Wednesday, March 12, 2008

Gavana Mpya wa New York atakuwa Mweusi!


Si muda mfupi tutasikia jambo la kihistoria. Gavana alieyaibika kwa kutembea na malaya, Eliot Spitzer, anatarajiwa kujiuzulu leo. Makamu wake Lieutenant Governor, David Paterson, 53, ataapishwa mara moja.

Paterson atakuwa ni mweusi wa kwanza kuwa Gavana wa New York, na Gavana wa nne mweusi katika historia ya Marekani. Pia atakuwa ni Gavana wa kwanza asiyeona (kipofu) katika historia ya Marekani! Mungu ambariki Bwana Paterson!

Sasa kuhusu huyo Spitzer aka. Client No. 9, aka. Eliot Ness, aka Mr. Clean, anazidi kuaibika. Wanachunguza alipata wapi dola $80,000 za kulipa malaya wake. Pia kashitakiwa chini ya Mann Act ya 1910, inayosema kuwa ni marufuku kumsafirisha mtu kati ya majimbo kwa ajili ya ngono. LOL! Pia imefahamika kuwa alivyokuwa anatembea na malaya alikuwa hatumii kondomu! DOH! Mke wake lazima atakuwa amechukia kweli hapo!

Kwa habari zaidi someni:

2 comments:

Anonymous said...

utatumiaje kondomu uku unatembea na mtu!?mbona sasa chemi unaharibu kiswahili ama ii ndi kiswanglishi?

Anonymous said...

Wewe anony wa juu yangu hujui kiswahili nini? Kutembea hapa manake kufanya sex!