Saturday, January 24, 2015

Punguza Hasira!

Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguoza kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.
Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.
Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”
Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!
Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.
Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu”
“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.
Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.
Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:
“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”

HEKIMA:

1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI
KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.


2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILAYA KUJALI HALI ULIYONAYO.

No comments: