Thursday, March 06, 2008

Aisha Madinda Amepona!


Wadau, mnakumbuka mwezi January, niliposti kuwa Mnenguaji Aisha Madinda, anaomba msaada wa pesa za matibabu? Mungu yu mwema! Aisha Madinda amepona ugonjwa wake wa miguu na amerudi kazini.
********************************************************************

Picha na Maelezo kutoka Michuzi Blog:

mnenguaji mashuhuri wa twanga pepeta aisha madinda amerejea ulingoni kwa kishindo baada ya kuwa mngonjwa wa miguu kwa muda kiasi. hapo pichani ni katika shoo ya jumatano katika ukumbi wa maisha. atakuwepo kuonesha makeke yake kwenye shoo za twanga kuanzia leo usiku klabu ya maisha ambapo twanga wanatumbuiza kila jumatano, ijumaa twanga watakuwa dar west park tabata, jumamosi kama kawa ni mango garden kinondoni na jumapili wanaanzia leaders club na kumalizia tcc chang'ombe. kazi kwenu mashabiki wa twanga pepeta, mtoto ndom keshapona huyo na safu ya ushambuliaji imekamilika kama ilivyokuwa siku zote

6 comments:

Anonymous said...

Wale waliomroga wanalia sasa!

Anonymous said...

Sasa mbona hatujasikia ni nani aliyegharamia matibabu yake.

Simon Kitururu said...

Kila la kheri Aisha!

Anonymous said...

Mungu bado anampenda mmependa, lakini yeye hata hamjali.Ila mungu ni wasubira huwa hana haraka wala pupa na viumbe vyake iko siku atamtia mikononi tu, mwache acheze uchi!Alibipiwa mara ya kwanza hajakoma wala hajaona maana ya kumrudia mungu, sasa mara ya pili wallah akisimama mie ntarudi tumboni kwa mama yangu. Tungoje haiko mbali.....

Anonymous said...

Ndugu yangu unayesema Mungu bado anampenda na hajarudia kwake kisha unasema akiumwa tena hatasimama. Mimi sidhani kama hayo ni maneno mazuri ya kumuombea binadamu mwenzako, hujafa hujaumbika cha msingi ni kumuombea kwa Mungu amuongoze katika njia iliyonyooka na si kumlaani kwani hakuna faida yoyote inayopatikana kwa kumlaani iko siku Mungu atamuongoza na ataongoka.

Anonymous said...

Kila la kheri Aisha. Ila nakuomba dada yangu mtangulize Mungu kwa kila jambo kwani yeye ndiye muweza wa yote na bado anakupenda sana.nafurahi kusikia kwamba umerudi tena jukwaani. Kila la kheri na Mungu akubariki. Achana na maneno ya binadamu kwani mara nyingi hujisahau na kuwahukumu binadamu wenzetu nakuomba jaribu kuyachambua yale mazuri na mabaya kwani hakuna binadamu aliyekamilika dada yangu.