Tuesday, April 06, 2010

Mbaguzi Eugene Terreblanche Ameuwawa!

Wadau, sijui tusherekee au tuwe na majonzi. Mbaguzi Eugene Terreblanche ameuwawa huko Afrika Kusini na wafanyakazi wake wawili. Waliomwua ni vijana wenye miaka 21 na 16. Wamejisalimisha kwa polisi.

Huyo Terreblanche alikuwa ni mshenzi kupindukia, alikuwa hapendi uhuru kwa weusi, na alikuwa anaongoza kikundi cha wazungu wenye sias kali huko. Mikutano waliyokuwa anongoza ilikuwa inajaa wazungu wenye chuki dhidi ya weusi. Alikuwa na mtindo wa kutuma mbwa wake ku'gata watu weusi, na pia alijaribu kumwua mlinzi wake mweusi. Alitega mabomu zaidi ya 20 kabla ya uchaguzi wa kihistoria wa mwaka 1994 huko Afrika Kusini.

Kuna watakaosherekea kifo chake na watakaolia.

Mnaweza kusoma habari zaidi:

http://www.cnn.com/2010/WORLD/africa/04/04/south.africa.terreblanche/index.html?hpt=Sbin

4 comments:

Kaka Trio said...

Kama wana adamu wenye uanadamu siku zote si vizuri kuua. Kila kitu tunamkabidhi Mungu kama kupitia maombi ya watu Mungu kaitikia kwa kuwatumia vijana hao kumuondoa duniani ni sawa kama si mapenzi ya Mungu pia hatuna chochote cha kufurahia pale mtu anapouwawa hata kama kafanya makosa ya namna gani! Hatukumpa roho na hatuna mamlako ya kumtoa roho, hiyo ni kazi ya Muuumba.

Anonymous said...

Yuko motoni!

Anonymous said...

hao makaburu a.k.a boer warudi kwao uholanzi wasituleteee fujo kune africa yetu.get out africa zimbabwe,botswana bondeni kwote rudini kwenu europa africa na ya watu weusi tu.

mdau chaka zulu

mike pima said...

hapa watu wote weusi kwa ujumla wamefurahi wanasema This boy the do us big favour na waliandamana wale vijana walivopelekwa mahakamani. kaburu wanasema watafanya world cup isichezeke .wanachekesha kweli hikichama kina watu 50,000 tu nakinasambaratika.mumewao ndo vile tena kauliwa. hakuwalipa mshahara na akawasemea ovyo wakamrudia na panga