Tuesday, July 09, 2013

Ramadhan Karim


RAMADHAN‬ KARIM
Uzuri wa Ramadhani si tambi kwa iliki
     bali ni kusoma Qur-an kwa wingi.
Wala si uji kwa ndizi
bali ni kumuomba MOLA atuhifadhi.
Tena si chapati kwa mchuzi
bali ni kuacha yote ya kipuuzi.
Na wala si juisi kwa sambusa za nyama
bali ni kuomba istighfar kwa Maulana.
Pia wala si daku la wali wa nazi kwa jodari
bali ni tahajudi kwa wingi.

"MOLA ATUWAFIKISHE KUUDIRIKI MWEZI WA
RAMADHANI NA KUPATA FADHILA ZAKE".

2 comments:

Anonymous said...

Inshallah, Da Chemi.

Anonymous said...

Asante sana Da Chemi. Na wewe pia!