Wednesday, February 22, 2012

Nafasi za Kazi Kongwa Beef

NATIONAL RANCHING COMPANY LIMITED
(KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA LIMITED)
NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO “SALES AGENTS”

“Kongwa Beef” ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na NARCO,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya maboresho ya namna
ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya “Kongwa Beef”. Ili kuhakikisha tunawapatia
wateja wetu huduma zinazozidi matarajio yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za
Wakala Mauzo “Sales Agents” kwa vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii
ni fursa muhimu sana kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga
uzoefu na kufanya kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.
Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za “Kongwa Beef” kutoka kwa
wateja, basi hii ni nafasi yako.

MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA “KONGWA BEEF”
 Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja kwenye
maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
 Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua “Kongwa Beef”.
 Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
 Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef

MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA
 Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha imemfikia
mteja kupitia wasambazaji wetu.
 Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri zaidi ndivyo
utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
 Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto za
kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
 Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi.
 Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
 Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za
biashara,ujasiriamali na masoko.

TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA
Mwombaji:-
 Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
NATIONAL RANCHING COMPANY LIMITED
(KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA LIMITED)
 Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
 Uwezo wa kuongea Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
 Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
 Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa za
Mauzo na Masoko.
 Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
 Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe “CV” yako pamoja
na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe mzazi au
mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
 Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
 Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri na yenye
picha yako.

Maombi yote yatumwe kwa:
Meneja Mkuu,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
Mavuno House, Azikiwe Street,
S.L.P 9113,
Dar es Salaam.
Simu : +255 22 211 0393/211 1956
Barua Pepe: info@narco.co.tz
Tovuti: www.narco.co.tz
Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila tutakapopokea
maombi tutayafanyia kazi mara moja.

*********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********

No comments: