Saturday, January 24, 2015

Mungu Akulinde Sospete Muhongo

MUNGU AKULINDE  SOSPETER MUHONGO

Na Happiness Katabazi

LEO  saa tano asubuhi, Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alitangaza rasmi kujiuzuru nafasi hiyo ya uwaziri kwasababu ya zogo la Escrow.

Tangu mwanzo kupitia makala yangu msimamo wangu niliweka wazi Kuwa naunga mkono Utendaji kazi wa Profesa Muhongo na hata Leo hii ninavyoandika makala hii sitabadilisha msimamo wangu Kuwa Kwangu Profesa Muhongo ni Miongoni mwa Mawaziri wa Nishati na Madini ambao nimewashuhudia Kuwa ni mawaziri ambao wameacha alama ya kukumbukwa.

Pia tangu mwanzo nilisema wazi kupitia makala zangu mbalimbali kwa jicho la Sheria Katika zogo la Escrow Hakuna Mashitaka ya wizi Kama baadhi ya watu walivyokuwa wakiwa hukumu Moja kwa Moja watu  waliotajwa kwenye zogo la Escrow Kuwa ni wezi na kwamba Fedha za Escrow zimeibwa.

Hoja yangu ilipingwa  na baadhi ya watu waliokuwa wakisema Fedha za Escrow ni za umma na fedha hizo za Escrow zimeibwa na waliiba ni wezi wanastahili kushitakiwa kwa wizi, ilikuja Kufungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete, Disemba 22 Mwaka Jana, Katika mkutano wake na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na mengine alisema hatukuwa na wizi Katika Fedha za Escrow na Fedha za Escrow siyo mali ya umma.

Pia mapema Mwaka huu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili wafungulia  Kesi ya kupokea Rushwa kutoka kwa Lugemalila baadhi ya maofisa wa serikali ambao waliotajwa kwenye zogo la Escrow.

Tusubiri hatima ya Kesi hizo itapofika Tamati na tusubiri pia ushahidi utakaotolewa na Huyo Lugemalila  je Lugemalila akifika mahakamani atatoa ushahidi wa ni kweli au si kweli aliwapa rushwa? pia tusubiri utetezi wa washitakiwa hao na uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, utakapotolewa.

Profesa Muhongo ametaja baadhi ya Sababu zilizomsukuma kufikia uamuzi huo, Nampongeza kwa uamuzi huo licha amekuchukua wakati Tayari mashankupe na mapashukuna  wameishalipaka matope jina lake Mbele ya Jamii.

Waswahili wanasema penye ukweli, uongo ujitenga. Hivyo ipo siku ukweli wa hili zogo la Escrow utakuja kujulikana nani muhasisi wake?  Kwanini waliliasisi zogo hili?,Muhongo alishiriki kwa kiasi gani Katika jambo Hilo?Ni kweli Katika Utawala wa Muhongo Wizara ya Nishati ilipata Hasara na kwamba Hakuna jambo lolote la maendeleo alilolifanya?

Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa wakati akitoa hotuba yake bungeni wakati ajijuzuru  pamoja na mambo mengi alisema ; ' Tukiruhusu kila mwanasiasa ajijuzuru kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitika Hakuna mwanasiasa atakayebaki salama'.

Kweli sasa mantiki ya ubashiri huo wa maneno ya Mzee  Lowassa yameanza kutimia.

Hongera Muhongo kwa uamuzi huo Kwani utakupa fursa ya kwenda kufanya shughuli nyingine kwa Amani na utulivu kwa watu wenye akili timamu ambao wanamisimamo usiyoyumba na Kamwe hawaamini katika majungu na upashukuna.

Mema uliyoyafanya Katika Wizara ya Nishati na Madini,tutayakumbuka na tutaheshimu mchango wako katika sekta ya nishati na madini.

Utendaji kazi wako kumbe ulikuwa ukiwakera baadhi ya walafi .Na watu wanaofikiri sawa sawa tunajiuliza ni kwanini kila kukicha Mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika serikali ya awamu ya nne wamekuwa wakishambuliwa wazi wazi na mwishoe wamekuwa wakijiuzuru au kuondolewa katika wizara hiyo?

Mbona Wizara Kama Wizara ya Maendeleo ya Jinsia na Watoto hata siku Moja hatushuhuudii wanasiasa uchwara wakikomalia Kuwa mawaziri wake wameshindwa kazi Kwani kila siku ripoti zinaonyesha watoto wadogo ,wanawake wanafanyiwa vitendo Vya kikatiri Kama kubakwa na Kuuwawa?

Ni Wizara ya Nishati na Madini tuu ndiyo inastahili kumulikwa ? .Jibu ni Jepesi hapa ni manyang'au yenye Nguvu za kifedha yalizibiwa mirija ya kufanya biashara zao kwa njia chafu Katika sekta ya Madini na Nishati.

Ikumbukwe Kuwa wale wote ambao mnatumia Hiari na uchafu wa kila aina kuwachafua wenzenu na kuakikisha wenzenu wanatoka madarakani kwaajili ya mashinikizo yenu, ipo siku na Nyie wakati wenu utafika wa kulipwa hapa hapa na Mungu malipo ya hizo hira Zenu na msije kulia na Mtu.

Nchi hii Ilipofika hivi sasa, majungu, fitna,ushirikina, uzandiki Ndio umetawala na umeshika hatamu.Watu wasiyo na hatia na siyo kwenye Nyanja za siasa tu wanaangamia kwa ushenzi huo.

Imekuwa nchi ya watu tunaopenda Ujinga Ujinga na uzushi halafu na mbaya zaidi tabia hizo zinafaywa na wanaume amba wanawake nyumbani eti tunajiaminisha nchi hii itapata maendeleo kwa haraka.

Wito wangu kwa Watanzania wanaishi nchi za nje na kufanya kazi katika taasisi za kimataifa nje ya nchi na wamesoma vizuri ,wasiwe wepesi sana kurudi nchi Kuja kufanyakazi Hasa za kisiasa kwa kisingizio eti serikali imewaomba sana Kuja Tanzania kufanya kazi.

Nawaomba mjifunze kwa yaliyowakuta wenzenu ambao walikuwa wakifanyakazi nje ya nchi akiwemo Profesa Muhongo ambaye alikuwa akifanya kazi nje ya nchi, serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakyaa Kikwete ikamuona wa maana sana, ikamtaka arejee nchini aje alitumikie nchi na kweli alikuja kuitumikia lakini malipo aliyoyapata ndiyo hayo mmeyaona.

Ambayo minayafananisha na tabia zinazofanywaga na waswahili swahili huku mtaani za kumkodishia ngoma ya mdundiko mtu na kuja kumsuta mtu.
Au kumkodishia mapashukuna  kila kukicha wawe wanamchafua jina lake na kweli wamefanikiwa na waliokuwa wanatakiwa wadhibiti Hali hiyo wamekaa kimya.

Mke wangu IGP- Said Mwema na Mkurugenzi wa TAKUKURU ,Dk.Edward Hosea wakati Sakata la Fedha za EPA bado washitakiwa hawajapelekwa Mahakamani na wananchi walikuwa wakishinikiza wapelekwe.

Viongozi Hao ambao ni makachero wazuri tu walikuwataka wananchi wawe na subira na Kusema HIvi " Mafisadi ni watu hatari sana hivyo inatakiwa kwenda nao Polepole".  Ni kweli makachero hao walikuwa walikuwa wakijua wanavyosema na ndicho kilichomkuta Mtani wangu Muhongo.

Hivyo Muhongo muachie Mungu, yeye ndiyo muweza wa yote, endelea kulitumikia taifa Lako kwa uaminifu ila kwa taadhari pia  Kwani Tulipofika sasa watendaji waaminifu na wachapakazi nchi hii HIvi sasa nikama hawatakiwi.

Tusubiri tuletee Waziri wa Nishati na Madini ambaye uenda anaweza Kuwa malaika kutoka mbinguni ambaye Kamwe hataguswa na tuhuma yoyote Kama watangulizi wake Wizara hiyo walivyokabiliwa na tuhuma na kutakuwa kujiuzuru.

Pia tusubiri Huyo Waziri wa Nishati na Madini mpya ambaye atateuliwa  na Rais Kikwete ambaye ataweza kuendeleza Yale yaliyoachwa na Muhongo na alete mipango yake Mipya Katika Kipindi hiki kifupi kilichobakia  kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka 2015. Na tumpe ushirikiano siyo kuanza kumchokona.

Mwisho namtakia kila la kheri Mtani wangu Profesa Muhongo Katika majukumu yake mapya.Hongera kwa uamuzi huo wa kujiuzuru licha kwa wale walikuwa tunafahamu mchango uamuzi huo umekusikitisha ila hatuna jinsi.

Wewe siyo wa kwanza kujiuzuru nafasi hiyo kwa Sababu umeona jina Lako lime nafika. Hata aliyekuwa Waziri wa serikali ya awamu ya Tatu, Dk.  Kitine naye Alifikia uamuzi wa kujiuzuru uwaziri kwa Madai Kuwa alitafuna Fedha za umma kwa kisingizio Kuwa Mkewe alikuwa Amelazwa Canada kwaajili ya matibabu na Katika mahojiano yake na Gazeti la Mtanzania la Jumapili la wiki iliyopita , Dk.Kitine akifanya mahojiano na Gazeti Hilo alilitaja kundi la wanamtandao na  ndiyo walioshiriki kumzushia fitna hiyo na walifanikiwa kumchafua kwasababu walikuwa wakiisoma Rais Benjamin Mkapa alikuwa akimwandaa Kuwa Rais wa Tanzania Mwaka 2005.

Lakini Kamati ya Bunge ya Wizara ya Mambo ya nje ilikuja kumsafisha na kunekana ni kweli Mke wake alikuwa ni mgonjwa na alilazwa huko Canada.

Narudia tena wale wote mabingwa wa kufanya binadamu wenzao kwa Lengo tu la kupata maslahi Fulani ikiwemo biashara, vyeo Mkae mkijua ipo siku Mungu atawaadhibu.

Kumbukeni hawa mnao wafanyakazi ufedhuli nao wana Mungu na Mungu wao wala siyo kipofu wala kiwete anayetembelea Magongo.Ipo siku Mtalipwa Ubaya mnaofanyia  wenzenu.Aminini  hivyo.

Mungu akutangulie Muhongo nenda kafanyekazi na wasomi wenzio achana na hawa wanaume 'wachambue Michele'  ambao wametawaliwa na husuda na fitna na unafki na vichwa vyao wanavitumia kwaajili ya Kufugia nywele badala ya kufikiri.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Januari 24 Mwaka 2015
0716 774494.

No comments: