Monday, March 10, 2008

Gavana wa New York achunguzwa baada ya kukutana na Malaya!

Gavana Spitzer na Mke wake leo baada ya kukutana na waandishi wa habari
DOH! Leo tumesikia mchapo wa aibu wa Gavana Eliot Spitzer, wa New York kukutana na malaya akiwa kwenye safari Washington D.C. . Kwa kweli hapa Marekani ni jambo la aibu kwa kiongozi kufanya upuuzi kama huu.
Na kama kawaida ailiitisha Press Conference na kuongea na waandishi wa habari. Lakini nauliza hivi, kwa nini hao viongozi wakifanya maovu ,wake zao wanatoka pamoja nao na wanapigwa mapicha. Kweli hutakuwa na hasira na aibu kusikia jambo la aibu kama hili?
Aliomba msamaha kwa watu wa New York na familia yake. Lakini hajajiuzulu. Leo ndo kwanza tumesikia hizi habari chafu za Gavana Spitzer ambaye nickname yake ni 'Mr. Clean' (asiye na kasoro). Nadhani siku zinavyoenda tutasikia habari zaidi za aibu na itabidi aachie ngazi.
FBI wanasema kuwa wametepu! Kwenye tepu zao wanamwita 'Client No. 9' Pia wanasema huyo malaya sijui kalipwa dola $5,000 kwa saa! Sijui kazilia yeye au walipe kodi wa New York!
MAKUBWA!
Kwa habari zaidi someni:

8 comments:

Anonymous said...

KABAMBWA NA FBI! SIJUI KAWAKOSEA NINI HUYO GAVANA MZIMA! KWELI NI AIBU!

Anonymous said...

Yes, this man must step down! Our next Governor will be a black man!

Look at the look on his wife's face, she is embarassed to he-lll!

Anonymous said...

Tusidanganyane kwenye mambo haya, hakuna asiyepataka kule chini. Wanaume wanataka wajaribu chini ya kila mwanamke mzuri. Wanawake nao hutaka kujaribu chini ya kila mwanamme wanayemsujudu, basi tu mambo ndiyo yalivyo. Hata walokole wa evangelicals wamekuwa wanakumbana na kashehe hizi huku wakidai no gay marriage halafu wao wenyewe wakienda kuwavuruga hao hao ma-gay huko mafichoni.

Ukimwona mke wako akirudi kazini kavalia kama alivyoondoka nyumbani asubuhi, usidhani kuwa mambo yote mswano; inawezekana wenzako washakuvurugia. Vile vile ukimwona mme wako akirudi nyumbani na kujidai kachoka, usishangae kwani wenzako wanaweza kuwa wameshakuchoshea.

Kinachotakiwa ni nidhamu ya hali ya juu ama sivyo mambo haya ni vanguvangu tu.

Anonymous said...

AJIUZULU! MAREKANI HAWANA MCHEZO NA WAZINZI! RESIGN!

Anonymous said...

AJIUZULU! MAREKANI HAWANA MCHEZO NA WAZINZI! RESIGN!

Anonymous said...

ILA BONGO UKIWA KIONGOZI MZINZI UNAONEKANA KWELI WEWE NI DUME LA MBEGU

chesi said...

...Baadhi ya vyombo vya habari vya marekani vinasema ukiona mwanamke anakubali kusimama na mume wake anayejitetea baada ya kukumbwa na masahibu ya aibu basi ujue mwanamke huyo ni juha wa kupitiliza ama kuna faida fulani ya binafsi anayopata kutokana na mume wake kuendelea kukalia ofisi ambayo anatakiwa ang'atuke!

Anonymous said...

Hebu sema tena! Dola elfu tano kwa saa? Mbunye tu? Wallah huyo jamaa amedata si kitoto! Ati kisa ni star wa nini sijui! Sie wengine tunagonga bure tena walimbwende kuliko huyo! Acha atimuliwe kazi, fala kabisa!