapa nyumbani no doubt! lakni ktk issue hii ya kanumba sikubaliani naye kwa sababu ni dhahiri kwamba kanumba ameudanganya umma mimi nikiwa mmoja wapo,unless mniambie kwamba si kanumba aliyetuletea habari zake binafsi za kupata tuzo huko hoollywood.
sasa huyo mtoa mada anyesema sisi watanzania hatujikubali mimi nataka niseme hivi,sitaki kujikaubali kwa staili hii ya kanumba yaani ya kujidanganya,kwanza ,pili ya kudanganya umma kwa sababu au misingi isiyoeleweka yaani anailewa yeye mwenyewe tuu.hebu nieleze ni kwa nini nijikubali ktk misisngi ya kujidanganya na kudanganya umma?
kwa mtu wa kawaida yaani mpenzi tuu wa kuangalia sinema ambaye hana ufahamu wa sanaa hiyo na ulimwengu wake ni rahisi sana kufikiri kwamba tunamwonea wivu na kwamba hatutaki maendeleo ya wenzetu. kama unafahamu nyenendo za kisanaa na biashara hii ya sineam pamoja updates za shughuli hizo from the front na behind the scenes za fani na ulimwengu wa kisinema ,ni rahisi mno kugundua na kumpuuzia kanumba kwa sababu amedanganya !
kimantiki ,kiurahisi ni kwamba kufika au kukanyaga hollywood siyo mafanikio ya kiusanii.kukanyaga eneo la mastudio au hollywood kwenyewe siyo kwamba sasa umekuwa superstaa au ndio kusema kwamba basi kipaji chako cha sanaa ya sinema kimekuwa .,kimsingi mtu yeyote yule anaweza kufika pale akafanya anchofanya na kupiga picha na mastaa au ktk mastudio nk
tuzo alizosema (kama ni kweli) ni non existent.
kwa kuongeza kimsingi na kuzingatia kanuni za kiungwana na za asili ni vema wakati woote ule mtu akajikubali na kujiamini ktk misingi ya ukweli kulingana na kiwango chake halisi cha ustadi wa fani husika,mathalan,sinema .

kwa maono yangu,nafikiri kwamba Tanzania ndio nchi pekee au miongoni mwa nchi chache sana hapa duniani ambapo mtu hujiita dokta ,profesa, nk na japo mtu huyo hana ustadi wowote uliopimwa kitaalam na kutambuliwa na taasisi husika ili mhusika huyo aitwa dokta
pia hata majina ya watu tuu mashuhuri mathalani denzel,bruce lee nk Tim Sebastian wa bbc ,Amanpour wa cnn nk tumekuwa na utamaduni huu na sasa sijui ni Tanzania tuu peke yake au vipi sifahamu lakini utamaduni huo umeota mizizi kwetu
hapa swali la msingi ninalojiuliza kwani haiwezekani mtanzania yoyote yule ktk fani inayohusika akafikia kilele cha ustadi ktk fani yake yaani kufikia kiwango cha kuwa taasisi ktk fani bila kujilinganisha au kujiita jina la mtu mwingine mashuhuri
binafsi tabia hii inanionyesha ni jinsi gani tulivyo inferior tumejijengea utamaduni wa kuwa chini tuu.lakini ukweli usiopingika ni kwamba tunaweza kufikia viwango vya ustadi wa juu sana ktk fani mabalimbali kuliko na zaidi ya denzel au bruce lee nk
mfano ,hebu angalia soka la bongo au hata mambo ya walimbwende tanzania .tunaacha kusema ukweli yaani sisi washabiki kwamba kiwango hiki ni cha chini tuongeze biddii na badala yake tujajribu kuwasifu na kuleta uzalendo usio na misisngi endelevu kwa wasanii ,wachezaji,walimbwende nk matokeo yake sote tumeyaona wakati wote ni suala la aibu tupu
wengi watu tunazani kwamba kumsifu mhusika na japo kiwango chake kiuhalisi ni cha chini ni kumpa moyo muhusika matokeo yake wahusika wa fani mabalimbali hutoka kuwakilisha nchi wakiwa na vichwa vimevimba wakifikiri ni makini na hodari ktk fani husika ni hapo sasa wanapokutana na changamoto za kiufundi na umahiri wa hali ya juu kutoka kwa wapinzani .matokeo yake hushindwa na kuanza kutoa lawama zisizo na msingi na hata wakti fulani kuleta mtafaruku miongoni mwa washika dau wa fani husika
kwa hiyo mimi maoni yangu ni kwamba ni vema kujikubali ktk misisngi ya kisayansi na ya kikweli kufuatana na viwango halisi vya ustadi na umahiri ktk fani tunazoshiriki na siyo kusema uongo kwa kufikiri kwamba huo ndio uzalendo na ndio uungwana kwa msingi kwamba itawapa moyo endelevu wahusika wa fani .tusema ukweli tukosoe na tujikubali kama hatuna ustadi ktk jambo fulani ili kwamba tuweze kuongeza bidii ya kujiinua kiustadi
ofcourse ninaposema ukososaji ni ule ukososji endelevu wenye kujenga .
ni wazi kabisa kanumba amedanganya na sijui ni kwa sababu gani,anajua yeye mwenyewe
sijui nini hasa lengo la kujikweza kusiko endelevu kiasi hicho? yaani kusiko na busara endelevu pia ?
nimesikitishwa sana kama msanii mwanafunzi ktk fani hii ya sinema
Raceznobar

Anonymous said...

Soma toleo recent la Raia Mwema. Kanumba bado sana katika kuigiza, badala ya kujisifu, aongeze juhudi na kusikiliza kwa makini critcs, hapo ataendelea. Unamsifia mtu ambaye anajitahidi kufika, sio yule ambaye hajafika, unamsifia, badala yake unampoteza njia tu!