Tuesday, August 17, 2010

Michuzi Post


Habari Muhimu Kutoka kwa Kaka Michuzi

*********************************8
Asalaam Aleikhum Wadau,

Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya
la www.michuzipost.com ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika
kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa
kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza
kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa.

Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya
libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza
Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo
nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia
kuboresha libeneke hili.

Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama
ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion
sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu
kwa muda wote huu.

Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda
sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la
www.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamii
itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya
ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa
mapana na undani zaidi.

Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi
mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka
mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii
inavyojionesha http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments.

Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa
nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa
sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo
yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani
huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea
kama kawa.

Libeneke hili jipya la www.michuzi.post.com limewezekana kwa ushauri
na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw.
Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja
tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa
bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi
kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke
hili.


Muhidin Issa Michuzi
Mkurugenzi
Michuzi Post Ltd

2 comments:

emu-three said...

Tunampa hongera sana kwa kazi yake nzuri nasi tupo nyuma yake, maendeleo yake yanatupa faraja na sie kuwa huenda siku mojana sisi tuweza kama yeye

Anonymous said...

CCM OYEEEEE!!!!!!!!!!!!