Tuesday, March 04, 2008

Mji wa Dar es Salaam kukosa Maji siku Tano!


Wadau huko Dar, naomba mtueleze hali ilivyo kule. Poleni sana!
*****************************************************************
TANGAZO.
Dar kukosa maji siku tano

Kutoka Food for Thought Blog

JIJI la Dar es Salaam, litakumbwa na uhaba wa maji kwa muda wa siku tano kuanzia leo.Taarifa ya kukosekana huko kwa maji imetolewa jana kwa vyombo vya habari na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) kwa niaba ya Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASA).

Hata hivyo, ukosekanaji wa maji hayo ambao unatokana na kufanyiwa ukarabati mkubwa wa mtambo wa Ruvu Juu utayakumba baadhi ya maeneo ya jiji.Kwa mujibu wa Dawasco, ukarabati huo mkubwa wa mtambo umearifiwa kufanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka (Dawasa).
“Dawasa inawataarifu wakazi wa jiji kwamba mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu utafanyiwa ukarabati mkubwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Jumatatu Machi 3 hadi Ijumaa Machi 7, 2008 hivyo kusababisha kutopatikana kabisa kwa maji baadhi ya maeneo ya jiji,’ ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa maeneo yaliyotajwa kukumbwa na ukosefu huo wa maji ni ambayo yanapata maji kutoka Ruvu juu.

Maeneo hayo ni Kibaha, mkoani Pwani, Kibamba, Mbezi, Kimara, Changanyikeni, Ubungo, Kibangu, Makuburi, Tabata na Kisukuru. Dawasa imewaomba radhi wateja wake kwa usumbusu utakaotokea wakati wa ukarabati huo.

2 comments:

Anonymous said...

Nawapa pole sana wakazi wa Dar yaani wanavyo nyanyasika na hayo Majai? Mbona moshi husikii waki teseka na Maji wamewezaje? Natoka nje ya topic kidogo Dachemi tupe habari za Baraka Obama mbona siku hizi kimya?

Anonymous said...

Yaani matatizo ya maji Dar bado tu! Ni miaka mingapi tangu Uhuru? AIBU!