Friday, January 04, 2008

Obama ashinda Uchaguzi wa awali Iowa!

Mbaguzi Jefferson Davis

Senator Barack Obama (Illinois)


Sijui niseme ni miujiza au ni kuwa Marekani inabadilika katika maswala ya rangi ya binadamu. Senator Barack Obama, ambaye baba yake ni MKenya na mama yake ni mzungu, kashinda katika uchaguzi wa urais upande wa Democrats huko Iowa. Obama ni mweusi na asilimia 95% ya wananchi wa Iowa ni wazungu. Wiki ijayo New Hampshire watapiga kura zao za awali.

Kama umefuatilia habari za ubaguzi hapa Marekani, lazima unaelewa kuwa ni vigumu sana mtu mweusi kupanda hivyo katika siasa za Marekani. Watu wengi wanasema kuwa hawakutarajia kuona mtu mweusi anafika mbali hivyo katika ugomebeaji wa uraisi Marekani.

Ubaguzi ulivyokuwa mbaya kuna weusi walisema kuwa hawatampigia kura maana wanahofia kuwa akichaguliwa kuwa rais atauliwa na wazungu wabaguzi kama Martin Luther King Jr. na Medgar Evers! Hofu yao si ya kuchekwa maana Obama amepewa ulinzi wa Secret Service mapema kabla ya wagombea wengine. Hiyo ni kwa sababu hao wabaguzi walitishia kumwua.

Na kuna maajabu mengine kuhusu Obama. Mama yake mzazi ni mjukuu wa Jefferson Davis! Kwa wasiojua historia ya Marekani, Jefferson Davis alikuwa rais wa kwanza na wa pekee wa Confederacy hapa Marekani. Hiyo Confederacy walitaka utumwa wa weusi udumu na ndo waliopigana na watu wa Union na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe hapa Marekani. Weusi wangekuwa bado utumwani kama wasingeangushwa na Union!

Lazima huyo Jefferson Davis alijigeuza kaburini kwake alivyopata mtukuu mweusi, na anajigeuza tena kuona kuwa huyo mtukuu mweusi anakaribira kuwa rais wa Marekani.

Ukweli watu Marekani wamechoka na hao Repeblicans. Wamechoka ukoo wa Bush na uongo wao uliosababisha vita isiyo na maana huko Iraq. Wamechoka kuona hali ya maisha inashuka kwa Mmarekani wa kawaida huko matajiri wanazidi kutajirika, asante Bush. Pia kwa wanaokumbuka Bush aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa rais bei ya mafuta itashuka. Mbona bei imezidi mara mbili na hao wenye kampuni ya mafuta (wakiwemo familia yake) wamo!

Obama ameahidi kuwa akichaguliwa kutakuwa na mageuzi Marekani! Ningependa kuona anachaguliwa na kuona kama atafanya mageuzi ya kweli!

Mungu abariki na awalinde Senator Barack Hussein Obama na familia yake! Safari bado ni ndefu!

2 comments:

Anonymous said...

mmmh! Obama amerithi masikio ya babu yake mbaguzi! LOL!

Anonymous said...

Lakini bado kuna wanaomkejeli kibaguzi. Hivi karibuni niliangalia comedy moja ambayo walikuwa waaelezea mabadiliko yanayotokea Marekani, aliyekuwa anaigiza kama MC akasema "Ladies and Gentlemen, give a warm welcome to the president of the USA, Mr Osama!" Basi akatokea mtu mwenye sura kama Obama na anaongea sauti kama ya kwake! Sijui kama walimaanisha nini, kwangu niliona kama wanaonya wazungu wenzao kuwa kwa mwendo huu kuna siku atakuja mjukuu wa Osama kugombea urais wa Marekani. Lakini zaidi niliiona kama propaganda dhidi ya Obama.