Tuesday, March 04, 2008

American Idol in WANAFIKI!

Antonella Barba (kushoto) Frenchie Davis (Kulia)
David Hernandez
UPDATE 3-5-07 Producers wa American Idol wameruhusu David Hernandez kubaki! Kweli ni wanafiki. Frenchie alionyesha matiti yake, huyo njemba alikuwa uchi wa nyama! Unafiki kabisa! BOFYA HAPA kusoma UPDATE
****************************************************************************

Leo nimechukia sana kusikia kuwa mmoja wa contestants wa American Idol mwaka huu, David Hernandez, aliwahi kuwa stripper! Tena alikuwa anavua ana nguo kabisa na kubakia uchi wa nyama na kucheza ma lap dance! Ustripper huo alikuwa anafanya kwenye bar ya mashoga/wasenge. Hao aliokuwa anawachezea lap dance ni wanaume. Alifanya hiyo kazi kwa muda wa miaka mitatu.

Ukweli nisingejali kusikia habari kama hizi. Maana kwa hapa Marekani kuna watu wengi wanaofanya kazi ya stripper na kucheza hizo lap dance. Tena huyo David anaimba vizuri kweli.

Kinachoniudhi tena sana ni hivi. Kuna dada fulani, mmarekani mweusi, Frenchie Davis, amabaye aliwahi kufukuzwa na producers wa American Idol mwaka 2003. Kisa cha kufukuzwa kwake, alipiga picha akiwa nusu uchi matiti yanaonekana. Frenchie aliwaambia producers mapema kuhusu historia yake na alisema kuwa alikubali kupiga picha hizo kwa vile alihitaji pesa za kulipia ada zake Chuo Kikuu.
Producers hawakumwonyesha huruma hata kidogo Frenchie, alifukuzwa kama mnyama. Je, ni sawa? Kuna watu ambao wanasema kuwa ni wazi kuwa American Idol wana 'double standard'. Pia kuna watu ambao wanataka Hernandez atolewe kwenye mashindano mara moja maana si mfano mzuri kwa vijana na si mtu anayestahili kuitwa 'American Idol'

Mwaka jana kuna binti wa kizungu, Antonella Barba ambaye naye alikuwa na picha kwenye interenet lakini hwakumfukuza.

American Idol wamwombe msamaha Frenchie au wamrudishe apate chensi kama walivyopata hao wazungu waliofanya maovu zaidi yake. Mnasemaje?

Kwa habari zaidi someni:

http://www.mtv.com/news/articles/1582721/20080304/id_0.jhtml

4 comments:

Anonymous said...

A Double Standard indeed. American Idol producers should ashamed of how Frenchie was treated. In fact all traces of Frenchie were 'smote' from their website after they kicked her off.

Anonymous said...

kwani huko marekani matiti ni uchi?

Chemi Che-Mponda said...

Hapa nawashangaa sana. Mwanamke akinyonyesha hadharani ni dhambi kubwa anaweza kufungwa jela. Wanathamini matiti ya mwanamke kuliko huko chini! Kwa kweli wamemwonea huyo dada.

Anonymous said...

Chemi ni kweli lakini matiti funga kazi mama,we huoni watu wanavoyatafuta kwa masindano yajaejae!.Pia,fikiria kuwa mwanamke afu huna matiti utaonekanaje?Pamoja na double standard zao hio pia ni njia ya kutujulisha kwamba mtu mweusi hapaswi kushiriki katika madudu kama hayo,kama kupiga picha uchi.Huu si utamaduni wa mtu mweusi(mwafrika)tuwaachie wao wenyewe,waendelee na laana hiyo.