Saturday, April 10, 2010

Misiba

Askofu Abel Muzorewa wa Zimbabwe amefariki dunia. Habari zinasema Askofu Muzorewa amefariki dunia mjini Harare jana Ijumaa. Alikuwa na miaka 85. Askofu Muzorewa alikuwa anaitwa 'puppet' (kibaraka) wa wazungu kwa vile alijaribu kupooza waafrika wasitake uhuru Zimbabwe. Alikuwa waziri mkuu katika utawala wa mbaguzi Ian Smith.

Kwa habari zaidi someni:
Rais wa Poland, Lech Kaczynski na mke wake wamefariki katika ajali ya ndege usiku wa kuamkia leo. Ndege hiyo ya raisiilikuwa inajaribu kutua huko Urusi wakati wa ajali. Habari zinasema kwa kulikuwa na viongozi wengine wakuu na wakuu wa jeshi kwenye hiyo ndege. Watu 132 wamefariki katika ajali hiyo.

Kwa habari zaidi soma:

Aliyewahi kuwa Chifu wa wahindi wekundu, kabila ya Cherokee, hapa Marekani, Chifu Wilma Mankiller amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa. Chifu Mankiller alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza kabila la Cherokee.

Kama mnafahamu historia ya Marekani, wazungu waliwakuta hao wahindi wekundu hapa. Waliwaua kwa njia mbalimbali....kuwapiga risasi, kuwapa sumu, kuwaambukiza magonjwa kama smallpox kwa makusidi kusudi wafe. Nia yao ilikuwa kuiba ardhi ya na wazungu walifanikiwa kufanya hivyo!

Mnaweza kusoma habari zaidi hapa:

http://www.google.com/hostednews/ap/article/ALeqM5jmKy3_vtUk06fgt2_rFw9nSis-EwD9F028NG0


*********************************************
Kwa wenye watoto Marekani wataijua sinema ya The Wizard of Oz. Meinhardt Raabe ambaye aliigiza kama 'coroner' katika hiyo sinema amefariki dunia. alikuwa na miaka 95. Sinema the Wizard of Oz ilitoka mwaka 1939. Raabe alikuwa katika ile scene dorothy anapotua na nyumba yake 'Munchkinland' Nyumba inamwua mchawi mwenye roho mbaya wa magharibi.

Meinhardt Raabe, who played the Munchkin coroner in "The Wizard of Oz" and proclaimed in the movie that the Wicked Witch of the East was "really most sincerely dead," has died. He was 94.

His caregiver, Cindy Bosnyak, said Raabe - pronounced RAH'-bee - died Friday morning at a hospital in Orange Park, Fla. He was one of the few surviving Munchkins from the 1939 film.
Bosnyak said he complained of a sore throat at his retirement community before collapsing and going into cardiac arrest. He was taken to Orange Park Medical Center, where he later died, she said.

Kwa habari zaidi soma:

http://www.myfoxla.com/dpp/entertainment/celebrity_news/meinhardt-raabe-oz-munchkin-dies-at-94-20100409

No comments: