Thursday, March 20, 2008

Deodorants Bongo

Deodorants za Kike
Deodorants za Kiume

Kwanza ni nini mtu utumie deodorant?

Inajulikana kuwa Jasho pekee halina harufu ila kunapokua na bacteria na unyevunyevu kama vile kwapani hapo ndipo harufu huwepo.

Kwapa ni mojawapo ya eneo la mwili ambalo lina joto na unyevunyevu karibu muda wote. Na nywele kwapani zinaongezea harufu kwa kuwa zinawapa bacteria eneo zaidi la kuzaliana.
Deodorants zinasaidia kuzuia harufu na kupunguza jasho kwapani. Deodorants bora zenye perfum mbalimbali zapatika SINZA MAPAMBANO, karibu na Africasana.

Kwa maelezo zaidi piga au tuma sms kwa Beauty Specialist
@ 0784-521171 au email deodorants123@yahoo.com

****************************************************************************
Wadau, nimefurahi kuona hii tangazo kwa Michuzi maana wakati mwingine Bongo unakutana na mtu ana Kikwapa hasa. Si mwanaume si mwanamke. Mara ngapi umeshuka kwenye daladala uliyojaa na unanuka jasho la mtu mwingine. DUH. Kwa wasiojua matumizi zinapakwa makwapani kila baada ya kuoga.

13 comments:

Anonymous said...

CHemi wewe ndio umeandika hiyo paragraph ya mwisho ?kama ni wewe nitasikitika sana kama na wewe uko kwenye mkumbo wa kuwatusi ndugu zako

Anonymous said...

Wabongo hatutaki kusikia habari ya vikwapa lakini kweli kero. Tumieni deos jamani!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 2:11PM, asante kwa maoni, na samahani kama nimemtusi mtu. Ukweli ni kwamba hatupendi kusikia ukweli. Wakati mwingine unakutana na mtu 'kawaiva' kweli. Nikisema sijawahi kukutana na mtu mwenye kikwapa Bongo nitakuwa nimesea uwongo. Na si mila ya nchi nyingi za Third World kutumia hizo deo.

Hata hapa USA unaweza kukutana na mtu mwenye Kikwapa.

Summer iliyopita, mume wa jirani yangu anatoka Dominican Republic, alikuwa anatembea nje bila fulana. Tulikuwa upande wa pili wa barabara lakini tuliipata hicho kikwapa.

Ubaya sehemu za kazi mtu kama huyo anakuwa labled kama mtu mwenye 'poor hygiene' (usafi wa mwili). Na ni grounds ya kumfukuzisha mtu kazi.

Kuna jamaa nilikuwa nafanya kazi naye. Alitoka Nigeria. Sasa anaingia kazini smart, ikifika saa 4 unaanza kumsikia. Wazungu hawakupenda ingawa alikuwa anafanya kazi vizuri. Nilijaribu kumwelemisha kuhusu deos, akasema anaoga kila siku. Aliitwa HR na kupewa onyo, bado aligoma. Mwisho walimfukuza. Alikuwa hana la kufanya maana ilikuwa imeandikwa wazi kwenye employee handbook ambayo una saini kuwa umepokea. "Poor personal hygiene is grounds for termination"

Anonymous said...

Usiombe kwenda saluni na kusukwa nywele na msusi mwenye kikwapa! Bora umesema Da Chemi. Deo oyee.

Anonymous said...

Sisi Tanzanians ni wanafiki. Tunaongea na mtu, tunamchekea huko ana kikwapa. Tukitoka kuongea naye tunaenda kuwaambia watu fulani ananuka! Sema mengine dada!

Anonymous said...

Vibaya Da Chemi! Hakuna mbongo mwenye kikwapa wote tunanukia freshi. Umekuwa mzungu!

Anonymous said...

ASANTE SANA! MAENDELEO HAYO! SIYO UNAKUTANA NA MTU KAVAA VIZURI HALAFU ANA UVUNDU!

Anonymous said...

wewe chemi,wewe mwenyewe,wakati unasoma zanaki ulikuwa na kikwapa,sasa leo ushakuwa mtaalam wa kukosoa watu

Anonymous said...

Enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna deo inauzwa Bongo. Hiyo kitu imeingia siku hizi. Hivyo siku hizi hakuna sababu ya mtu kuwa na kikwapa Bongo kama ana hela ya kununua.

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wadau wote kwa maoni. Mdau wa 12:35pm, actually siku zote hata enzi Mwalimu wahindi City Centre walikuwa wanauza deo za 'Mum', ndo tulikuwa tunanunua kwao. Halafu hawakuwa na variety kubwa. Lakini sikuziona sehemu zingine kama Kariakoo.

Anonymous said...

Na mimi nasema asante kwa kuposti. Ingawa hatutaki kukubali hizo deo ni kitu kigeni kwetu au tunaweza kuona ch kizungu.

Sababu ya watu kuvaa vizuri lakini wanakuwa na vikwapa ni kwa vile wanadhani kupaka perfume kwenye nguo itaondoa arufu. Bora wewe umetoa somo ya kupaka deo kwapani mara baada ya kuoga.

Nasema tena asante kwa niaba ya ndugu zetu wanaoona aibu kuzungumzia hiyo suala.

Anonymous said...

Sema Usiogope Sema! Naomba uwapashe wanaume wabongo kuhusu jinsi miguu yao invyonuka vibaya. Wanavaa soksi na viatu haviendani na joto. Miguu inanuka.

Anonymous said...

jamani mbona hizo deodorant zimejaa bongo!nenda pale S H AMON zipo tele yaani zinavyoelezwa hapa kama kitu kipya. pili jamani angalieni hazina chemicals acive ingredient iwe natural maana zingine zinasadikika ni factor katika breast cancer kwa wanawake.Angalieni jamani msipeleke bidhaa zinazoanza kukosa soko zikawadhuru watu. Ukitaka uhakika wa zilizo bora nenda health stores ziko zilizo natural. asanteni