Leo asubuhi mwanaume aliyekuwa anavuka barabara alikanyagwa na lori Cambridge! Habari zinasema kuwa jamaa alifariki hospitalini. Marehemu ametambulika kama Graduate Student wa Harvard University mwenye miaka 28. Jina linahifadhiwa mpaka familia yake inajulishwa.
Ajali hiyo ilitokea kwenye kona ya Massachusetts Ave. na Prospect St., (pichani) pale unapopandia subway (treni) Red Line. Nilifika baada ya jamaa kuchukuliwa na ambulance. Watu walioshuhudia wanasema alikuwa na hali mbaya sana. Nilisikia watu wakisema, "this is the worse thing I ever saw!"Aliyekuwa anavuka barabara hakuwa na kosa maana taa ilikuwa ya waenda kwa miguu. Kwa wanaopafahamu pale Central Square, Cambridge, magari yanaruhusiwa kupinda kona huko watu wanaruhusiwa kuvuka. Ila wenye magari wanatakiwa kupisha waenda kwa miguu. Kila siku napita pale na lazima niseme huwa wakati wenye magari hawaheshimu waenda kwa miguu! Wanakupita kwa mbele au nyuma bila kujali.
Sasa leo asubuhi maskini, huyo mwanaume alikuwa anavuka barabara na lori ya SHAW's supermarket, tena zile kubwa kabisa 18 wheeler ilikuwa inapinda kona. Jamaa alikanyagwa na magari ya nyuma na kuburuzwa hadi kwenye taa nyingine pale mbele ya Dunkin Donuts na Liquor Store. Hiyo lori imesajiliwa Maine. Sidhani kama malori yanaruhusiwa kupita kwenye hiyo barabara nyakati hizo.
Kulikuwa na alama ya madamu na nyama za binadamu kwenye barabara! Hiyo alama ya damu inaonyesha jamaa alivyoburuzwa! Watu walioshuhudia wanasema kuwa ilibidi watu wapige makelele kumwambia dereva wa lori kuwa amemkanyaga mtu!
Nimeona nyama na vitu vyeupe sijui ndo mifupa. DOH! Wewe leo nimeona watu walioshuhudia wakichanganyikiwa! Nilimkuta jirani yangu (mwanamke kutoka Haiti) analia, ilibidi nimsindike hadi nyumbani kwake ndo nianze safari tena ya kuelekea kazini. Mimi mwenyewe bado natetemeka nikikumbuka zile nyama na madamu barabarani!
Cambridge police, State police walitokea na walizungusha eneo yote kuanzia kwenye kona ya Mass Ave. hadi kwenye kona ya Pearl St. na kamba ya njano (crime scene). Nafuatilia kuona kama wataweka habari zaidi kwenye TV. Nimepiga picha lakini sijaziprocess bado.
Cambridge police, State police walitokea na walizungusha eneo yote kuanzia kwenye kona ya Mass Ave. hadi kwenye kona ya Pearl St. na kamba ya njano (crime scene). Nafuatilia kuona kama wataweka habari zaidi kwenye TV. Nimepiga picha lakini sijaziprocess bado.
Na vituko havikuisha hapo! Nafanya transfer kwenda kazini. Nilikuwa nangojea treni ya Orange Line pale Downtown Crossing halafu nilishuhudia jamaa akiruka kwenye reli. Treni ilikuwa inakuja nikahofia atakanyagwa. Lakini alipanda juu ya platform kabla treni haikumfikia! DUH! Kabla hajaruka kwenye track alinipita anaongea peke yake.
Kwa habari zaidi soma:
http://www.thebostonchannel.com/mostpopular/15619169/detail.html
1 comment:
This is a very saddening story. I always thought drivers in the west respect traffic lights, kumbe ni otherwise. Condolences to the family of the deceased
Post a Comment