Sunday, January 27, 2008

Maelfu wajitokeza kwenye Casting Call Boston


Maelfu na maelfu ya watu wanaotaka kuwa Extras katika sinema mpya ya Martin Scorsese, Ashecliffe, walijitokeza jana Boston University. Watu walianza kupanga foleni tangu saa 12 asubuhi!

Mimi nilifika saa 8:30 (2:30Pm). Walikuwa wanaingiza watu kama 300 kwa mpigo kwenye ukumbini. Tulipewa lecture kuhusu kazi ya Extra. Siku inaweza kuwa ndefu masaa 12 hadi 16, fanya kama mnavoambiwa. Fika saa uliyopangiwa etc. Walitaja na bei ya malipo, dola $100 (Masaa manane) kwa siku plus overtime, kwa wasio union. Watapiga sinema maeneo ya Boston, Medfield na Taunton, Massachusetts kuanzia Machi 6 hadi mwisho wa Juni.

Baada ya hapo, watu walipanga foleni nyingine na kutoa fomu na kipigwa picha. Weusi walikuwa wachache sana kulinganishwa na idadi ya wazungu. Najua wengi wa weusi waliotokea watapata nafasi kwenye hiyo filamu.

Kufika mezani niliwapa Acting resume na headshot. Niliulizwa kama nimewahi kuactin kama Nurse. Nikawaambia ndio, niliwahi kuacti Nurse Malika kaitika sinema, Maangamizi the Ancient One.

Kama tunavyosema kwenye dunia ya acting, 'Break a Leg'. Kama kuna mdau aliyeenda huko karibu mtoe experience yako katika hiyo Casting Call.

Kwa habari zaidi soma:

http://wbztv.com/local/Martin.Scorsese.Leonardo.2.638533.html

4 comments:

Anonymous said...

DOH! Yaani ukitaka kuwa katika sinema kuna kazi kumbe! DOH! una moyo Da'Chemi!

Anonymous said...

Na wewe kwa kujisifia hujambo.Ndio mnaompoteza Kanumba

Chemi Che-Mponda said...

Wewe anonymous wa 11:29am, najisifia kwa vipi? Acting Marekani ina process, wanaotaka kujifunza wasome wajifunze. Kanumba ni superstar -lead actor, mimi ni extra, nitampoteza kweli?

Anonymous said...

Hi Chemi I'm so proud of you keep it up. Remember Chemi "there is no rule for success but the rule of failure is trying to please every body" wish u all the best. Back to you "anonymous" posted on Jan 28,2008 @ 11:29 AM just Zip it up looks like ur a big time looser get a life.