Saturday, April 17, 2010

Gavana Deval Patrick Akutana na Waafrika wa Massachusetts

Leo, Gavana wa Massachusetts, Bwana Deval Patrick, aliongea na waafrika waishio Massachusetts. Mkutano huo uliitwa African Town Hall. Ilifanyika Tobin Comunity Center mjini Boston.

Waafrika walitokea kutoka nchi nyingi za Afrika, hasa waafrika kutoka Magharibi walikuwa wengi. Wakutoka Afrika Mashariki tulikuwa wengi pia, hasa waGanda. Lakini kama nilivyotabiri, hao wa Magharibi walijaribu sana kuiteka mkutano. Ila nashangaa watu wengine hawaelewi kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Mkoa (State Government), na serikali kuu ya nchi (Federal Government) ambayo inaongozwa na Rais Obama. Wengine hawakuewelewa kuwa mambo mengine yanahusu serikali ya mji wanaokaa na si mkoa.

Masuala makuu yaliongolewa, ni elimu kwa wahamiaji, bima ya afya, na umuhimu wa census hasa. Kuna waafrika walisema kuna wana majina ya kiislamu na walihofia kuwa wakijaza fomu watanyanyaswa. Wengine walisema kuwa hawana makatarasi na walihofia kukamatwa wakirudisha fomu. Wasaidizi wa Gavana pia walijaribu kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa fomu hizo na kuwa haziendi uhamiaji. Kwenye bima ya afya alisema kuwa baada ya mwezi Agosti itakuwa rahisi zaidi kuipata. Pia alisema kuwa wanajitahidi kuruhusu wanafunzi wasio na makaratasi wanaokaa Massachusetts waweze kulipa ada ya 'In State' kama wakisoma katika State Colleges.


Gavana Patrick aliwaomba waafrika wampigie kura katika uchaguzi ujao na waombe ndugu na marafiki wampigie pia.

****************************************************************************


Wasichana wa KiGanda wakicheza ngoma ya asili kumwingiza Gavana kwenye Ukumbi. Gavana yuko nyyuma yao anasalimiana na watu.
Gavana Patrick akielezea hatua alizochukua kama Gavana ilikusaidia wahamiaji wanaokaa Massachusetts.

Gavana Patrick aliwahimiza waafrika wajaze fomu za Census. Aliwaambia watu wasijali kama wana makaratasi au hawana, maana si fomu ya uhamiaji bali fomu ya kujua kuna watu wangapi katika eneo fulani serikali iweze kuwapa huduma ya kutosha, kama shule, hospitali,polisi.

Hao waGanda walipiga ngoma wakati Gavana anaiingia ukumbini. Gavana alifurahi sana.

Huyo MKameroon, alichekesha watu pamoja na Gavana alipoomba waafrika wasinyangywe chakula chao cha asili wakitua katika uwanja wa ndege (Logan Airport) Boston. Gavana alimjibu kuwa ana imani kuwa chakula hicho ni kizuri, lakini hizo ni sheria za serikali kuu ya nchi (Federal) na yeye mwenyewe hawezi kuvunja sheria.

Viongozi wa kidini wa waafrika Massachusetts wakipiga picha na Gavana baada ya shughuli. Huyo mama Mngieria aliyeshika simu alikuwa alijaribu kuleta fujo wakati wa maswali na majibu. Dume MNigeria mwenzake kamkalisha chini!

Shughuli iliisha kwa fujo! Ilibidi walinzi wa Gavana wamzunguke na kumtoa kwenye mlango wa pembeni. Kisa, kila mtu alitaka kupiga picha naye. Jamani, Gavana alisukumwa!!!!! Ila lazima niseme sisi waTanzania ni wastaarabu sana. Sikumwona MTanzania akifanya fujo mle wala kushiri katika kundi la waliomsukuma na kumsakama ili apige picha naye. Shughuli ilianza vizuri, lakini iliisha vibaya!

1 comment:

Anonymous said...

Huyo Weste African ndo kaona chakula ndo muhimu kuliko masuala ya elimu na afya! Mimi nitakula pizza mradi nina elimu na huduma ya afya nzuri.