Sunday, September 11, 2011

Safari Yangu World Trade Center 1991 na Kumbukumbu Zangu za 9/11

Wadau, mwaka 1991 nikiwa Alfred Friendly Press Fellow, nilibahatika kutembelea World Trade Center, New York. Watalii walikuwa wanapenda sana kwenda juu ya WTC kuaangalia view ya New York City. Duh! Hizo Towers ziliangushwa September 11, 2001.

Me on Top of the World Trade Center in August 1991

Me checking out the view of New York City from the top of the World Trade Center

Tanzania Flag on Display in the Lobby of the World Trade Center

My fellow AFPF Fellows (Sameh From Egypt  standing andAbdul on his back from Pakistan)

View of New York City

*****************************************************************

MARUDIO - KUMBUKUBU ZANGU ZA SEPTEMBER, 11, 2011

Nikikumbuka siku ya Septemba 11, mwaka 2001, naweza kusema ni siku nchi ya Marekani ilibadilika. Maana waMarekani hawakutegemea kuwa kitendo cha kigaidi hivyo kingeweza kutokea hapa japo mwaka 1995, mzungu Timothy McVey alilipua jengo la serikali huko Oklahoma.


Siku enyewe kwangu ilikuwa hivi. Nilienda kazini kama kawaida. Ajabu hali ya hewa ilikuwa ni nzuri sana, jua na si joto sana. Wazungu wanasema ilikuwa ni "perfect day". Nilivyofika kazini mume wangu alinipigia simu na kuniambia anaangalia TV na wanaripoti kuwa ndege imegonga World Trade Center. Wala sikutilia manani sana, nilidhani labda ndege ndogo.

Haijapita muda, mume wangu kanipigia simu tena. Alisema kuwa akiwa anangalia taarifa ya ile ndege ya kwanza, aliona ndege nyingine ikigonga jengo la pili huko World Trade Center na sasa wana hofia kuwa ni terrorism!

Sasa mimi niliingia kwenye internet, lakini ilikuwa haifanyi kazi vizuri. Pages hazifunguki. Hatukuwa na TV ofisini. Dada moja ofisini alifungua redio. Mume wangu alinipigia simu nyingine na kusema kuwa ndege imeanguka Pennsyvania na nyingine imeangusha Sears Tower Chicago. (Kweli ilitokea uzushi kuwa Sears Towers imeanguka). Kukaa kidogo kanipigia simu na kusema kuwa ndege imeguka huko Washington D. C. na Pentagon inaugua moto. DUH! nilivyowaambia watu hivyo kuna mzungu moja alisema," Ah, huwezi kuamini kila kitu unachosikia, hata siku moja Pentagon haivamiwi!" Yule dada aliyekuwa anasikiliza aliwaambia watu kuwa nilichosema ni kweli naye alisikia kwenye redio.

Basi wazungu ofisini walianza kuingiwa na kiwewe na kuanza kulia. Wengine walisali, maana ofisi yetu nayo ni ghorofani na tulikuwa financial district kama World Trade Center. Wengine walisem ni mwisho wa dunia! Watu walisema huenda wakavamia Boston. Nilienda dirishani na kutazama nje. DOH! Sijawahi kuona! Wazungu walikuwa wanatembea haraka haraka, wengine walikuwa wanakimbia na suti zao na ma briefcase kuelekea South Station kupanda matreni!

Na mimi nilirudi kwenye deski yangu na kuanza kumpigia simu mdogo wangu ambaye alikuwa anafanya kazi karibu na World Trade Center. Simu zilikuwa haziendi! Wakati huu walianza kutangaza kuwa Tower imeanguka na watu 20,000 wamekufa!Huko nami nasali namtafuta mdogo wangu. Wake wa watu waliosafiri kutoka ofisini nao walianza kupiga simu kujua hali za waume zao maana walitangaza kuwa ndege ziliondoka Boston, Logan Airport na wengine walikuwa wanasafiri siku hiyo. Bahati hakuna aliyekuwa kwenye ndege iliyoangushwa. Ila huyo shujaa Amy Sweeney, aliyekuwa Flight Attendant na ndiye alitoa habari za nani kateka ndege alikuwa ni jirani wa bosi wangu. Kukaa kidogo walitangaza kuwa jengo letu linafungwa na kila mtu aondoke kwenda makwao.

Basi tuliondoka. Njiani kwenda subway ungeona macho ya watu walivyokuwa wanazubaa na kushangaa. Ajabu watu wasiofahamiana walikuwa wanaongea habari hizo mitaani. Na kama unajua maisha Marekani hiyo siyo kawaida. Nikiwa kwenye treni ndo nilisikia kuwa Tower ya pili imeanguka!

Nilianza kumtafuta mdogo wangu wa New York. Ubaya simu landline na cell phones zilikuwa hazifanyi kazi kwa long distance ilikuwa ukipata ni bahati. Wanasema simu zilikuwa overloaded siku hiyo ndo maana hazikufanya kazi. Ajabu nilishindwa kupiga simu New York, na sehemu zingine Marekani, lakini niliweza kupata simu ya Tanzania mara moja. Nilipiga simu nyumbani kwa wazazi wangu na kuongea na baba. Alikuwa na wasiwasi kweli na alisema mama analia hajiwezi na hawezi kuongea, maana aliambiwa kuwa watu laki mbili wamekufa na alijua mdogo wangu anafanya kazi karibu na pale.Doh, ilikuwa kwenye saa kumi na moja jioni tukapigiwa simu na mdogo wangu mwingine. Alisema kuwa aliongea na rafiki wa mdogo wangu wa New York na yuko salama. Mbona tulipumua. Nilipiga simu Tanzania kutoa taarifa. Mbona ilikuwa shangwe kule nyumbani.

Jioni ile niliongea na mdogo wangu, aliniambia kuwa alienda kazini kama kawaida. Alivyotoka kwenye subway aliona makaratasi mengi hewani naoshi, na alishangaa imetokea nini. Aliendelea mpaka ofisini kwake. Kufika huko ofisini, waliwaambia watu waondoke ana walikuwa wanatoa chupa za maji ya kunywa na matunda mlangoni. Anasema watu walikuwa na wasiwasi kweli, huko mbele kuna nini.

Alisema kuwa kulikuwa hakuna usafiri wa treni, basi wala teksi, hivyo ilibidi atembee mpaka Brooklyn alipokuwa anakaa. Na alisema hata hivyo hayuko kwake bali kwa rafiki yake anakaa karibu zaidi na New York City. Pia alisema watu madukani walipandisha bei ya vinywaji na chakula.

Kuna rafiki yangu mwingine wa New York, aliniambia kuwa alikuwa karibu na World Trade Center alijaa mavumbui, hakujua nini inatendeka, lakini alijikuta yuko kwenye ferry kwenda New Jersey. Anasema hajui hata alifikaje kwenye hiyo ferry, lakini alishukuru Mungu kuwa alikuwa hai.

Sasa nikirudi hapa Boston, macho yetu kwenye TV. Walikuwa wanaomba wenye utaalamu wa medical waende New York kusaidia. Misafara ya magari ilienda New York na watu wa kusaidia jitihada za kuokoa watu huko New York.

Kesho yake, Septemba 12, kwenda ofisini ilikuwa kama vile unaenda kumtembelea mtu gerezani! Kuna geti na lazima uonyeshe kitambulisho, wakati jana yake unaingia tu hadi kwenye floor yako, ndo unaingiza kadi kwenye security scanner.

Asante bin Laden, mtu aliyefanana na mwarabu alipata shida kweli. Kusimamishwa na polisi mara kwa mara. Kupanda kwenye ndege ndo ilikuwa usiombe, hiyo security na warabu na wahindi walivyokuwa wananyanyaswa na kupekuliwa. Kuna jirani yangu MPalestina, alikamatwa na uhamiaji siku hiyo ya 9/11 na hatujamwona hadi leo. Watu walijitolea kwa wingi kujinga na majeshi ya Marekani.

Jambo cha kusikitisha, watu walikuwa wanavaa hijab, au nguo za kiislamu na hata wahindi singasinga walikuwa wanapigwa ovyo na wengine walipoteza maisha. Nakumbumuka msingasinga jirani yangu alivua kilemba chake na kuvaa baseball cap kwa muda.

Pia ilikuwa kila sehemu kuna bendera za Marekani, watu wakionyesha uzalendo wao. Na biashara za waarabu na wahindi walijaza hizo bendera na hata kuweka bendera kwenya ma Pizza box.
Cha kusikitisha zaidi ni kuwa kabla ya 9/11 ilikuwa rahisi kuja Marekani na kupata Visa. Sasa hivi ulie tu, ni kama bahati nasibu. Watu wanachunguzwa na inabidi watoe na fingerprints ndo wapte hiyo visa!

Na waarabu waliokuwa wanapendwa kwa pesa zao za mafuta sasa ni maadui! Na nukuu usemi wa kizungu, "HOW THINGS CHANGE!"

Ubaya huyo Rais Bush alienda kuvamia Iraq na vita iko mpaka leo, lakini hiyo ni hadithi nyingine. Juzi kuna Mbunge wa Marekani alisema kuwa, "Bush kuvamia Iraq ni sawa na Marekani kuvamia Mexico baada ya Pearl Harbor kuvamiwa na Wajapani"

4 comments:

Anonymous said...

asante dada kwakutuandikia hii habari kwakweli hiyo siku ilikuwa hatari sana ilikuwa siku mbaya Mungu atunusuru na hayo majanga inatisha kwelikweli

Anonymous said...

dada asante kweli,nikulize swali moja tafadhali,hizo ndege zilikuwa zinatoka wapi?mi naona ninjama za Bush na mayahudi kuinesha duniya kama uislam ni dini hatari,dada naona kuna wazungu wengine hawaamini mpaka ivi kama ni kweli sio?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:55am, ndege mbili zilitoka hapa Boston, moja Newark na nyingine Washington D.C.

Sawa kama unataka kupotoshwa eti ilikuwa njama ya Bush na wayehudi. Unamaana kuwa hao waIslam wenye itikadi kali walinunuliwa na Bush?

Una habari kuwa moja wa wahudumu kwenye ndege iliyotoka hapa Boston alikuwa jirani yaani nyumba wa pili na bosi wangu? Ni yule mama aliyekuwa anatoa habari kuwa mateka ni akina nani na ndege ilikuwa inaelkea wapi.

Robert said...

Dear Chemi,

wonderful images of people on top of the WTC.

Please take a look at MY-WTC.COM

It would be a pleasure hearing from you!

Best Robert from Berlin/Germany