Saturday, March 01, 2008

Hali ya Maisha inazidi kuwa mbaya Marekani!

Great Depresssion Soup Kitchen 1933

Asante Rais Bush, hali ya maisha kwa Mmarekani wa kawaida unazidi kuwa mbaya. Bei ya kila kitu kimepanda mishahara iko pale pale.
Ukienda dukani bei ya kila kitu kimepanda, mkate, mayai, maziwa, nyama, sukari. Jana nilimsikia mtu mwenye restaurant akisema kuwa zamani watu walikuwa wananunua sana large pizza. Alitoa mfano ya familia ya watu wanne. Zamani waalikuwa wananuna kubwa lakini siku hizi hawana hela wananunua medium na inabidi iwatoshe wale wale..
Bei ya kumwona daktari umepanda. Bei ya petroli imepanda na wanatabiri utafika hadi dola $4 kwa galoni kabla ya mwezi wa saba. Watu wanapoteza majumba yao kwa vile wanashindwa kulipa mortgage. Watu wanashindwa kulipa na biliz ao zingine.
Pantries zinazotoa chakula kwa maskini zinasema kuwa hata wasio maskini wanaenda kupata misaada.
Unajua hali umekuwa mbaya ukiona wazungu wanalamika. Maana kwa kawaida wao wanakuwa na hali nzuri. Wanapata kazi nzuri na mishahara mizuri na mortgage zenye rate nzuri kuliko minorities yaani weusi na waspanish.

Na wataalam wa uchumi wanasema haliutazidi kuwa mbaya! Watu watazidi kupoteza kazi na kufukuzwa kwenye majumba. Wanasema hali unaweza kuwa mbaya kama GREAT DEPRESSION ya miaka ya 1930's.
Sasa kuna wimbi la wafanya biashara kutoka nchi za nje waliokuwa na biashara hapa USA, kuondoka na kuaacha biashara zao. Wanaziacha na madeni. Leo unawaona kesho hawapo.
Juzi Rais Bush aliulizwa kuhusu bei ya mafuta na waandishi wa habari. Alijibu kuwa hana habari. Watu walizidi kumchukia.

Sawa alienda Afrika na kutoa misaada. Watu wanasema ilikuwa ni 'Guilt Trip'. Yaani anapooza moyo wake kwa maovu aliyofanya akiwa rais kama kuanzisha vita isiyo na maana huko Iraq.

Sasa watu wanamwona Senator Obama atakuwa mwokozi wa nchi hii. Wanavyomwamudu! Na mimi najua kuwa Obama atakuwa rais mzuri. Ukiwa mweusi nchi hii ni lazima ufanye kazi mra nne ya mzungu kusudi uonekane umefanya kitu.
Mungu awape nguvu waMarekani nguvu katika kipindi hiki kigumu!
Kwa habari zaidi ya hali ngumu ya maisha Marekani someni:

3 comments:

Anonymous said...

Rudini Bongo rudini Bongo. Kisascha kusota uzunguni!

Anonymous said...

Uliona wapi kwa ugumu wa muwa mlaji... kaususia...Habanduki mtu hapa... mpango tumalize kifundo...Ganda la muwa la jana haleshi kuona kivuno... Kwaheri

Anonymous said...

Huo ubaya unaozungumzwa ni kwa wamarekani/wageni wala hawaambiwi . Utashangaa hachomoki mtu, na wewe utaendelea kukuota tu.Ukiona kidonda ni kibaya na kichafu inzi msafi hufiaga papo hapo.. Kwaheri