Monday, February 14, 2011

Je, Bei ya Vyakula Vimepanda Huko Ulipo?

Wadau, jumamosi iliyopita nilienda dukani hapa Boston kununua vyakula vya wiki. Ajabu, nilikuta bei ya karibu kila kitu kimepanda! Mkate, maziwa, mayai, mafuta ya kupikia, sukari! Je, ulipo bei zimepanda pia? Wiki iliyopita bei ya kikombe cha kahawa kilipanda kwa senti 10 pia.

Naomba mtaje ulipo, na bei ya vyakula gani vimepanda.

4 comments:

Anonymous said...

Da Kemi we ndio umeona wiki hii wenzio Salt Lake City, Utah mimi nimegundua tangu Mwishoni mwaka jana yaani Dec! lkn kutangaza nimeona kwenye News last week, labda kuna sehemu walikuwa bado km huko kwenu

Anonymous said...

Wewe ni mshamba wa wapi? kutuuliza bei za vyakula kama zimepanda, kwa hiyo kama vimepanda unao uwezo wa kushusha bei? au umezubaa kwenye chumba chako huna la kufanya? nenda kanisani kama umeboweka.

Anonymous said...

Niko North Carolina. Ni kweli tumeona bei ya vitu ikipanda ghafla ingawa ni kwa senti 5 hadi 25. Kweli ukijumlisha vitu uavyonunua unaumia.

Anonymous said...

Tanzania bei za bidhaa zinazidi kupaa. Watanzania tuongezee bidii kuchapa kazi ili kukabiliana na hali hii. Vinginevyo maisha yatazidi kuwa magumu sana.