Tuesday, March 04, 2008

Mnakumbuka?


Nani anakumbuka enzi za Mwalimu mtu akitaka kusafiri nje ya nchi?

1) Uombe STATE HOUSE CLEARANCE (bahati yako ukipata)
2) Upate kibali cha INCOME TAX
3) Uwe na kibali cha kununua fedha za kigeni. Mara nyingi unaruhusiwa dola $70 tu! Yaani wabongo walikuwa wanasafiri kimaskini kweli! Na mtu anayekupangia utapata ngapi, una bahati ukiambulia dola $40!

4) Ukitaka kununua tiketi ya ndege mpaka upate ruhusa. Kama unaletewa kutoka nje ni sawa.

5) Na ukirudi hizo harassment airport! Wakati huo vitu adimu hivyo sharti/kiatu mpya mali, sabuni/dawa ya mswaki mali.
Ni kweli vijana walikuwa hawatoki nje ya nchi kirahisi. Wakati huo kuzamia meli ndo fesheni.
Bongo kuna stories si mchezo. Kweli ilikuwa ukitoka njea ya nchi lazima watu wakuonee wivu.

5 comments:

Anonymous said...

DOH! Enzi hizo mtu ukifanikisha hatu zote za kutoka nje ya nchi unalia machozi ya furaha! Unaona ndege kama mkombozi wako!

Vijana hawajui habari ya mateso ya enzi hizo! Foleni, bidhaa adimu!

Anonymous said...

Nyerere katurudisha nyuma sana. Tulikuwa tunalipishwa kodi ya kumiliki Tv set ili yeye peke yake awe nayo tuu. Tunashukuru kwa umoja na siye yeye aliyeujenga ila ustaarabu wetu wa kuishi pamoja ndio ulioleta amani.Kama unavyosema kusafiri ndio ilikuwa big deal utaona gari ya mashushu usiku mzima karibu ya nyumba yako, kila kitu sasa ni historia na tushukuru Mungu.

Anonymous said...

sasa enzi hizo nje unaenda kufanya nini? mbona wanasema zamani mambo yalikuwa safi

Anonymous said...

Anonymous wa 5:21PM, enzi hizo ilikuwa mwiko kuwa na TV. Zanzibar ndo walikuwa wanaruhusiwa kuwa na TV. Ilikuwa ukileta TV una nyang'anywa! Au unweza kufungwa jela! Watu has wahindi walitupa matv baharini si mchezo!

Mwinyi ndo aliruhusu TV bara!

Anonymous said...

Enzi hizo ukisafiri unaondoka na briefcase tu. Sharti uliyovaa umechaka. Ukirudi una masandauku yamejaa sabuni, nguo, viatu, dawa ya mswaki na wewe uko smati! Kila mtu anajua katoka Ulaya huyo. Ananukia!