Wednesday, March 05, 2008

Senator Hillary Clinton Afufuliwa! - Uchaguzi 2008


Majuzi watu walikuwa wansema kuwa ni bora Senator Hillary Clinton, ajitoe katika mashindano ya kugombania urais wa Marekani. Hiyo ni baada ya Senator Barack Obama, kushinda katika states 12 mfululizo.

Jana Senator Clinton alishinda states za Ohio na Texas ambazo zina wajumbe wengi watakao piga kura katika mkutano mkuu wa Democrats mwezi Agosti. Hao ndo wanampitisha mgombea. Pamoja na ushindi wake Obama bado ana kura nyingi.

Kwa kweli sijafurahi hizi wiki mbili zilizopita kuona jinsi Mama Clinton alivyochafua jina la Obama. Mara aseme hawezi kuwa na uhakika kuwa si mwislamu. Na alifanya hivyo maksudi kwa vile alijua waMarekani ni waoga na waislamu baada ya mashambulizi ya 9/11. Halafu walifufua ile picha aliyopiga Kenya amevaa nguo za kiSomali mwaka 2006. Na kuna maovu mengine ambayo kampeni yake ilifanya.

Naomba mjue kuwa ubaguzi bado upo hapa Marekani. Hasa katika hizi states za Kaskazini. Sijui kama mlisikia yaliyotokea jana huko Ohio kwenye maeneo ya weusi. Weusi walijitokeza kwa wingi kupiga kura lakini walishindwa. Mfano, sehemu moja walikuwa na kura 50 na watu 300 walijitokeza. Hivyo watu wengi walishindwa kupiga kura. Ilibidi watu wa Obama wamwombe jaji aamuru shemu za kupiga kura zikae wazi kwa saa moja zaidi ili watu wapate nafasi ya kupiga kura. Matatizo kama hayo yalitokea hapa Massachusetts kwenye maeno ya weusi wakati Gavana wetu, Deval Patrick, alivyogombania.

Pia huko Ohio kulikuwa na matatizo kibao, hitilafu za mashine, matishio ya mabomu na mengine.
Halafu washenzi kama Rush Limbaugh, waliomba marepublicans wampigie Senator Clinton kusudi Obama asishinde. Alisema Clinton akishinda basi atazidi kumpaka matope Obama. Siasa bwana!

Leo, Hillary anadokeza kuwa kama atachuguliwa kuwa mgombea wa Democrats atamchagua Obama kuwa running mate, yaani makamu wake. Sijui kama mimi ningekuwa Obama ningekubali maana huyo Mama Clinton ameonyesha ana ukatili ndani yake. Yuko tayari kufanya chochote ili ashinde.

Pia Bush akiondoka January 2009, ataacha nchi na hali mbaya sana ya kiuchumi na kila kitu. Ambaye atashinda atakuwa na kazi kubwa mbele yake. Mungu ambariki atakayeshinda.
Kwa habari zaidi someni:

5 comments:

Anonymous said...

Uchambuzi wako ni mzuri japo uko biased.Mbona huzungumzii impact ya skendo la Rezko,ambapo majuzi Obama alionekana kabisa kuelemewa na maswali ya mapaparazi?Vipi kuhusu kuyumba kwake kwenye suala la NAFTA?Kusema ubaguzi ni moja ya sababu za yeye kushindwa ni ku-miss point,je hizo previous consecutive wins za Obama zilizikuwa kwenye states za weusi pekee?Labda article hii ya washington post inaweza kukusaidia kuondoa bias yake ktk analysis
http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2008/03/04/AR2008030403392.html?hpid=topnews

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:34PM, asante kwa mchango wako. Hiyo skandali ya Rezko nimesikia na kuwa Obama alinunua ardhi kwa bei chee.

Ila hao akina Clinton wana skandali kubwa kuliko hiyo ya Rezko. Wao wana Whitewater. Wataalam wanasema hiyo ya Obama ni 'small potatoes' Labda watu wamesahau.

Kuchambua inahitaji mada ya peke yake.
Asante.

Anonymous said...

Kama the Clintons wana skendo nzito zaidi ya hiyo ya Obama then yeye (Obama) anashambuliwa na kukaa kimya,kuna haja kweli ya kumhurumia?Tukubali tusikubali,Obama amekuwa akipata special treatment from media hata kwenye ma-conservative kama FOX.Of recent,Billy O'Reilly amekuwa akilalamika waziwazi kuhusu vituo kama CBS ambavyo vimekuwa vikimpa Obama an easy ride.Kwa hakika hakuwa na sababu ya msingi ya kushindwa Ohio na Texas.Kama ishu ni ubaguzi,huko kwingine alishinda vp including states ambazo ni predominantly White?
In fact,akina Clintons hawajakuwa so harsh to Obama bcoz laiti wangeleta hoja kwamba Obama has been a chairman of subcommettee flani ya foreign affairs na hajaitisha meeting hata moja,hilo linge-support madai kuwa agenda yake ya hope ni hypotherical than practical.
He had to win bcoz Hillary amekuwa target ya kila kona,na only scrutiny abt Obama ni hii wiki iliyopita.

Angalia mfano huu wa media bias quoted from the Politico.com
" a Nexis search of major world newspapers Tuesday yielded 2,568 hits for the words “Clinton” and “Hsu” versus only 426 for the words “Obama” and “Rezko.” Expanding the search to include all media outlets, the Clinton/Hsu query produced more than 3,000 hits, while Obama/Rezko turned up 1,741" Unaweza kusoma makala nzima kwenye link hii
http://www.politico.com/news/stories/0308/8855.html

Pia Gallup Poll inaonyesha Hillary amerejea kileleni nation-wide
http://www.gallup.com/poll/104788/Gallup-Daily-Clinton-48-Obama-44.aspx

Na hawa wanaolalamika wanaweza kuwa na point pia
http://www.tuscaloosanews.com/article/20080304/APP/803040759

Samahani kwa kuweka links nyingi.Mie pia natamani sana Obama sio ashinde tu nomination ya Democrats bali aingie Ikulu kabisa lakini napendelea zaidi kuwa objective than subjective,tatizo ambalo sisi watu weusi limekuwa likitusumbua kwa muda mrefu.

Anonymous said...

Nami sikatai naona Obama kapata easy ride kweli. Sijui wanaogopa kwa vile ni mweusi wataitwa racists.

Anonymous said...

kuhusu media mie nina swali moja, je kipi kilitangulia-mafaniko ya Obama au easy ride?? Lazima mkumbuke kuwa kila mtu anapenda kujihusiha na mafanikio.

Obama amefanikiwa kuwanyamazisha "pundits" wote kwa maneno mengine amezidi matarajio (exceeded expectations).

Haya maswala ya media yameanzishwa na Hilary baada ya kulalamika kuwa huwa kwenye debate anaulizwa swali la kwanza kila mara.

Ubaguzi upo, Chemi-lakini Obama ni aina ya kiongozi mpya ambaye anajaribu kuunganisha rangi zote-na kwenye huu uchaguzi amefanikiwa.

Kama anony hapo juu alivyosema-tusikimbilie sana swala la ubaguzi, kampeni ni ngumu sana na huyo Mama Clinton ni mpiganaji haswa-hatakubali kushindwa kirahisi.