Saturday, September 03, 2011

Rest In Peace Nick Ashford 1942-2011
Mwimbaji/Mtunzi maarufu Nick Ashford alifariki dunia wiki iliyopita. Alikuwa ana miaka 69. Alikuwa anaumwa kansa ya koo Unawajua Ashford & Simpson kwa nyimbo Solid, in't Nothing Like the Real Thing, Ain't No Mountain High Enough, na Reach Out and Touch.

Nick na mke wake walikuwa pamoja karibu miaka 50. Mapenzi yao ilisifika sana hasa kwa Hollywood ambako watu hawaishi katika ndoa kwa muda mrefu.

Mimi nilibahatika kuwaona mwaka juzi kwenye kituo cha treni Back Bay Boston, Orange Line. Nilivyowaona nikasema doh hao wanugu wanaonekana matajiri kweli! Nikaona watu wengine wanawatazama ndo nikajua ndo Ashford & Simpson.

Mungu ampe mjane wake Valerie, na watoto wao nguvu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.

REST IN ETERNAL PEACE NICK ASHFORD!

No comments: