Saturday, September 10, 2011

Meli Imezama Zanzibar - Mamia Wamekufa!


Wadau, kumradhi muda huu nimegundua hii ya meli iliyozama ni feki. Siyo MV Spice Islandder. Picha ya Juu ndo MV Spice Islander. Picha hii ilipigwa 2007.

(Pichani - Meli M.V. Spice Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi  Picha kwa hisani ya mdau  Ahmed Muhamed Ahmed wa Zanzinet)

Meli M.V. Spice Islanders imezama baharini ikitoka Zanzibar kwenda  Pemba. Habari zinasema kuwa meli iilikuwa imejaza kupita kiasi abiria na mizigo! Imezama eneo la Nungwi, pwani ya Zanzibar. 


*********************************************************
STONE TOWN, Tanzania (AP) - An overcrowded ship sank in deep sea off mainland Tanzania on Saturday with about 600 people onboard, and about 370 people are believed missing or dead.

The ferry, M.V. Spice Islanders, was heavily overloaded and some potential passengers had refused to board when it was leaving the mainland port of Dar es Salaam, said survivor Abdullah Saied. It sank in an area with heavy currents in deep sea between mainland Tanzania and Pemba Island at about 1 a.m. Saturday.

About 230 people had been rescued and 40 bodies had been recovered, said Mohamed Abud, the minister for the vice president's office.

Thousands of residents mobbed the docks of Stone Town on Zanzibar, an island near Pemba, waiting for news. One man was screaming that he had lost 25 members of his family, including his sisters, his wife and grandsons. He was too upset to give his name. Many of the crowd were crying or screaming.

Seven bodies have washed up so far, said witness Abdirizak Juma.

Many of those present expressed anger that the ship had been allowed to leave port so overloaded and called on government officials to resign.

The green and hilly island of Pemba is often described as one of the best scuba diving destinations in the world.

3 comments:

Anonymous said...

Nadhani vyombo vingi tayari vimeshaanza kutowa taarifa za ajali ya meli ya Mv. Spice Islander katika safari yake kuelekea kisiwani Pemba.

Inasemekana abiria waliomo ni kadiri ya 600 lakini wengi wana wasiwasi kwamba wanaweza wakazidi ya hapo ukichukulia idadi hiyo ni idadi ya kawaida ya abiria kwa boti ndogondogo za mwendo wa kasi kama Kilimanjaro za Bakhressa.

Mpaka saa nne asubuhi, waliokolewa wanakadiriwa kuwa ni 490 na waliokufa ni takriban 40 lakini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa nambari zionyeshwavo kupitia Zanzibar Broadcasting Cooperation (ZBC) ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la TVZ, idadi inakadiriwa kufikia 120 na bado inaendelea. Tunamuomba Mwenye Enzi Mungu awalaze mahala pema peponi, Aaamin.

Anonymous said...

Taarifa za uhakika zimeshatoka na kweli hii meli imezama ikiwa na abiria 620 sasa hivi nasikia wapo watu waliokuwa wamekaa kwenye mgongo wa meli na tayari wameshaokolewa kinachofanyika sasa hivi ni kuanza kutoa maiti za waliofariki dunia
Hili tukio limeitikisa sana Zanzibar mji umegubikwa na simanzi na vilio kila upande .Watu wengi wako Nungwi kushuhudia kwa macho yao kinachoendelea.
Vyombo vingi vya majini viko maeneo ya ajali na Helicopter ya polisi toka Dar ndio iliyosaidia kutambua sehemi ilipo meli

Taarifa tutaendelea kuwajulisheni kadri tutakavyokuwa tunazipata

Fatma

Anonymous said...

Poleni ndugu zetu kweli nchi yetu sijui niseme uelewa au ni akili nyingi sana au ni ujinga mwingi sana hatujifunzi kutokana na matukio si serikali wala wananchi ni jambo la kusikitisha sana. tumuombe Mungu atujalie hekima ilituweze kukwepa majanga mengine yaliyo ndani ya uwezo wetu si kila wakati tunaema shetani wakati mwingine tunasingizia shetani ni sisi wenyewe.