Thursday, January 17, 2008

Steven Kanumba apata Tuzo Hollywood???




Kaka Kanumba, nimeulizwa na wengi na sina jibu. Ni Tuzo gani uliyopata huko Hollywood? Je, wafadhili wametoa Press Release, je umefanya press conference? Ni tarehe gani ulikabidhiwa? Je, ni akina nani wengine waliopata maana kama ni International awards lazima kuna wengine waliopata pia kutoka nchi zaidi ya Nigeria. Ulipata kwa ajili ya sinema gani na ulicheza kama nani?

Hiyo Trophy inafanana sana na zile unazaopata kwenye souvenir store huko Hollywood. Tena ukiongeza hela wanaweka na jina. Haifanani na Oscar maana ni mwiko kampuni yoyote kutengeneza replica (inayofanana). Tunaomba jina la Award Committee.

Tueleze kusudi tukupambe na tukupongeze kama unavyostahili maana kama ni kweli ni habari kubwa sana! Na ukirudi Tanzania ni lazima upokelewe kwa shangwe.

22 comments:

Anonymous said...

Guys, hata mimi maswali hayo nimejiuliza sana. Infakti naona tuzo hizyo ni kama bosheni vile. hembu mlioko kwa joji kichaka, tupeni faktis kuhusu tuzo hilo na wengine waliopata.

Anonymous said...

Yani ndicho kinachonifanya nikuheshimu Da Chemi na Blog yako.Nadhani ni kama uliingia akilini mwa wengi tunaotatizwa na habari hii.Sio kwamba watanzania wasingependa Kanumba apate award huko Hollywood,bali nadhani jinsi habari hizo zinavyotoka kwenye magazeti ya udaku zinapoteza maana nzima.I hope Bwana Kanumba atakuwa amesoma maswali uliyotoa,na tunasuburi kwa hamu majibu yake.
Big up,Da Chemi

Anonymous said...

Kanumba, na mimi nina swali. Ulipat na cash prize pia? Yaani hela?

Anonymous said...

Kanumba acha ushamba, mtu akipokea award hama hiyo ana vaa TUXEDO siyo sweatshirt.

Anonymous said...

Alright,here's the hard facts:

1)The Academy awards are on February 24th,that is,next month.It's the 17th of January :|

2)They give the Oscar...AT the Oscars.They don't hand them out at Universal Studios in front of a Coca Cola hut :|

3)No one from Africa is nominated for an Academy award.No.One.

4)That statue bears some of the fakest Gold I've laid my eyes upon.Real Gold sparkles and s-h-i-n-e-s when the Sun is out.

5)Kanumba has about a 0.0001% chance of winning an ACTUAL Oscar in his lifetime.Sorry,but that's what we call the harsh truth.

Now let's move on to something else,perhaps something with an element of TRUTH and REALISM.Like,oooh say,Obama kicking Hilary's ass in South Carolina?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 1:59PM, you are wrong on Number 3. Several Africans been nominated, Djimon Hounsou (Benin), Sophie Okenedo (Nigeria), Thandie Newton (Zimbabwe)and Charlize Theron (mzungu from South Africa). Charlize won!

Truthfully it would be very difficult to get in a position where you can even compete for one.

I played the role of Nurse Malika in the film, Maangamizi the Ancient One. It was nominated by Tanzania in 2001 for the Academy Awards. It did not make the Top 5. That is the closet I got, but it was for the film and not as an actor.

Mind you the Committee that awards the Foreign Oscars is different from the committee that nominates the other categories is Best Actor etc.
Hiyo Academy imejaa siasa za rangi. Naweza kuzungumia siku nyingine.

Anonymous said...

Da Chemi...will your movie Bongoland II be nominated for those awards you spoke of? When it coming out anyway or is it out already.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous of 7:23am, thank-you for your comments. Bongoland II is in post-production. It is not yet ready for theatrical release.

I expect it to win some awards but no, it will not make it to the Oscars unless it is submitted by Tanzania in the Foreign Language categories. I hope that the Tanzanian nomination committee will find it worthy of being submitted as the 2nd film from Tanzania for consideration.

We shall see.

Anonymous said...

"you are wrong on Number 3. Several Africans been nominated, Djimon Hounsou (Benin), Sophie Okenedo (Nigeria), Thandie Newton (Zimbabwe)and Charlize Theron (mzungu from South Africa). Charlize won!"

I was talking about the Oscars Awards for this year,not every year ;)
They haven't released the nominees yet,but going by the movies that have come out last year,I can SAFELY say that my fellow Africans aren't winning anything this time around.

C'mon now,you as well as I know that Kanumba ain't won no Oscar.That 0.0001% may have been an overstatement,but we all know what it takes to win an Oscar:

1)Looks
2)Excellent critic reception and media coverage of a movie you've starred in.
3)Connections.

On the looks side,well,Kanumba is Kanumba-i'll leave it at that.On the critic reception side,I ain't heard no Kanumba film review by Roger Ebert.On the connections side,he has none,plain and simple.

I work in the music industry so I don't know much about how the movie studio agents scout for foreign/oversea talent,but one thing that I do know is that if you from Africa,specifically,Tanzania,and you're trying to make it over here?Chances are,you're on the bottom of the Scout's list,and you ain't winning no Oscar without an INCREDIBLE amount of talent AND media attention.

Anonymous said...

masifa tu labda kajichongea mwenyewe anacheza na hollywood huyo na zee zee zake

Anonymous said...

Jamani hii kali.Yaani its obvious kabisa Kanumba kaamua kudanganya umma wa watanzania.And he even wasted his time to pose with such a cheap replica.Unajua ushamba inabidi uwe na mipaka.Hii imezidi.Umeenda kupokea award muhimu hivyo,na sweta?!!!!Hollywood!!!Kanumba hapa umejiabisha kupita maelezo.Ingekuwa huku Marekani..this could be the end of your career.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous of 8:12PM, I have to agree with you that I have also not heard of any buzz in regards to an African actor or an African film this year in the foreign categort. We shall see.

Of course Kanumba cannot win an Oscar until he has acted in a film and it better be of good qaulity. I checked and found that the Nigerian productions are not considered films but video productions. Mr. Ebert does not review videos.

Yes, to win an Oscar you need a great film, great director and most important a great script!

I have to disagree with you on the Looks aspect. Yes looks help but these days even ugly people and fat people can win and Oscar. Their acting has to be superb though.

Anonymous said...

We chemi, fat people wana nini mpaka unawatofautisha na wengine ..eti even fat people!! Jamani waafrika miili yetu ndivyo imeumbwa acheni kujishindisha njaa ili mkonde!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 8:55, huko Hollywood wanatofautisha sana saizi ya mtu. Kama wewe ni zaidi ya size 6 wewe ni Fat. Huoni walivyokondeana mpaka unaona mifupa?

Camryn Manheim alipopata Oscar alisema, "This is for the Fat People". Kwanza hakutegemea kushinda kwa sababu alijua unene utamponza.

Hata wanaume wa Hollywood wamekondeana.

Siku hizi wanaitwa Heayset, hata mimi nikituma acting resume inabidi niandike Heavyset. Si mbaya maana kwenye commercial fulani walitaka Heavyset Black woman. Nilituma resume na picha na nilipata hiyo commercial, japo unaniona sekunde moja.

Anonymous said...

"I have to disagree with you on the Looks aspect. Yes looks help but these days even ugly people and fat people can win and Oscar. Their acting has to be superb though."

To me(the way I see it,that is)looks and talent go hand in hand in the Hollywood of today.

That's not to say that if you look 'good' according to Hollywood standards(You know-Tall,Slim/Buff,sharp Facial features etc)you're guaranteed an Oscar,but if you've got talent AND look 'good',your chances of getting the good roles are greater.You get a good role=you get more media attention.And more media attention leads to more interest from critics and movie-goers,and this ultimately leads to nominations.

I agree,being Fat/Overweight isn't a barrier to a nomination/Oscar win,but if you are packing a few extra pounds,you better be one hell of an Actor/Actress.This is why you have a lot of successful Fat Comedic Actors/Actresses,because Comedic films don't lean heavily on the Actor's/Actresses looks in the same way a Drama/Action/Thriller film does,it's all about verbal humor,and putting the actor/actress in a funny and quirky situation in Comedy movies.

Now,back to the lying Actor.Kanumba doesn't have the typical African American looks,nor does his features stand out from the millions of other struggling black actors,this is the first problem.The second problem is,his history/background is not 'grabbing' enough to draw mass interest,at the end of the day,he's simply a black foreign actor that hails from a 3rd world country.The third problem is directly connected to the second one,but this one has to do with Language;Can he speak fluently enough in English?I've heard him talk,sadly,the answer to this is no.

To sum this all up; Kanumba PRESENTLY does not have what it takes to make it as an actor in America.You have other Tanzanians that have established a considerable amount of interest in American organizations/institutions,such as your Hashim(The college basketball player),you got your Cynthia Masasi(The hip hop video girl),and others.Both of these,have what it takes to make it in their field,Hashim has the height that generates him interest and praise,Cynthia has the 'typical' video girl looks that generate her interest.Kanumba?Unless he enrolls in a lot of English and Acting courses and starts hitting the Gym hard,he's going nowhere in Hollywood.

Anonymous said...

"Jamani waafrika miili yetu ndivyo imeumbwa"

No no no,being overweight has absolutely NOTHING to do with your heritage.That's equivalent to me saying that Asians are good at Math because they're Asian.

Makes no sense at all.

Anonymous said...

jamani tutadanganyana mpaka lini,ukweli ni kwamba hata mimi ningekuwa tanzania ningedanganywa,tuzo gani hiyo inayotolewa barabarani?
ukweli ni kwamba hata mimi ninayo tuzo inayofanana na ya oscar nilipewa shule,ambayo ndiyo ameishika kanumba.
na hao washenzi wanaochapisha magazeti ya udaku wanatoa tu uongo kama walivyosema solothang yupo finland anaandaa album kumbe yupo hapa ireland amejilipua.
chemi,lazima unajuana na hao wa magazeti ya udaku au mtumie hata michuzi wawaambie kwamba hiyo habari ni ya uongo,maana wewe ukweli unaujua,usiache watanzania walionyumbani waongopewe.

Anonymous said...

Dada Chemi Chemponda naomba ni ku sahihishe kidogo , Camryn Manheim hajawahi pata tuzo ya Oscar wala kuwa nomminated , aliposema "This is for the Fat People". ilikuwa ni alipo shinda tuzo ya Emmy na kwa usahihi alisema "This is for the Fat girls ".

....naomba swali kwako, wewe ni ulikua mmoja wa Black Sisters?

Anonymous said...

Ngoja nishangae km waruguru jaaaa huu ushamba wa hali ya juu,kanumba usifikiri watz hawana habari ya mambo yanavyokwenda,watz wapo wengi kila kona ya dunia hii,na mi mwenyewe naishi huko los-angeles hiyo award mbona cjaickia,kweli ujanja ukizidi kinachofuata ni kuitwa mshamba,acha upuuuuzi wako watz wapo juu na wanajua kila kitu karne hii,umenunua kijimbao hiko unadai zawadi,mwehu kitu gani

Chemi Che-Mponda said...

Aisei! Anonymous wa 5:10PM asante sana kwa sahisho. Ni kweli Camryn alishinda kwenye Emmys na siyo Oscar. Niliangalia hiyo na nakumbuka alivyonyanyua tuzo lake juu na kusema maneno hayo. Huwa kila mwaka naangalia Award shows kuanzia mwanzo hadi mwisho mpaka sasa ukiniuliza naweza kuchanganya mwaka wa ushindi. Mwaka huu tumenyimwa uhondo shauri ya mgomo wa waandishi wa WGA.

Haya heavyset wa kike wengine walioshinda Oscars ni Shelley Winters (1973), Jennifer Hudson (2007), Hattie McDaniel (1939), Geraldine Page (1986), na Marie Dressler (1931 & 1932).

Anonymous said...

Ni LAZIMA Kanumba aombe msamaha akirudi Tanzania. Amedanganya umati kuhusu ushindi wake eti Tanzania achievement award kutoka Universal Studio na John Wayne International Award. Hakuna kitu kama hicho.

Anonymous said...

Nilimnunulia mwanangu Statue kama hiyo kama zawadi ya Christmas. Ina jina lake kabisa. Uzuri alisema kuwa iko siku atapata Oscar ya kweli.