Wednesday, February 29, 2012

Mzee George Mbowe Afariki DuniaMarehemu Mr. George Frederick Mbowe
1935-2012
  Familia ya George Mbowe wa Msasani, Dar es Salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha mpenswa wao, Mzee George Frederick Mbowe, kilichotokea usiku wa kuamkia leo jumatano 29/2/12 nyumbani kwake.

Mipango ya mazishi inafanyika nymbani kwa marehemu Plot. No. 94, Msasani, Old Bagamoyo Road karibu na nyumbani kwa Rais Mstaafu , Ali Hassan Mwinyi.

Misa ya kumuage marehemu itafanyika Ijumaa saa nane mchana katika kanisa la Anglican St. Alban.  Heshima za mwisho zitatolewa pia nyumbani siku ya Ijumaa saa 12 jioni.

Mazishi yatafayika Dodoma siku ya jumapili saa kumi jioni.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA MBINGUNI. AMEN.

***************************

Binafsi, ninatoa pole sana kwa familia ya Mzee Mbowe. Alikuwa rafiki wa familia yetu miaka mingi, alisoma na baba yangu.  Mara nyingi tulienda kwenye shughuli mbalimbali nyumbani kwake na pia alikuja nyumbani kwetu mara nyingi kwenye shughuli.  Mzee Mbowe alikuwa haachi kutabasamu.


Mara la mwisho nilikutana naye kanisani St. Albans mwaka 2009. Alikuwa amepata ugonjwa wa kupooza (stroke) na kuongea ilikuwa shida kwake. Hata hivyo bado aliweza kutabasamu na kuniambia jinsi aliovyofurahi kuniona baada ya ya miaka mingi. 


May Mzee Mbowe Rest in Eternal Peace. Amen.

2 comments:

Anonymous said...

Rest in Peace Mzee Mbowe

Anonymous said...

What an amazing man. What a great loss.
May you rest in eternal peace.