Saturday, February 04, 2012

Bei ya Bidhaa Yapanda Ghafla Dar!

Kuna mdau ameleta maoni aliyoona leo kuhusu vitu kupanda bei kutokana na bei ya umeme kupanda.

******************************************************


Kwa masikitiko makubwa, ninalazimika kuandika ujumbe huu kufuatia ninayoyaona sokoni leo.

Kwa bahati mbaya, anaeathiriwa na mabadiliko yote haya ni mlaji wa mwisho ambae ni mwananchi.. Kupanda kwa gharama ya umeme, kumeongeza bei za vitu kwa takribani asilimia 25 hadi 40.

Mfano, maji ya Azam (1 lt) yalokuwa yanauzwa kwa Tzs 500 sasa ni Tzs 600. Yale ya (1/2 Lt) yanauzwa Tzs 400 na yale ya (1/4 Lt) yanauzwa Tzs 250. Bei hizi ni kuanzia leo. Maji hayo kwa bei ya jumla yamepanda kwa takriban Tzs 700 kwa kila carton.

Kwa bahati mbaya, makampuni mengine ya ya maji ya kunywa kama Kilimanjaro, Sayona na Maisha nayo yako mbioni kupandisha bei. Bei ya cement na nondo nayo imepanda na viwanda hivyo navyo vinajipanga kupandisha bei ili kufidia gharama ya umeme.


Viwanda vya bia navyo vimepandisha bei jana kwa Tzs 6000 kwa crate kwa bei ya jumla. Bia ya Serengeti haijapanda lakini nayo iko njiani kupanda. Kwa ufupi, mfumko wa bei (Inflation) itafikia 23% hadi 25% mwezi huu kama serekali haitachukua hatua za ziada kupunguza machungu hayo ya umeme.

Kwa ufupi, tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya safu yote ya uongozi wa nchi hii, tangu serekalini hadi kwenye mashirika ya umma, ili kuleta tija na kuwa na maamuzi yasiyo ya kisiasa.

TUFANYE NINI kubadili hali yetu ya maisha kwenye mfumko wa bei unaosababishwa na kupanda kwa bei za mafuta na umeme?

Mdau EK

No comments: