Leo nimefanya audition kwa ajili ya sinema mpya, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis. Hadithi yake ni ya Science Fiction.
Role niliofanyia audition ni mama moja mwenye hasira ambaye anamwua character wa Bruce Willis kwa kumpiga risasi kichwani. Ila siye mwenyewe ni kloni yake.
Ilibidi nifanye 'pantomine', yaani kuigiza bila kifaa. Sasa waliniambia nijifanye nimeshika bunduki na naifyatua baada ya kusema line. Hapo ilibidi nikumbuke mazeozi ya SAR (semi-automatic rifle) ya enzi za JKT.
Ilikuwa audition safi sana kwa vile niliambiwa kuchangaya action na maneno. Haya sisi actors tunaambiwa ukifanya audition tegemea hapo ndo mwisho, ukiitwa tena ni bahati wakikuchagua ni kama kushinda bahati nasibu! Haya tuone mambo yatakavyokuwa.
Ila nilifurahi sana kuona waigizaji wengi weusi waliitwa kufanya audition.
Kwa habari zaidi ya sinema, The Surrogates bofya HAPA:
11 comments:
Big up sister, I am so proud of you.
Kama sinema ina star Bruce Willis na ukipata hiyo role si itakuwa break yako! Hongera sana. Tutakuombea upate. Usipopata usiwe na wasiwasi utapata nafasi nyingine.
Asante and Thank-you both for your nice comments. Asante sana. Kwa bahati nzuri mwaka huu sinema nyingi zinapigwa Massachusetts. Hata nisipopata role ya kuongea kazi ya 'extra' napata. Asante.
Nakutakia kila la kheri Dada Chemi!
i wish all the best, i hope you will get that role, i pray for you sister
best of luck
Kumbe muigizaji Chemi mungu atakusaidia.natamani ningeenda na mimi kwani wanajali figure ya mtu pia na mambo ya sura hivi?kama ni hivyo basi nitaweza kupita maana Iam a very good actor not by prof lakini Iam sure I can act if I get a chance gooooood luck sweet sister
Da Chemi,
tupo pamoja nakuombea ufanye vema.
Haijalishi mtokeo yatakayo kuja,ila naamini upo mbali na unaweza kufika mbali zaidi.
Kila la kheri
Asanteni Simon, Edwin, na maanonymous wote. Kwa kweli competition ni kubwa na sitashangaa kama watamchangua mzungu kufanya hiyo role. Lakini kuitwa tu ku-audition ni jambo kubwa!
Kwa wanaotaka kuingia kwenye acting hapa USA niko tayari kuwaongoza. Nilishasema siku nyingi. Na kama nilishawahi kuandika kwenye blogu ni waNigeria na waSouth Africa ndo wanatamba Hollywood. Siku hizi kidogo unasikia waKenya. Nataka kusikia na waTanzania wanatamba huko pia.
UNAFIKIRI WATU HATUPENDI DADA CHEMI MIMI MAIMUNA NDIO OUR MAJOR PROBLEM LAKINI HII NI KWASABABU MOJA WE TANZANIANS ARE SO IGNORANT.UNAJUA TABIA YA KUPUUZIA NI MAMBO NI MBAYA SANA TENA KAMA UNAJUA UMUHIMU WAKE UNAJIFANYA UFAHAMU.PIA KUAHIRISHA JAMBO KWAMBA NITAFANYA BAADAE AU KESHO NI KOSA SANA.KWA WALE AMBAO MMEISHI NCHI ZENYE WA WEST AFRICANS WHAT DO YOU SEE FROM THEM.WORKERHOLICS RIGHT !!! KWASABABU WANAJUA KESHO AU KESHO KUTWA WATAPUMZIKA SASA SISI UNAKUTA MVIVU UNARIDHIKA NA VIHELA HIVYO HIVYO KILA SIKU BASI SASA MAENDELEO UTAPATA WAPI.SASA ATAKAE CHUKIA AU ANAONA NASEMA UONGO BAKI HIVYO HIVYO LAKINI KAMA UNAONA NAONGEA CHA KWELI CHUKUA ATA 1% YA HII BAADAE KAA FIKIRIA KUMBUKA MARAFIKI ZAKO WOTE UONE KUNA UKWELI AU LAAAAAAAA(TUACHE TABIA YA KURIDHIKA NA MAKARATASI YA NJE AU BENEFIT )
HILDA
Dada Chemi, acting unahitaji moyo. Wengine tunatamani lakini moyo wa acting hatuna. Nakusifu kwa jitihada zako.
Dada chemi hongera sana kwa hiyo hatua uliyopiga, kupata audition ya kuigiza ni neema,na mungu atakubariki na meningine tele. Keep-up good work.
Mariah
Post a Comment