Saturday, March 01, 2008

Kingwendu - Mapepe



Hii kideo kinachekesho lakini naona kama maneno ya huo wimbo yanadhalalisha wanawake. Hivi wanaume si mapepe. Ningependa kuona inaimbwa "HUYO DUME MAPEPE!"


9 comments:

Anonymous said...

This is a very funny video. I don't understand what they are saying though.

Anonymous said...

Kweli Tanzania tuna safari ndefu kuhusu haki za wanawake. Maanake hata watoto wadogo naona wanashanagilia, sijui tunafundisha nini watoto wetu. Huu mwimbo ulitakiwa uhakikiwe tena, labda uwe maalum kwa watu wazima tu. Itakuwa ni aibu kama hata watoto wanaimba. KWELI KABISA UNADHALILISHA WANAWAKE!!!

Anonymous said...

Its nice lakini nadhani anaimba pia kuhusu wanaume"hajatulia tulia huyu meni mapepe" katika mstari wa pili kwenye kila chorus..sikiliza vizuri

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Da Chemi,mi nahisi umesikiliza kwa haraka na kutaharuki.

Maana ukisikiliza vema huo wimbo kuanzia sehemu video inapoonyesha dakika ya 4:33 hadi 5:08 amefafanua akisema.Siyo mademu tu mapepe hata mabishoo..hapo akaendelea kutoa ufafanuazi Kingwendu na kuwaonya pia MADUME mapepe..hivyo wimbo u[po sawa..

sikiliza tena..huyo ndio kingwendu gwendulilie..aaa aaa ..lol...

Anonymous said...

Chemi, utakuwa umepotoka pia kama na wewe uta-suggest wimbo huo kuitwa hili dume mapepe, kwani huo pia utakuwa ni UDHALILISHAJI WA MADUME. Usawa wa kijinsia unajumuisha watu wote wanaume na wanawake.

Anonymous said...

wallmind.blogspot.com

Anonymous said...

Tunajua huko busy sana ila ukiamua kuwa blogger inabidi ujitahidi sana au mpe shemeji basi nayeye akiwa free awe anatuletea habari nimechoka kila nikifungua namkuta kingwendu na ninavyomchukia huyu kiumbe mungu nisamehee sipendi ujinga wake anaofanya kuonyesha mate yake siwezi hata kumpa mkono

Anonymous said...

Nasdhani kuna wakati hili songi lililwekewa zengwe na likawa halirushwi hewani kwa sababu ulionekana kama unakandamiza jinsi fulani

Ila pia anasema kuna ma meni mapepe, ila msisitizo ni kwa demu

Anonymous said...

Hii video cha mtoto kuna nyingine ya KIngwendu inaitwa "Mipango sio matumizi".