Tuesday, July 16, 2013

Daladala laparamia na kugonga ukuta wa Kanisa la St. Joseph mjini Dar!Kutoka Wavuti.com


Walemavu wa miguu walijikuta wakiangalia mabaki ya baiskeli zao zilizoharibiwa baada ya kunusurika kugongwa na daladala namba T 989 BCN linalofanya safari zake kati ya Mabibo na Kivukoni lililoacha njia na kuparamia ukuta wa mlango wa kuingilia Kanisa la Mtakatifu Yosefu (St. Joseph) jijini Dar es Salaam leo.

Daladala hilo lilipata ajali wakati likijaribu kukwepa gari jingine dogo lililokata kona bila ya kuchukua tahadhari wakati likiingia katika Kanisa hilo.

Gari lingine dogo lenye namba za usajili T 674 BRL lililokuwa limeegeshwa nje ya Kanisa hilo liliharibiwa baada ya kuangukiwa na ukuta.

Picha, Maelezo: Dotto Mwaibale

KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA DA SUBI
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2ZE38gx6S

1 comment:

Anonymous said...

Chemi, hiyo barabara ni one way kwa hiyo suala la gari kukata kona ghafla kuingia kanisani halipo. Huu ni uzembe wa dereva wa daladala.