Sunday, July 28, 2013

Story ya Wazee Kusubiri Kufa

 Na Nape Nnauye

Nimestushwasana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwa kweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikua ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wanawajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wanawajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!
Imenisikitishasana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity

Mh. Nape Nnauye

6 comments:

Anonymous said...

UMEYASEMA HAYO USIKATAE, LAKINI KUMBUKA UZEE NI HAKI YA KILA BINADAMU AMBAYE ATATUNUKIWA KUUFIKIA KWANI KUMBUKA WAZEE HIVI SASA HUISHI LONGER THAN HAO VIJANA.

LAZIMA TUWAHESHIMU NA WAWE NA SAUTI KALI KATIKA MAAMUZI HATA KAMA KUNA KIFO ! BILA WAZEE WEWE MWENYEWE USINGEKUWAPO HAPO ULIPO HIVI SASA INA MAANA MZAZI WAKO HIVI SASA HANA THAMANI?KWA SABABU KISHA JUMLISHWA KWENYE KUNDI LA WAZEE? ANGALIA KIJANA SIASA NI KAZI YA KUTUMIA AKILI KABLA HUJA FUNGUA MDOMO WAKO NA NINI UNACHOKITOA NDIO MAANA UMEFAHAMIKA VINGINE.

MAWAZO YATATOLEWA NA KILA RAIA, MTOTO,KIJANA,MZEE,MWANAMKE, MWANAUME,SHOGA,MSAGAJI NK. WOTE WANA NAFASI KATIKA DUNIA HII. MESSAGE SEND.

Anonymous said...

Sishangai. Wote tunaijua ajenda ya gazeti la Mtanzania.

Anonymous said...

Wewe Nape iko siku na wewe utakuwa mzee, Utapenda kusikia unatukunwa na kijana asiyejua maisha?

Anonymous said...

Nape, Binafsi sikuamini. Na kwa kuwa nina uzoefu na baadhi ya waandishi ambao hukaa chini ya mti na kutunga stori nashawika kuamini mshangao wako. Pole sana

Anonymous said...

Mimi naona amesema vijana wana haki na wajibu zaidi ya kutoa mawazo. Ni kweli hii? Wazee nao si raia wa Tanzania?

Anonymous said...

Chukua hatua Nnape, haiwezekani taarifa iliyokukariri wewe isibebe ujumbe uliokusudia halafu ukaishia kusikitishwa na kukerwa. Hala hala usifuate maagizo ya PM Pinda