Saturday, January 24, 2015

Profesa Muhongo Ajiuzulu

Akitangaza kujiunzulu mbele ya waandishi wa habari mapema leo Jumamosi Januari 24, 2015
Kutoka Jamii Forums

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo, ametangaza kujiuzulu Wadhifa wake wa Uwaziri Katika mkutano wake wa waandishi wa habari aliouitisha hii leo. Profesa Muhongo ametangaza hatua hiyo leo asubuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Amesema atabaki na Ubunge nafasi aliyo ipata kwa kuteuliwa na Rais Kikwete.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Prof. Muhongo amezidi kusisitiza kuwa yeye hakuhusika na chochote kile katika sakata hilo lakini baada ya kutafakari sana akagundua kwamba, katika sakata hilo amenyooshewa kidole yeye kama Profesa Muhongo. “Mimi nashangaa leo watu kila kona wananiona mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndio nimechukua mabilioni ya escrow wakati ukweli upo wazi. wakati wizara ya nisharti inaingia kwenye mkataba huo mimi sikuwepo kwenye nafasi ya uwaziri, lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi.

Acha niaachie ngazi nafasi hii ya uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni mtu msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali duniani nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija, lakini leo naonekana mwizi, wakati historia yangu inaonesha mimi ni mtu msafi sina doa na wala sijawai hata kumwibia mtu, lakini watu wananiona mimi mwizi”alisema Profesa Muhongo, na ni kwa sababu hiyo ameamua kujiuzulu kwa kuzitaja sababu mbili kuwa ni:-

-Ana matumaini kuwa kuachia kwake ngazi, mjadala wa ‘escrow’ utakuwa umefikia tamati.
-Anafanya hivyo ili kukiweka safi Chama Cha Mapinduzi ambacho kimekuwa kinanyooshewa kidole.

Amesema kwa namna moja ama nyingine, sakata hilo si tu kuwa limekuwa likikigharimu Chama bali pia baada ya kutafakari aliwasiliana na mkuu wake wa kazi, Rais Jakaya Kikwete na familia yake na watu wake wa karibu kuwataarifu kuwa anajiuzulu.

Amesema akiwa katika nafasi hiyo, aliweza kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka vijana wengi nje kusomea masuala ya gesi, nishati na sayansi kwa ujumla kwani ili Taifa liendelee, linahitaji kuwa na wataalamu katika sekta hiyo muhimu.

Waziri huyo mtaalamu wa miamba, amejiuzulu kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya bunge lililopita, lililoiagiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya viongozi wote na watendaji waliohusika na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow iliyobainisha kiasi cha fedha bilioni 302 kuchotwa BOT zilipokuwa zikihifadhiwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, 2014, Bunge la Tanzania lilitoka na maazimio ya kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri Profesa Sospeter Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, kutokana na sakata la uchotaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT) kwa kutaka mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao. Mbali na hao, yumo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Profesa Muhongo anakuwa ni kigogo wa nne kufuata mkumbo baada ya Waziri Profesa Anna Tibaijuka kufukuzwa nafasi yake na Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kujiuzulu mwenyewe, huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akisimamishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunjwa.

Katika hotuba ya mwisho ya Rais Jakaya Kikwete, siku alipotengua uwaziri wa Profesa Anna Tibaijuka alisema amemeweka kiporo Profesa sospeter Muhongo wakati uchunguzi zaidi wa kashfa hiyo ukifanywa.

===============

Mapema leo hii Waziri Muhongo alikuwa ameitisha mkutano na Waandishi wa habari ==>Prof. Muhongo aita waandishi wa habari leo

8 comments:

Anonymous said...

I like this statement by Muhongo:

"I did not do anything wrong and I did not steal any money. My record speaks for itself, I am incorruptible."

He says that he's resigning, not because he's guilty of anything, but because he wants this issue to end.

He's sacrificing himself in order for the nation to get on with national development !!! Kajitolea mhanga !!!
That is a classy thing to do.

P.S.
The man has a good clean-cut face and is very well-dressed.
That's a good thing.

Anonymous said...

Wandugu....siku mkiingia kwenye siasa mtajua....huyu jamaa kaisadia sana wizara hii...mgawo wa umeme umekwisha.. hujuma zote za wafanyabiashara alidhibiti...umeme vijijin kajitahid......hebu jiulizen akina ngereja wamepata wapi mabilioni wanayotembea nayo kwenye mabegi?.....Binafsi, naridhika na uwajibikaji wa Muhongo kisiasa lkn naamini atahitajika tena muda ukifika.

Anonymous said...

OK Badala ya kufukuzwa na asipate mafao, sasa gharama nyingine inakuja ya kumlipa mafao yake yote na kumuenzi.

Hapa ndipo udhaifu wa serikali yetu. Sasa inatugharimu woooooote kumlipa kwa aliyofanya.

Akili nywele

John P said...

PROF: SOSPETER MUHONGO SHUJAA WANGU SERIKALI YA AWAMU YA NNE

Kama mtanzania wa kawaida nimesikitishwa na taarifa za kujiuzuru kwa Prof. Sospeter Muhongo waziri wa nishati na madini ni wazi kwamba maamuzi haya yamekuja kutokana na shinikizo la watu wanaolazimisha kusikia wanachotaka kusikia na kuukataa uhalisia. Huu ni ushindi kwa baadhi ya mabwanyenye wanaotaka kunufaika na gas kwa kigezo cha uzawa ilhali hawana sifa na uwezo wa kuwekeza, watu ambao wanamaslahi yao binafsi ila wakatumia rasilimali zao kuuaminisha umma kuwa wanapambana kwa maslahi ya Taifa.

Ni huzuni kubwa, itachukua miaka mingi sana kwa Wizara hii kupata waziri thabiti kama Prof. Muhongo, kitendo hiki kinaonesha wazi kwamba ukiwa na msimamo wa kupambana na mabepari huna nafasi katika kuiongoza Tanzania. Wasomi wanaipenda nchi yao ila wanakatishwa tamaa kwani siasa za Tanzania hazitoi fursa kwa wasomi kuzitumia taaluma zao objectively. Mabepari wanapambana kuhakikisha wazalendo wanafutika katika mfumo wa serikali.

Ili uonekane mwanasiasa bora Tanzania Muhitimu wa kidato cha nne anataka kusikia kwamba anao uwezo wa kufundisha chuo kikuu kwasababu ni mzawa. Watanzania wamezowea viongozi wanaowadanganya na kuwapa moyo hata kwenye vitu ambavyo haviwezekani.

NITAMKUMBUKA MUHONGO KWA:

1. Uwazi wake kwa Watanzania bila kujali mihemko ya walioukataa ukweli
2. Kusimamia kazi ya kusambaza umeme vijijini kwa kasi ya ajabu
3. Kudhibiti tatizo la mgao wa umeme
4. Uwezeshaji kwa wachimbaji wadogo
5. Kuweka mbele maslahi ya Taifa dhidi ya maslahi binafsi
6. Ujasiri wa kukata mirija ya wanyonyaji wizarani bila kujali utajiri wao.
7. Kusimamia kigezo cha kuwa na mtaji kwenye mradi wa gas
8. Ni waziri ambaye bajeti zake zilikuwa clear zimejaa miradi ya msingi na si porojo za kisiasa

Kutokuwa tayari kuwadanganya watanzania na kuwapa matumaini kwa vitu ambavyo haviwezekani, kukata mirija ya mapepari uchwara wa ndani, kuwana msimamo kwa anayoyaamini haya ndiyo yaliyomuondoa Muhongo. Watanzania tumekubali kuwapa ushindi ni watu wabadhirifu waliomuona Prof. Muhongo ni kikwazo kwao kwasababu walinyimwa vitalu vya familia kwa maslahi ya umma.

Any way Hongera kwa kazi nzuri, hongera kwa msimamo kwa tunaotambua uwezo wako tumesikitishwa na jambo hili. Hakika ulikuwa waziri wa kutiliwa mfano wewe ni shujaa uliyesimamia na kuitendea haki taaluma yako na kukataa kuburuzwa na wababaishaji.

Kwa hali hii tusitegemee wasomi wengine wa Tanzania ambao wanafanya kazi kwenye mashirika makubwa duniani kukubali kuziacha nafasi zao kwa kigezo cha uzalendo wa kuja kuisaidia nchi yao ilhali nchi inaendeshwa kutokana na mihemko na mfumo haupo tayari kuona wala kusikia uhalisia wa mambo.

--

Anonymous said...

Katika watu waliojiuzuru kiroho ngumu na kikatili ni huyu re=professor ...mie kujiuzulu kwake nimefananisha na jinsi paka alivyo mgumu kufa kwa kipigo cha mwanadamu " mpaka tulikuwa tunasema kuwa paka na roho saba" na kwa mtizamo wangu mie niliona mr. tumbiri- weremaa ndo angekuwa wa mwisho kung'oka ukizingatia sura yake na undava ndava wake aliokuwa akifanya kuzeveza watu kumbe hamna kitu ni mweupe tu.
hakika hakuna marefu yasiyo na ncha . sasa hii ndo kama ya Proffesor muhongo , ila namkaribisha hapa JF tuungane na wadau wa jukwaani hapa kuendelea kusaka na kukamata majizi mengine.

Last edited by Kim-Jong-Un; Today at 15:09.

Teddy said...

Kwanini kajiuzulu kwani kaiba nini?

Anonymous said...

Nchi haijatikisika au ndiyo tunasubiri mtikisiko?

Anonymous said...

Huyu aliachwa kiporo na mamlaka ya uteuzi. Yalafu sasa amejiuzulu. Huku siyo kumdhalilisha rais kweli? Yunajuaje kama angemsamehe. Alitakiwa asubiri awajibishwe kama Tiba na Maswi. Kwa suala la kiporo sasa linakuwaje?