Thursday, July 08, 2010

Kumbukumbu - Siti Binti Saad 1880 -1950

Wadau, leo ni miaka sitini tangu mwimbaji maarufu wa Tanzania, malkia Original wa Mipasho, Siti Biti Saad afariki dunia.

Siti alizaliwa katika kijiji cha Fumba huko Zanzibar. Jina aliyopewa na wazazi wake ilikuwa Mtumwa. Wazazi wake walikuwa watumwa kutoka Bara. Aliishi maisha duni hadi alipohamia mjini Zanzibar na kuanza kupata umaarufu wa kuimba Taarab. Watu walimfurahia kwa vile alikuwa anaimba taarab kwa kiswahili lugha ambayo walikuwa wanatumia hasa ilikuwa kiaarabu.
Sultan alimwalika kuja kumwimbia. Baadaye alifanikiwa kwenda India na kikundi chake kurekodi santuri. Enzi zile zilikuwa zile 78's. Vijana wa siku hizi hawawezi kuzijua. Zilikuwa zinapigwa kwenye zile ,"His Master's Voice".

Marehemu Shabaan Robert alitunga kitabu, 'Wasifu wa Siti Binti Saad'. Anaelezea mengi kuhusu maisha ya Bibi Siti.

Siti Binti Saad 1880-1950

Siti na kikundi chake walipoenda Mumbai (Bombay), India kurekodi santuri kadhaa mwaka 1929.

Kwa habari zaidi za Siti Binti Saad someni:

http://www.zanzibarhistory.org/six_famous_zanzibari.htm

http://www.rhapsody.com/siti-binti-saad/feeds.html

5 comments:

Anonymous said...

Asante sana Dada Chemi. Siti binti Saad ni moja wa mashujaa wa Tanzania.

Anonymous said...

Chemi,

Samahani Sitti Sitawa Bint Saad hakuimba "mipasho". Sitti Bint Saad aliimba Taarab. Mipasho wanaimba kina Khadija Kopa.

Tafadhali mpe heshima anayostahili.

Chemi Che-Mponda said...

Mdau, wa 11:42pm, sijui mipasho kwa tafsiri ya leo, lakini Siti aliimba nyimbo zenye ujumbe kwa wana siasa wa wakati ule na pia zenye mafumbo. Wimbo wake 'Kijiti' unaweza kusema inahusu nini kama si kupasha polisi wa wakati ule na rushwa.

Tungeweza kuchambua nyimbo zote alizotunga, nina hakika kuwa hao wa leo hawamfikii.

Rose said...

Mimi naona Da Chemi hajakosea. Siti alikuwa anatoa mipasho kwa heshima si hii mitindo ya siku hizi ya kutukana ovyo ovyo! Hao wa siku hizi wameharibu. Hebu Bi Kidude atusaidie.

Anonymous said...

Asante kwa kutukumbusha kuhusu mchango wa Siti Binti Saad. Nashangaa sijasikia kitu kwenye media Bongo. Kweli sisi wabongo wepesi kusahau.