Monday, January 21, 2008

Ubaguzi Marekani

Mtu mweusi aliweza kuuliwa kwa sababu ndogo tu kama vile kumsemesha mzungu au kutokupisha nijiani! Siku za ya kuua ilikuwa picnic kwa wazungu kama vile wanaenda kwenya show!


Weusi walikuwa na sehemu zao za kungojea basi, na treni!
Walikuwa na sehemu tofauti za kunywea maji! (kabla ya maji ya chupa)
Mji mingine walikuwa na serikali tofauti!

10 comments:

Anonymous said...

Ilikuwa poa sana maana kwa kila mwafirika na mgeni aliyemaliza shule alirudi kwao , Sasa hivi tumeganda huku wengine shule haziishi kila ukitaka kumaliza unategewa mtoto na kama uko NH ,VT au RI utaishia kuwa digrii ya watoto shombeshombe angalia akina aggrey awori ,George saitoti , idris rashid na jonas kipokola si walisoma hapa tena kipindi hicho na walipomaliza tuu mkuku bongo hawakutaka kutoa kichwa na mtu lakini sasa hivi baby shower ndo graduation zetu.

Anonymous said...

Wengi kutoka nchi za nje walirudi makwao. Kisa cha kukaa kama mbwa. Hata mbwa alikuwa na thamani kuliko mtu mweusi enzi hizo. Na bado kuna ubaguzi hapo USA. Kaeni tu!

Anonymous said...

Anon wahapo juu umenichekesha sana sasa na wewe umerudi home au ndio umebanwaaaaaaa

Anonymous said...

Wazungu washenzi hata hii leo! Wao walikuwa na haki gani ya kuwaua weusi wakati hata wao walizamia kwenye nchi isiyo yao? Wenye nchi (Wahindi Wekundu) ndo walikuwa na haki ya kukataa wageni na si wakuja (wazungu)!

Anonymous said...

nikionacho siamini macho yangu hivi mambo haya ni kweli yalikuwepo au tunawasingizia!
mdau morogoro

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 1:03AM. Mambo hayo yalikuwepo na bado yapo! Juzi dada fulani mweusi aliuliwa na mzungu kwa kupigwa risasi akiwa amekaa ndani ya gari yake. Kijana mzungu alisema alimwua kwa vile anachukia watu weusi!

Ubaguzi bado upo Marekani. Watu wasikudanganye. Ukinunua nyumba eneo ya wazungu bado unaweza kuchomea. Familia fulani kutoka Liberia walinunua nyumba West Roxbury karibu na Boston. Wale wazungu waliichoma kabla hawajahamia!

Pia naomba ufanye sachi kwenye neti kuhusu utumwa Marekani.

Anonymous said...

Da chemi mzungu hata ufanyaje anachukia weusi,niko uk naboreka maana british ni wabaguzi kupita kiasi,especial baada ya wapolish kuja black hawatuhitaji kila huduma tunayopewa ni duni ,cha kushanganza kuna black wanaapa kuwa bora wafe huku kuliko kurudi AFRICA,IMEFIKIA HATUA GAZETI MOJA LINASEMA SEHEMU WANAZOISHI WEUSI WENGI ZINAMAGONJWA ZAIDI,MFANO RICKET,TB N.K.

Anonymous said...

Someni kitabu 'The Key to the Colors'. Humo utajua kwa nini wazungu wako hivyo, na kwa nini umshukuru Muumba wako alikuumba Mwafrika!

Anonymous said...

Chemmi, tena ungemhakikishia mdau wako kuwa hayo mambo anayoyaona hapo sio ya zamani sana bali ni miaka ya 1950 na kuja mbele. Lakini
angalia viongozi wetu wanavyowapapatikia....

Anonymous said...

Na bado weusi wananyongwa, wanasingiziwa na kufungwa maisha, wanapewa sumu kwenye madawa ya kulevya, wanapata ajali za ajabu! Acha tu. Ukiingia dukani wakakucheki wewe mweusi huko mzungu anaiba!