Wednesday, February 09, 2011

Sinema - The Gift


Mimi na binti yangu (mwigizaji Mimi Augustin)

Devin, Mimi Augustin, Chemi na Charles Jackson aka Mzee Matumbi

Wiki iliyopita niligiza katika sinema fupi iitwayo 'The Gift' (Zawadi). Inatengenezwa na wanafunzi wa filamu wa Emerson College hapa Boston.
Sinema inahusu familia ya kiislamu ambao wanakaa Marekani halafu wanamchagulia binti yao mchumba. Awali ilikuwa sinema iigizwe na wahindi lakini waiigazji walikosekana kukamilisha familia katika sinema. Hivyo waliamua kufanya familia wawe waafrika. Sinema imepigwa katika 35MM format hivyo inabidi ipelekwe lab kusafishwa. Wamechanganya mambo ya kihindi ya kiafrika. Mfano kwenye arsui Bibi harusi kavaa nguo ya kihindi halafu kuna chakula cha kihindi. Natumaini itapendeza lakini. Huenda ikakamilika kabla ya mwezi wa sita.
Katika sinema hiyo, mimi niligiza kama Mama, Charles 'Matumbi' Jackson aliigiza kama Baba, Mimi Augustin aliigiza kama binti Anum, na Devin ndo Mchumba/Mume.

5 comments:

Anonymous said...

Umependenza Da Chemi, na huyo binti utadhani ndobinti yako wa kweli!

emu-three said...

Mhhh, safi sana, wewe ni `msanii kweli' hongera sana na wenzako pia. TUNAISUBIRI KWA HAMU HIYO SINEMA...

KWA KUTUVUTIA ZAIDI KAMA INAWEZEKANA UNAWEZA KUTUWEKEA `VIONJO' (TRAILER)

Anonymous said...

Da Chemi u look great

Anonymous said...

Da Chemi
Umependeza sana. I wish I could date you !!!Napenda akina mama wenye umri kama wa kwako, can I contact u ???

Shebby Biboze said...

ACHENI MAMBO YEBU YA KUTAKA KUTUKANA UISLAM KWANI HAKUNA WAZAZI WA KIKRISTO WANOACHAGULIA MABINTI ZAO UCHUMBA MPAKA MUHUSISHE UISLAM AU MNATAFUTA LAANA YA MWENYEZI MUNGU HEBU KM HAMNA LA KUFANYA BORA MKALIME TUU