Friday, February 18, 2011

Hali Ilivyokuwa Dar Wakati wa Milupuko


Nimepokea picha na habari hizi kwa email:

Wanaoonekana kwenye picha ni watu wakiwa kwenye malori, wengine juu ya Carrier za mabasi aina ya DCM na wengine wakitembea kwa miguu wakiyahama makazi yako kufuatia tangazo la kuwataka wananchi waondoke maeneo hayo.

Kwa sasa simu hazipatikani, ambulance na magari ya msalaba mwekundu ndiyo yanayotoa msaada kwa walio na dharura.

Kwa anaefahamu mtaa wa Kongo DSM au Makoroboi Mwanza, idadi ya wanaotembea kwa miguu ndiyo hali ninayoiona sasa hivi hapa eneo la Tazara hadi Airport.

Tunaomba polisi wa usalama barabarani wasaidie magari yapite kwani kuzuia yanayotoka mjini au yaendayo barabara za kando ya Nyerere Rd, ni kuwanyima haki ambao wanahitaji kwenda kuokolewa.

Inabidi wahusika wajiuzulu mara moja. Its terrible!!!

Naona mabig shot wanapita na mamisafara yao yasiyo na tija kwa wananchi wakienda na kutokea huko Gongo la Mbotto.

No comments: