Wednesday, February 16, 2011

JWTZ na Mabomu

Hivi Jeshi la Wananchi Tanzania inashindwa kuhifadhi mabomu? Mwaka juzi mabomu yao yalilipuka Mbagala. Leo tunasikia yamelikpuka kambi la Gongo la Mboto. Hao wanaotunza mabomu wanafundishwa kuytatunza kweli? Au ni sabotage? AuTutasikia imekuaje miezi kadhaa baada ya Tume kuundwa na kutoa ripoti yake.

Mwaka 1984, nilipokuwa Masange JKT Tabora, kambi ilipewa ruhusa na Makao Makuu kutumia baruti (Dynamite) kutishia simba waliokuwa wanatusumbua. Hao simba wala watu waliua watu kadhaa katika kijiji cha jirani.

Haya, walipewa ruhusa na walikuwa walizitegesha. Aliyekuwa msimamizi alikuwa ni Luteni Usu. Sasa akatokea kuruta/private mwenye ujuzi na dynamite. Alikuwa mhandisi uraiani. Aliwaonya kuwa walikata utambi mfupi mno. Luteni usu alisema kuwa anajua anachofanya, na huyo 'msomi' anayamaze. Kuona wanakaribia kuwasha yule Kuruta alikimbia, waliwasha na walaiokuwepo walilipuliwa! Hakuna aliyakufa lakini jamaa moja alikatika mkono, Lusteni Usu alipofuka na wengine walipata majeraha kadhaa.

3 comments:

Anonymous said...

Sijawahi kuona hali ya kutisha kama hii!!!!!!!! Mimi nipo kama kilometa 8 kutoka eneo la tukio lakini mabomu yalikuwa yanapita juu kama missiles.
Hii serkali ni kipumbavu sana. mtawekaje mjini kambi za jeshi na mzifanye ndio stoo ya mabomu? Yaani wanajeshi na watawala they are foolish.
Nimechukia sana, kwa sababu walipata somo Mbagala badala ya kutafuta solution wame-concentrate kwenye wizi wa Dowans.
Rubbish all you in power

Mwananchi said...

Hivi hakuna utaratibu wowote wa kuharibu mabomu ya zamani katika makambi / maghala ya jeshi? Naongea hili sijajua sababu zitakazotolewa na msemaji wa Jeshi lakini hadithi isije ikawa ile ile ya kuwa ni ile stock ya mabomu ya zamani ambayo kimsingi yamepitwa na wakati. Je hakuna namna ya kuyaharibu badala ya kuyatunza? Na hili la haya maghala kukaa karibu na makazi ya watu serikali hailifahamu bado kuwa yanaweza kutokea madhara na hata maafa kwa mali na maisha? Ya Mbagala hayajaacha somo bado kwa wataalamu wetu wa kijeshi?

Hil tukio limetokea usiku Mungu saidia, watu walikuwa hawajalala, kama ingekuwa ndio usiku wa manane ingekuwaje? Na kwanini wahusika wakuu wasiwajibike kwa uzembe huu ambao hatujatambua hata athari na hasara zake?

Nini nafasi ya vyombo vya habari katika matukio kama haya? Mimi nilikuwa naanaglia TBC1 lakini hadi wanakuja kupitisha ujumbe kwenye screen tayari tushahangaika kutafuta habari bila mafanikio make tulikuwa tunawsiliana na ndugu zetu walioko Dar, na binafsi sikuona sababu ya kwanini wasisitishe mchezo wa kuigiza uliokuwepo ukiendelea na kutoa breaking news hata kutueleza kuwa kinachoendelea ni nini na tutafahamishwa zaidi kadiri muda na taarifa zinavyokuja? Hii ni dharula ambayo ilipaswa ipewe kipaumbele na Runinga ya Serikali badala ya kupitisha ujumbe kwenye screen.

Sitashangaa kesho serikali ikisema wote wanaopakana na makambi ya jeshi wahame mara moja bila hata kutafuta namna ya kuwasaidia..

Anonymous said...

hii ndo jamhuri ya "WADANGANYIKA". Hatujifunzi, hakuna uwajibikaji. Linatokea la kosa, tume inaundwa matokeo hakuna mwenye makosa , hakuna wa kuwajibika!!