Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts
Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts

Wednesday, November 20, 2013

Tamko kutoka kwa Mh.Zitto Kabwe kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”

 
Mh. Zitto Kabwe


NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema” ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.
Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.
Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.
Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.
Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.
Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.
Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.
Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.
Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.
Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.
Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.
Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.
Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.
Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah

Andrea Cortes Makes Demand to Chadema - Reipoti ya Siri Juu Juu ya Zitto Kabwe

Dear Hon. Dr. Slaa,

Dear Hon. Mbowe,

Dear Hon. Mnyika,


With great disappointment I got to learn that members of your party are spreading lies about my person.
A report with the title "RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE" of November 4th, which indicates that it is by CHADEMA headquarters *Nyaraka hii imechomolewa kwa siri toka Chadema makao makuu*, was first published in parts in the Internet platform "Jamii Forum" on the weekend of the 26th of October 2013.
 After bringing my complaint towards the owner of Jamii Forum the threads got deleted.

On the morning of the 6th of November 2013 the address of a created blog with the report was publically circulated by Mr. Yericko Nyerere via Twitter. The blog address http://halihalisi255.wordpress.com/2...a-zitto-kabwe/ only contained the above mentioned report.

 The report mentions me as a person to be involved in corrupt activities with your Deputy Secretary General Hon. Zitto Kabwe. It has indicated my private telephone number and the place where I am working.
 This defamation of my person is not acceptable.

I have reacted on the 6th of November by mentioning several facts to refute the report. Please find these tweets in the attachment. The tweets were mentioned towards Mr. Yericko Nyerere, who pretends to be a member of your party, to Hon. Kabwe and to Hon. Mnyika.

After my reaction the report was deleted in the evening of the 6th of November from the blog.
The deletion thus does not resolve the problem that a report which indicates to be from your party has tried to slander my name in the public. Moreover bringing my workplace into the game and therefore putting my organization in a wrong light and even bringing my appointment with this organization in danger.

I therefore request you to take necessary actions to recover my name in the Tanzanian public.
CHADEMA has to dismiss this report as not being written by the party but by an individual who intends to defaming one of your party leaders.
 If CHADEMA will not dismiss the parts of the report which mention my person then I kindly ask you to bring forward the proofs against me that I can accordingly refute them with the necessary actions.

I am awaiting a statement and clear position by your party to recover my name and to take necessary actions to take the authors of this report to court.

My organization and lawyer are informed about the slander campaign in regard to my person. Accordingly legal actions will be taken if CHADEMA will not refute the report officially and bring justice to the people affected from it.

 With warm regards
 Andrea Cordes

Wednesday, May 08, 2013

"Taifa Lina Nyufa" - Mh. Mbunge Zitto Kabwe



TAIFA LINA NYUFA

Na Mh. Mbunge Zitto Kabwe

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013


Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:

“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavior and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanians”

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki “hate speeches”. Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

Wednesday, March 27, 2013

Siri ya Kuuawa Zitto - Sio Kweli

PRESS RELEASE: 'SIRI YA KUUAWA ZITTO'-SIO KWELI




SIRI YA KUUWAWA ZITTO

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

--

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013

Thursday, January 03, 2013

Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji

Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi

Picha Hisani ya: Mtwara Kumekucha Blog by Baraka Mfunguo

'Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Dar inachangia 90% ya ufisadi. Uti wa mgongo wa ufisadi nchini'


Na Mh. Zitto Kabwe
Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi bora ya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini kuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwa kuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi. Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanya mkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wake alilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikali kuweweseka.

Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk, Serikali ilitaka kuonyesha umma kuwa watu wa Mtwara hawana shukurani. Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwa na Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu wa Mtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyo wao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani. Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi ya Watanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.

Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu wa Mtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi wa Taifa kupitia zao la Korosho. Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya dola za Kimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali ya Uchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010). Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingizia Taifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hili liliingiza dola 130 milioni wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu. Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za kigeni (sawa ni shilingi trilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo miaka 50 nyuma kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania. Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenye uchumi wa nchi yetu kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kauli rasmi ya Serikali haijataja Korosho kabisa? Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa Serikali wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke dhidi ya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?

Pili, Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katika ulinzi wa Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa nyuma kimaendeleo ni juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika. Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuwa Nachingwea. Kambi ya Frelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa 17 tu kutoka mjini Nachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Msumbiji. Rais Samora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza waliendesha mapambano kutoka kusini mwa Tanzania. Makaburu wa Afrika Kusini na Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es Salaam inaendelea kwa kila aina ya maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwara ilikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine waishi wa amani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa mikoa hii? Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia kuzalisha umeme wa kufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya Serikali kusahau kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara katika kulinda uhuru wa Taifa letu?

Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Dar ndio inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo. Ni aibu Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu cha kukusanyia mapato ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenye kuzalisha kodi unafanyika nje ya Dar es Salaam. Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam lakini uzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. Serikali itoe orodha ya walipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayo unafanyika wapi. Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar es Salaam inakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi. Basi na tuseme Dar es Salaam inachangia asilimia 90 ya ufisadi wote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi zinafanyika Dar es Salaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.

Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni kielelezo tosha kwamba watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na longolongo za Serikali. Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa Serikali kuhusu utajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu kutokuwa na laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara kudai maendeleo. Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni. Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara wahaini, wapuuzi na watu hatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani imekusanywa kutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14. Mpaka mwaka 2008, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani, kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa dola 11 milioni na kodi nyingine dola 16 milioni. Serikali itwambie ilipofika Disemba 2012 kodi kiasi imekusanywa kutoka kampuni hii?

Pia watu wa Mtwara na Lindi wameona historia ya bomba la Songosongo. Hata kodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (0.3%) ilikuwa inalipwa Halmashauri ya Manispaa Ilala na kampuni ya Pan Africa Energy. Ilichukua juhudi za mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu kuingilia kati ndio kodi ikaanza kulipwa Kilwa ambapo uzalishaji unafanyika. Watu wa Mtwara ni werevu, wanajua wafanyalo. Wanataka utajiri wa nchi unufaishe nchi kwa kuanzia kule utajiri ulipo. Kuna dhambi gani?

Uwajibikaji katika uvunaji wa Rasilimali ya Gesi ndio chanzo cha maandamano ya watu wa Mtwara. Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa kwamba ndio wamechochea maandamano haya. Haya ni maandamno ya wananchi wakitaka Serikali yao iwajibike kwao. Serikali ithubutu kufanya ubabe wa kujenga bomba la gesi bila ridhaa ya Wananchi wa Lindi na Mtwara. Wananchi wanapohitaji uwajibikaji ni wajibu wa Serikali kuwajibika kwao ni sio kuwaita wahaini, wachochezi, watu hatari, wapuuzi. Watu wa Mtwara wamechangia maendeleo ya Taifa letu kwa jasho na damu. Serikali ina wajibu wa kuwasikiliza, kuwaelimisha na kupata mwafaka. Kauli ya Serikali imewatukana watu wa Mtwara na Lindi. Hawatakubali kudhalilishwa. Hawatakubali historia yao kufutwa. Hawatakubali waendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Serikali ifikirie tena.

Saturday, December 08, 2012

Mh. Zitto Kabwe Ziarani Ulaya

PRESS RELEASE

Ndugu Zitto ziarani Ulaya
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo “Economic Conference: Commitment to Africa Initiative” utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.

Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.

Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.

Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.

Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.

Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini
8 Desemba 2012, Dar es Salaam 

Tuesday, November 27, 2012

Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

PRESS RELEASE: Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

by zittokabwe
Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini
Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.
2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.
 Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012

Tuesday, November 20, 2012

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta

by Mh. Zitto Kabwe


Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.
Nimeona ni vema nitoe kauli yangu rasmi kuhusu suala hili. Lengo ni kuweka rekodi sawa juu ya Azimio la Bunge na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza Azimio na sio kutoa kauli tata za kukata tamaa.

Moja, Suala hili japo sio jipya lakini limeandikwa kama ni jambo jipya. Suala la Serikali ya Uswisi kutaka majina lilisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akichangia hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni na pia wakati akileta maombi yake ya kuiondoa hoja ambayo yalikataliwa na Bunge. Kama sio sababu mpya ni kwanini imeibuka upya na kwa kasi? Ni wazi Serikali inajihami kwa kuona kuwa itashindwa kutekeleza azimio la Bunge. Watanzania wasikubali propaganda hii ya Serikali. Bunge limeagiza Serikali kufanya uchunguzi kwa kutumia njia za kiserikali au wachunguzi binafsi wa kimataifa. Kwa nini Serikali inaanza kubwabwaja ilhali wala haijaanza kazi hiyo? Serikali inajaribu kuficha nini? Kwa nini baada ya wiki iliyopita Benki Kuu kufanya uchunguzi kwenye Mabenki ya Biashara jijini Dar es Salaam na namna fedha zimekuwa zikipelekwa nje (international transfers), leo Serikali inakuja na kauli za kukakata tamaa? Kunani?

Pili, Watanzania wajue kwamba Taifa la Swiss limejengwa na linajengwa kwa fedha hizi za wizi ambazo watu mbalimbali duniani wanaiba au kukwepa kodi kwenye nchi zao na kuzificha huko. Serikali ya Swiss hata siku moja haiwezi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika suala kama hili. Ndio maana Azimio la Bunge linataka wachunguzi binafsi ambao hawatahitaji ushirikiano wa Serikali ya Swiss. Nawakumbusha kwamba mwaka 1997 mara baada ya Joseph Desire Mobutu kuangushwa na Rais Joseph Kabila kule Kongo - Kinshasa, Serikali ya Swiss iliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuonyesha ushahidi kuwa hela hizo za Mobutu zilikuwa zimepatikana kwa njia haramu! Waswiss walitaka Kabila awakakikishie kuwa fedha zile zaidi ya dola bilioni nane za Kimarekani Mobutu hakuzipata kihalali ndio waweze kuzirejesha. Zaire ilikadiriwa kuwa na zaidi ya dola za Kimarekani bilioni thelathini katika Mabenki ya nje ya nchi hiyo. Majibu ya aina aina hii ni majibu ‘standard’ ambayo kila nchi inapewa. Hata Marekani ilipokuwa inafuatilia wakwepa kodi wao walijibiwa hivi hivi. Hatimaye Serikali ya Marekani ikaamua kununua taarifa hizo na kuwakamata wakwepaji kodi wao walioficha fedha Uswisi. Hao ndio Waswiss ambao Serikali ya Tanzania inashabikia majibu yao. Bila Aibu Mawaziri wetu wanayanukuu majibu ya Waswiss kama kasuku. Tunasahau historia haraka sana. Tunakuwa kama mazezeta.

Tusiwe Taifa la mazezeta. Mabwege na mazezeta huimba kila wanachoambiwa kuimba. Sasa Serikali ya Tanzania imekuwa msemaji wa Serikali ya Swiss badala ya kuchunguza utoroshaji wa fedha haramu na kisha kutoa taarifa Bungeni. Naitaka Serikali ianze uchunguzi mara moja kama namna ilivyoelekezwa na Bunge. Suala hili sio suala la kisiasa, sasa ni Azimio la Bunge ambalo linahitaji kutekelezwa kikamilifu. Suala hili sio suala la Zitto Kabwe tena, ni suala la Bunge, ni suala la Wananchi. Wananchi hawataki uzezeta wa watu waliopewa dhamana ya kutekeleza Azimio lao. Kama hawawezi wapishe watu wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya Watanzania kwa kuchukua hatua stahili za kuchunguza utoroshaji mkubwa wa fedha za kigeni, ukwepaji mkubwa wa kodi na ufisadi uliopelekea Watanzania kuficha mabilioni kwenye mabenki nje ya Tanzania. Hatutakaa kimya mpaka tuone mwisho kamilifu wa suala hili. Utekelezaji wa Azimio la Bunge itakuwa ni salamu tosha mafisadi na watoroshaji wa fedha haramu kwamba hawana pa kujificha na Tanzania sio Taifa la kuchezeachezea. Lazima tushinde vita hii. Anayeona hawezi kutuongoza kuishinda atupishe mapema. Hatupaswi kuwa Taifa la Mazezeta. Watanzania sio mabwege tena, Mwakyembe alipata kusema.


Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Kigoma Kaskazini.

Sunday, September 11, 2011

Taifa Msibani, Umoja Wetu na Utu Wetu Shakani

Mh. Zitto Kabwe
Ndugu zangu wanawavuti salam kwenu, naomba mnifikishie ujumbe huu kwa watanzania. Shukrani zangu za dhati.

*******************************************
(Nimeandika makala haya nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible -Zitto Zitto and not Zitto a politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba.

Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii. Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili. 'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki.

Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa. Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni. Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa. Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza. Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu. Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria. Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.

Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe

--

Kabwe Z. Zitto,MP- Kigoma North, Tanzania.
Chairman Parliamentary Public Investments Accounts Committee (POAC),
Deputy Secretary General CHADEMA and Deputy Leader of the Opposition,
Shadow Minister of Finance
Mobile: +255756809535
Blog: http://www.zittokabwe.com/

Monday, July 14, 2008

Mh. Zitto Kabwe hajambo sasa.

Picha kwa hisani ya http://bongopicha.blogspot.com/

Wadau, kuna habari njema. Mh. Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini - Chadema) hajambo sasa na ametoka hospitalini siku ya Alhamisi wiki iliyopita.
*************************************************
Zitto atoka hospitali

Thursday, July 10, 2008

Mbunge Machachari nchini Zitto Zuberi Kabwe (Kulia) akiwa na ndugu yake mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa siku mbili.Mh Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo.


Wednesday, May 21, 2008

Habari zaidi kuhusu Kifo cha Balali

Hayati Dk. Daudi Balali (picha kutoka Michuzi Blog)

Written by KLHN/Tanzania Daima

Wednesday, 21 May 2008

KLH News imeweza kuthibitisha kwa uhakika kuwa misa ya kumuombea Marehemu Balali inatarajiwa kufanyika saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Stephen Washington DC. Kutoa heshima za mwisho kutafanyika katika kanisa hilo hilo na itakuwa si kwa hadhara nzima.

Mwili wake unatarajiwa kulazwa kaburini kwenye makaburi ya "Gate of Heaven" huko hukoJamaa wa karibu wa Ballali walioko Dar es Salaam na Washington walilithibitishia Tanzania Daima kuhusu kutokea kwa msiba huo.

“Ni kweli amefariki nyumbani kwake Ijumaa usiku. Na sasa hivi tuko katika maandalizi ya kwenda funeral home (taasisi ya kuandaa shughuli zote za mazishi) kwa ajili ya kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msiba,” alisema ndugu wa karibu wa Ballali kutoka Washington.

Habari zaidi zinaeleza kwamba, tayari familia ya gavana huyo wa zamani wa BoT imeshaitaarifu serikali kuhusu kutokea kwa msiba huo na kwamba taarifa rasmi kuhusu kifo hicho zitatolewa leo hii.Ndugu mwingine wa karibu wa Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima majira ya saa 4:00 usiku jana alisema mazishi ya gavana huyo wa zamani wa BoT yanatarajiwa kufanyika Ijumaa hii huko huko Marekani.

Mmoja wa wanasiasa aliye karibu na familia ya Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima jana alithibitisha pia kupokea taarifa za kifo cha Ballali kutoka kwa mkewe, Anna Muganda. Ndugu mmoja wa Ballali alipoulizwa na Tanzania Daima sababu za kushindwa kutangazwa kwa taarifa za kifo hicho mapema alisema walilazimika kufanya hivyo ili wapate fursa ya kuwasiliana na serikali kwanza na kisha ndugu, jamaa na marafiki wa familia yao kabla ya habari hizo kusambazwa.

Badhi ya jamaa za Ballali waliozungumza na Tanzania Daima walisema kulikuwa na wasiwasi kwamba kifo cha gavana huyo wa zamani wa BoT kikawa kikawa si cha kawaida.“Kuna wasiwasi kwamba huenda alilishwa sumu wakati akiwa nchini mwaka jana na hili limekuwa likizungumzwa sana ndani ya familia,” alisema mmoja wa jamaa za karibu wa Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima jana.

Taarifa za kuwapo kwa wasiwasi wa Ballali kulishwa sumu zilipata kusikika mwaka jana na wakati fulani ilielezwa kwamba alipelekwa Marekani kwa matibabu kutokana na sababu hizo.

Habari za kifo hicho cha Ballali ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Jakaya Kikwete Januari mwaka huu zimekuja siku chache tu baada ya serikali kupitia Ofisi ya Rais Ikulu kutoa tamko la kutangaza kwamba ilikuwa haimtafuti gavana huyo wa zamani wa BoT.

Tamko hilo la serikali lilitolewa mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu.Rweyemamu alisema kuwa serikali ina mkono mrefu na iwapo itafikia hatua ya kumtafuta gavana huyo wa zamani wa BoT ili aje atoe maelezo yake kuhusu wizi wa zaidi ya shilingi bilioni 133 uliogundulika katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) haitashindwa kamwe kumfikia alipo.

Alisema kutokuwepo nchini kwa Ballai, au kutojulikana alipo, si jambo linaloisumbua serikali kwa sasa kwa sababu hivi sasa yeye ni raia wa kawaida, hivyo anao uhuru wa kuishi popote anapopenda.“Serikali haimtafuti Ballali (kwa sasa), lakini ikiamua kufanya hivyo haitashindwa.

Kwanza ni private citizen (raia huru) siyo mwajiriwa wa serikali tena,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa, mkono wa serikali ni mrefu hautashindwa kumpata Ballali iwapo itamhitaji. kifafanua zaidi, alisema baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wake, serikali iliunda timu ya kuwachunguza watuhumiwa wa EPA, kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarudi na kuwachukulia hatua waliohusika, akiwemo Ballali.

Alisema: “Ninachofahamu ni kwamba, timu iliyopewa kazi kuhusu ubadhirifu wa EPA inaendelea na kazi yake na tunaona jinsi fedha zinavyorudishwa.”Mkurugenzi huyo pia alikiri kwamba serikali haifahamu hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali, licha ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kukaririwa akisema alimtafuta Ballali bila mafanikio alipokuwa jijini Washington, Marekani.

“Kwa kweli sifahamu hasa Ballali alikuwa akitibiwa katika hospitali gani, lakini najua alikuwa nchini Marekani katika Jimbo la Boston, ila hospitali kwa kweli siijui.“Lakini huyu ni mtu huru hivyo anaweza kuishi popote… huyu ana nyumba yake nchini Marekani… yupo huko anaishi na familia yake,” alisisitiza Rweymamu katika ufafanuzi wake.

Wiki iliyopita, ikiwa ni siku chache tu baada ya taarifa hiyo ya Ikulu, vyombo kadhaa vya habari viliandika habari zilizokuwa zikieleza kuwa makachero kutoka hapa nchini, walikuwa wamekwenda nchini Marekani katika miji ya Boston na Washington kufuatilia nyendo na maisha ya gavana huyo wa zamani.

Kwa mujibu wa habari hizo, ambazo zilikariri taarifa za ndani kutoka serikalini, makachero hao walikuwa wamekwenda huko ili kujua mahali anakoishi ili wakati wa kumhitaji utakapofika iwe rahisi kumpata. Ballali aliondoka nchini, Agosti mwaka jana kwenda Marekani kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa matibabu, na tangu wakati huo taarifa zake zilikuwa ni zenye utata mkubwa.

Mara ya mwisho kwa Ballali kuonekana hadharani ilikuwa ni Julai 12 mwaka jana alipozungumza na wanahabari na akasema alikuwa hatarajii kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu.

Katika mkutano huo, Ballali alisema madai ya ubadhilifu yanayotolewa dhidi yake ni uzushi na uongo mtupu.Huku akionekana kujiamini alisema; “Niko Comfortable, moyo wangu mweupe, ari yangu ya kazi iko juu kwani tuhuma hizo ni uongo na uzushi mtupu na siwezi kujiuzulu kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

“Tuhuma zote dhidi yangu ni za uongo mtupu. Kwanza sijui zimetoka wapi, nani mtunzi na kwanini amefanya hivyo. Hilo tunawaachia wanaofanya uchunguzi na naamini siku moja atajulikana na ukweli utajulikana, lakini mimi siwezi kujiuzulu kwa mambo ya uzushi,” alisisitiza.

Kashfa ya BoT kupitia mtandao wa Internet, uliibuliwa mara ya kwanza Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA).Akichangia maoni ya kambi ya upinzani wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha, Dk. Slaa alisema kambi ya upinzani imefarijika baada ya Waziri wa Fedha kukiri kufahamu taarifa aliyoitoa Bungeni kuhusu ubadhirifu mkubwa ndani ya BOT unaomgusa Ballali, pamoja na wafanya biashara wengine wakubwa akiwemo Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya (CCM), kupitia kampuni anayoimiliki.

Dk. Slaa alisema Dk. Mzindakaya alichukua mkopo kwa shughuli za kampuni yake ya SAAFI wa sh 6.217 bilioni, uliogawanyika kama ifuatavyo. Alisema aliomba ‘Overdraft facility ya 450 millioni zitakazolipwa kwa miaka 5; mkopo wa shs 2.8 bilioni zitakazolipwa katika miaka mitano; na Dola za Marekani 2.528. Jumla yote ni Bilioni 6.217.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, fedha zote zilikopwa Benki ya Standard Charter na Benki Kuu ilitoa (Guarantee) mdhamana wa asilimia 100. Mwaka huu wa 2007 Benki kuu kutokana na Mdhamana huo tayari imelipa kiasi cha sh 8.1 Billion kwa niaba ya Mzindakaya na fedha hizo pamoja na riba zinakisiwa kufikia 9.7 billioni hadi sasa (Hati ref. CIBD-14662 ya tarehe 24 May, 2007, na mkopo kutolewa 2005.

Kutokana na tuhuma hizo, Meghji wakati akifanya majumuisho ya hoja yake, alisema Serikali imeagiza kuanza kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje zinazoikabili Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Alikiri serikali kupata taarifa za kuwapo kwa vitendo vya rushwa na nyingine za matumizi mabaya ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Waziri Meghji alisema, tayari alikuwa ameshamwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali, kuanza uchunguzi kuhusu tuhuma hizo.Meghji alisema, serikali ilikuwa ikitarajia kukamilisha kazi hiyo na taarifa kamili ya uchunguzi huo kutangazwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Mbali ya BoT kutuhumiwa kutumia fedha nyingi kuliko inavyostahili katika ujenzi wa majengo yake mapya ya ‘minara miwili pacha’ (Twin Towers), kiasi cha Dola za Marekani milioni 30.8 sawa na shilingi bilioni 40 kinatuhumiwa kufujwa katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje.

Taarifa zinaonyesha kuwa, wakopeshaji wa kimataifa kutoka nchi 12 waliingia mkataba wa kusimamia akaunti hiyo na kampuni ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la Kagoda Agriculture Ltd kati ya Septemba na Novermba mwaka jana.Uchunguzi wa awali wa wakaguzi wa nje wa mahesabu ya akaunti hiyo unaonyesha kuwapo kwa mazingira yenye utata mkubwa unaozingira makubaliano kati ya wakopeshaji na kampuni hiyo iliyolipwa dola milioni 30.8.

Akichangia hotuba ya Waziri Mkuu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) alihoji kwa nini Serikali ilikalia kimya suala la kashfa ya BoT mara baada ya habari za kashfa kutangazwa kupitia mtandao wa internet tangu Novemba 2006 na kuonya kuwa hali hiyo inaathali kubwa kiuchumi iwapo kashfa kama hizi zinaachwa bila ya ufuatiliaji wa serikali.

Taarifa za awali za uchunguzi huo zinaonyesha kuwa, BoT ilifikia hatua ya kuipa kampuni hiyo fedha zote hizo ikidai kuingia mkataba na wakopeshaji hao katika mazingira ambayo nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa na hitilafu nyingi.Miongoni mwa hitilafu zilizobainishwa katika uchunguzi wa awali ni, kukosekana kwa karatasi rasmi zenye majina ya makampuni hayo ya kimataifa.

Thursday, October 25, 2007

Mheshimiwa Salome Mbatia afariki dunia katika ajali ya gari





Picha za ajali kwa hisani ya Mheshimiwa Zitto Kabwe

Picha ya Mh. Salome Mbatia kwa hisani ya Food For Thought blog:

Nimepokea habari za kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendelo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Salome Joseph Mbatia (55) kwa huzuni mno. Dada Salome alifariki jana jioni huko Kibena mkoani Iringa kwa ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso. Madereva wote wawili pia walipoteza maisha.

Dada Salome alikuwa Iringa, kwenye ziara maalum ya kuelimisha akina mama juu ya mila na desturi mbovu zinazochangia vifo vya akina mama na watoto.

Pamoja na majonzi niliyonayo kwa kweli nimekasirika mno. Hayo magari yalikuwa yanaenda mwendo gani? Je, dereva wa gari alikuwa amekunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya. Najua Tanzania kuna tabia, oh kafa hatarudi hata ukifanyeje lakini....

Naomba wana usalama barabarani na pia serikali wachunguze ajali hii!
Akina mama wote wa Tanzania tumepata hasara na kifo cha Dada Salome. Mungu awape familia yake hasa watoto wake na mume wake nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Mungu ailaze roho yake mahali pema mbinguni. AMEN.
******************************************************************************
Ajali ya Mhe. Mbatia Sumaye, Zitto chupuchupu
2007-10-25 Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredric Sumaye, Mbunge Machachari wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. David Mathayo ni miongoni mwa watu walioponea chupuchupu kupatwa na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Marehemu Salome Joseph Mbatia.
Bw. Sumaye, Zitto na Mathayo walikuwa kwenye magari tofauti wakiongozana katika barabara moja na gari la Mhe. Mbatia lililopata ajali, bila wao kufahamiana. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema lori aina ya Fuso liligongana uso kwa uso na gari la Mhe. Mbatia, ndilo lililopoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.
Kwa vile magari yaliyokuwa yamewabeba waheshimiwa hao yalikuwa yakiongozana, basi kama lori hilo lisingegonga gari la Mheshimiwa Mbatia huwenda lingeyavaa magari ya waheshimiwa wengine. Akizungumza na Alasiri kwa njia ya Simu leo asubuhi, Mheshiwa Zitto amesema gari lililokuwa limembeba marehemu Salome Mbatia lilikuwa mbele yake wakiongozana barabarani, lakini hakujua kuwa aliyekuwamo alikuwa ni Naibu Waziri Salome Mbatia.
`Gari hilo lilikuwa mbele yangu, nililiona lakini kwa vile marehemu alitumia gai binafsi, sikujua kuwa aliyekuwemo alikuwa ni Mhe. Mbatia,` akasema Zitto.
Akasema Mheshimiwa Zitto kuwa yeye alifika ndani ya muda wa dakika tano baada ya gari la Mheshimiwa Mbatia kupata ajali, lakini kwa jinsi gari hilo lilivyokuwa limepata ajali hakuwe . Zitto amesema muda mfupi baadaye wakati wakiendelea kuwatoa majeruhi kwenye magari,likafika gari lingine alilokuwemo Bw. Mathayo, ambaye alimtambua moja kwa moja Naibu Waziri Salome Mbatia, kwa vile alikuwa na taarifa za safari yake hiyo na alilijua gari hilo lililopata ajali. `
Mheshimiwa Mathayo ndiye aliyemtambua Marehemu Mbatia,` akasema. Kwa mujibu wa Bw. Zitto wakati wakiendelea kuiondoa miili ya marehemu kwenye magari, pia likafika gari lingine alilokuwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ambaye pia aliungana nao katika kusaidia kuitoa miili ya marehemu kwenye magari ambayo yalikuwa yamepondeka vibaya.
Bw. Zitto akasema baada ya kuona ajali hiyo akaamua kukatiza safari yake na gari lake likatumika kuwakimbiza majeruhi wengine hospitalini. Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Advocate Nyombi amesema dereva wa gari aina ya Fuso liligongana na Gari la Naibu Waziri huyo na kusababisha kifo chake amenusurika.
Kamanda Nyombi ameiambia Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi kuwa aliyekufa papo hapo katika ajali hiyo ni Utingo wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Castory Kilagwa, 22, ambaye ni ndugu wa mmiliki wa Fuso hilo. Amesema hata hivyo Dereva huyo inadaiwa kuwa alikimbia au aliondolewa haraka eneo la tukio, na hivyo hajulika alipo na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
Kamanda Nyombi amesema Polisi imemkamata mmiliki wa Fuso hilo aliyemtaja kwa jina la Jackson Kilagwa ili awaaidie kumpata dereva wake.
`Tunaamini hawezi kumkabidhi mtu mali yake ya thamani kiasi kile bila kujua mahali anapoishi, ndio sababu tunamshikilia mmiliki wa gari hilo ili atusaidie kumpata dereva wake,` akasema Kamanda Nyombi.
Jina dereva wa Mama Mbatia ambaye naye alifariki katika ajali hiyo ni Anaclet Mongella.

Wednesday, August 15, 2007

Mheshimwa Zitto Kabwe Asimamishwa Ubunge!

Mh. Zitto Kabwe

Ama kweli huko Tanzania siasa zinachemka. Habari kwenye ippmedia.com zinasema kuwa Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe, amesimamishwa Ubunge baada ya mzozo bungeni.

*****************************************************************************

From ippmedia.com

Kabwe suspended 2007-08-15 08:52:39

By Pascal Shao, Dodoma


A day of heated debate triggered by a private motion ended dramatically here yesterday with the mover, MP Zitto Kabwe, being suspended after the House voted against him by acclamation. CCM legislator Mudhihir Mudhihir moved a motion to have outspoken Kabwe suspended, saying the MP should be penalised for humiliating Energy and Minerals minister Nazir Karamagi.

Mudhihir suggested that Kabwe be suspended for cheating the House when he accused the minister Karamagi in Parliament on July 17, 2007 of lying in regard to a controversial mining contract which the minister had signed in London.

MPs who spoke in support of Kabwe`s suspension were John Malecela (CCM-Mtera), Adam Malima (CCM-Mkuranga), and Stella Manyenga (CCM-Special Seats). The North-Kigoma (Chadema) MP had earlier kept the minister on his toes throughout the prolonged House session, after he had tabled a private motion requiring the formation of a committee to investigate the mining contract.

Karamagi and a commercial miner signed the Buzwagi Mine deal in February this year, triggering a controversy that has touched off debate among legislators. The latest deal comes at a time when the government is reviewing mining contracts, policies and laws to create what has been termed a win-win situation.

The proposed Parliamentary committee, according to Kabwe, should be tasked to investigate the review of mining contracts signed between the government and investors. He said the on-going mining review process was marred by irregularities and questioned the removal of a provision on Income Tax of 1973 on the 15 per cent capitation allowance on unredeemed qualifying capital expenditure without Parliamentary approval. Kabwe's motion sparked off heated debate, and the House was split into two camps.

The legislator questioned the fast-tracking approach used in signing the contract between the government and Barrick Gold, who own the Buzwagi project. `What basis did the minister use to justify the signing? Why did he say that the contract he signed in London was perfect and had no shortcomings?` he asked. Karamagi told the House on June 16 this year that Buzwagi was simply a marginal mine and that Barrick Gold owned only three mines ? Bulyanhulu, North Mara Gold Mines and Pangea Minerals Limited (Tulawaka) - and according to his statement, Buzwagi was not a mine.

If Buzwagi is not a mine but a project, why did the minister sign the new MDA? According to my understanding, Buzwagi is the second Barrick Gold investment. They have invested $400m on the mine,` he said. `If Buzwagi is a minor mine, why is it that its investment capital has surpassed that of Tulawaka and North Mara?` he queried.

According to the MP, minister Karamagi signed the contract even before the National Environmental Management Council had conducted an environment impact assessment. Kabwe said he had personally reviewed the Finance Act 2002 and also found that in Section 8 of the Income Tax Act of 1973 on the 15 per cent capitation allowance on unredeemed, the Mining Act was not mentioned. The then Finance Minister, Basil Mramba, had once mentioned the ambiguity on the section.

My question is: Why are the mining companies that signed contracts with the government since July 1, 2001 yet to start paying income tax?` questioned Kabwe. All these controversial questions can clearly be disclosed by the proposed parliamentary probe committee ? which can unearth violations of law and corruption elements in these contracts,` he said. `It is a national issue and should be not taken as a party affair.

I believe that fellow legislators will make a decision for the benefit of our country,`Kabwe said. Responding, Minister for Energy and Minerals Nazir Karamagi said Buzwagi was still a project and would qualify to be a mine after being issued with a mining licence, which would be issued after completion of the construction of premises and commencement of mining activities. `Buzwagi is a marginal mine, whose life span is short.

Without using the existing opportunity, especially the price of gold, its investment would not be profitable,` said the minister. `The ministry evaluated the project and found that investors were developing it into a mine. Comparing investments made on Bulyanhulu, which was set up in the 1990s, with the Buzwagi mine that is expected to be constructed in 2008 is not proper, considering the current inflation rate and value of money,` said the minister.

He said Parliament had made amendments to the Income Tax of 1973 and the House had agreed to delete the 15 per cent additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure without considering mining contracts the government had signed with mining companies under the Mining Act of 1998, which was instituted before the changes were made. Karamagi said the meaning of the amendments was that the 15 per cent additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure would be refunded to the mining companies that signed contracts with the government before July 1, 2001.

`This is reason the mines that signed contract with the government before the July 1, 2001 continued with the 15 per cent additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure even after the removal of that section,` he said.

SOURCE: Guardian