Tuesday, April 20, 2010

Flaviana Matata Na Russell Simmons


Aisei, wiki hii na siku zijazo utasikia Tanzania, na jina la mrembo wetu Flaviana Matata ikitajwa sana huko Hollywood. Habari kutoka Hollywood zinasema kuwa Flaviana Matata yuko kwenye uhusiano na Russell Simmons. Wanasema kuwa wamekuwa pamoja kama miezi mitatu ila wiki hii ndo habari zimekuwa wazi kwa kila mtu kujua.

Hongera Flaviana, wakilisha Tanzania!

Hebu someni habari wanazoandika na badooo.... wengine wamempachika Flaviana jina BALDILOCKS! (Mwenye upara). Wengine wanasema huyo Simmons ni mzee mno kwa Flaviana. Wengine wanasema kuwa Flaviana mrembo na Simmons ana sura mbaya...yaani.

Wengine wanasema kwa vile Kimora Lee Simmons aliamua kuzaa na Djimon Hounsou (Mwafrika) naye Simmons analipiza kisasi kwa kumchukua Mwafrika.....yaani maneno. Kimora na Simmons waliachana mwaka 2006. Simmons ni tajiri aliyewahi kuwa CEO wa kampuni Phat Farm, na pia ana kampuni ya muziki.

Lakini namtakia Flaviana mafanikio mema. Ajiendeleze katika fani ya umodel. Flaviana ana mkataba na kampuni ya Umodel New York. HONGERA! Waonyeshe urembo asili ni nini!

Mapenzi ni mapenzi. Kama wamependana, wamependana. LOVE IS BLIND! Na kumbuka watu watasema, mwisho watachoka!

Kwa habari zaidi someni:

http://juicycelebgossip.wordpress.com/2010/04/19/russell-simmons-is-in-a-new-relationship-with-a-former-miss-tanzania/

http://www.honeymag.com/2010/honeymag/who-is-russell-simmons-new-boo/

http://bossip.com/238971/who-is-choppin-this-thang-down/

http://fashionjunkii.onsugar.com/Flaviana-Matata-Face-Forward-Nylon-mag-April-2010-8031036

http://blog.mtviggy.com/2010/04/19/flaviana-matata-the-original-hottest-bald-model/

17 comments:

Fadhy Mtanga said...

Wenye kusema waseme sana lakini mapenzi ni ya wawili. Heko mdada.

Anonymous said...

Hongera Flaviana! Wala usijali hao wenye wivu. Kupata Millionaire mmarekani si mchezo. Ila naomba usisahau kwenu! Jenga shule kwneyu, somesha ndugu zako.

Anonymous said...

Ameukata dada wa watu! Hongela!

Anonymous said...

Russell Simmons,ni kaka wa Run-DMC,
kama mtamkumbuka yeye alikuwa rappa maarufu sana enzi hizo.

Ndio,Russell ni mtu mzima lakini ukiachana na mambo ya mshiko bado anaoneka na mvuto tofauti na umri wake,kwa hiyo si flaviana tu, msichana yeyote anaweza kuanguka kwenye kwenye penzi vilevile.
ananyuka pamba wala hapitwi na wakati,si unajua mzee wa ma-fashion,kwa hiyo kuchukua ana-fit kuchukua model.
zaidi ya hayo,Russell si mtu wa skendo za ki-california.yeye na familia yake ni wacha mungu,kwa hiyo hapo dada nafikiri ameangukia kwenye mikono ambayo haiwezi kumwaribia kwenye maisha yake ya mbeleni

Anonymous said...

Anaoa au anachezea tu kisha anaacha. Kama ni kuchezea mimi sioni sifa yoyote ile.

Nautiakasi said...

Hahahah Da Chemi MB*#&o ya mwezio we ukaivalia kibwaya ina huuuuuu?

Anonymous said...

Ataoa Spring Chicken.

Anonymous said...

Hakuna lolote hapo jamaa ni kicheche tu....ameshakuwa na mademu kibao kabla ya Flaviana....Cha msingi dada yangu Flaviana wewe mchune kwa sana kabla ajakupiga chini.

cheap said...

bado sielewi hongera ni ya nini hapo? kupata mwanamme tajiri? au kupata mwanamme? kama swala ni kupata mwanamme kipi kipya? na kama ni kupata mwanamme tajiri, hivi ni kweli chemi unampa mtu hongera eti kwa sababu ana mwanamme tajiri?

Anonymous said...

Uongo mbaya watu watataka kujua Tanzania iko wapi na huenda utalii ukaongeza. Wanampwna Flaiana kama ni exotic.

Anonymous said...

she is furthering her career and he is "helping"...

Anonymous said...

Hongera Flaviana. Wanaokuonea wivu walie tu! ENJOY!

Anonymous said...

Hata akina beyonse, walianzia hivi. na kina jz wenye mahela, ili wawapandishe chati.

Anonymous said...

As far as I’m concerned, CHEMI isn’t to be blamed for outrageously supporting Miss MATATA’s course (refer a comment from ‘Cheap’). In fact, today’s Western world is predominantly materialistic and CHEMI has been living there for sometime and she has imbedded the mainstream culture of the west. Needless to say, in western world, money doesn’t talk, it shouts loudly!

Take an example of Tiger Woods’ transgressions. For those women involved is not big shame at all, instead it’s a big source of ‘income’! In fact, the more they reveal on how Mr Woods dropped their knickers down, the more the dollars go into their ‘greedy’ accounts! This is bizarre!

I don’t know what exactly going on between the pair but if what has been reported is to be the case (they are an item!) then I should warn Miss MATATA to be prepared for life in the media! She will be scrutinised from what pair of pants she’s wearing to the type of sex they had a day before! Welcome to the fame life of HOLLYWOOD, babe!
---------------
Jua Kali

Anonymous said...

OHH LALAAA!!KWELI DADA ZETU SIKU ZOTE NI VICHWA MAJI ETI WANAPEANA HONGERA KWA KUPATA WANAUME!!HUU NI UMASKINI WA KIFIKRA HAMUONI KAMA MNAJIDHALILISHA KUTUMIWA KAMA BIDHAA?MAANA UKIJISIFU UMEPATA MWANAUME TAJIRI MAANA WEWE UMEGEUKA KUWA BIDHAA!!KILA MWENYEPESA AMA MWENYE UTAITO ATAKUTUMIA AMA KUNUNUA!!HII AIBU YANI SISTER CHEMI NILIKUWA NAKUONA NI MTU MZIMA UNAAKILI KUMBE HOVYO KABISA NIWALEWALE!!NA MIDUME MENGINE NAYO WENYEKUSEMA NAWASEME!!JAMANI MWANAMKE SIOCHOMBO CHA KUTUMIA,UCHI SIO SWALA LA KUUZA NI KITU CHA KUKIPA THAMANI NIAIBU KUUZA AMA KUTEMBEA NA MTU KISA PESA!!NDIYO MAANA WAAFRIKA POPOTE PALE TUNADHARAURIKA!!ME NITAMHESHIMU MAMA YANGU TU MAANA WANAWAKE WENGINE WOTE MNAFANANA AKILI ZENU!!HILI NI JAMBO LA AIBU KULIWEKA MTANDAONI!!DADA ZETU MNABABAIKA SANA NA WAZUNGU NA WATU WENYE MAJINA NDIO MAANA MNAFANYWAGA VIBAYA!!KICHEFUCHEFU

Mumu said...

Anony wa 11:33am, huenda wamependana kweli. Unajuaje kama kampenda jamaa sababu ya pesa?

Anonymous said...

Kweli ukitizama picha unaweza kusema mtu na baba yake. Lakini Bongo wazee wangapi wanaoa masping chikeni? Wache kama walivyo!