Wednesday, July 24, 2013

Pesa Ina Majina MengiPESA INA MAJINA MENGI. Ona;

Kwenye ibada inaitwa Sadaka au Zaka,

Msibani inaitwa Rambirambi,

Shuleni inaitwa Ada au Karo,

Kwenye Vyombo Vya Usafiri inaitwa Nauli,

Ukinunulia Haki inaitwa Rushwa,

Kumdhaminia Mtu Mahakamani inaitwa Dhamana,

Pesa ya uchumba inaitwa POSA,

Pesa ya itolewayo mtu akabidhiwe mke inaitwa MAHARI.

Je PESA inayohongwa kwa mpenzi inaitwaje?

 Jibu tafadhali.

1 comment:

Anonymous said...

Napenda pesa, hela, fedha! Tena mamilioni mfukoni!