Thursday, March 13, 2008

Huyu ndiye aliyemwangusha Gavana Eliot Spitzer

Nyuso za malaya, Kristen


Wadau, huyu ndiye yule malaya, 'Kristen' wa Emperor's Club. Jina lake hasa ni Ashley Alexandra Dupre (Youmans), ana miaka 22. Ana ukurasa wake binafsi kwenye Myspace.
Wanaomjua Ashley wanashangaa kuwa alikuwa anafanya kazi ya umalaya. Walijua kuwa yeye ni mwanamuziki!
Imefahamika kuwa mteja mwingine, wa Emperors Club ni, The Duke of Westminster, wa Uiingereza (Royal Family)! Kukodi malaya wa Emperors Club inaanzia dola $1,000 hadi $5,500 kwa saa! Bei ya Kristen ilikuwa $4,300 kwa saa. Sijui alikuwa antoa huduma gani!
Haya Gavana Eliot Spitzer alijiuzulu jana. Gavana David Paterson, ataapishwa jumatatu ijayo. Umati wa watu wanajiona kama wamepigwa mangumi na bondia baada ya kugundua kuwa 'Mr. Clean' (Spitzer) ni mnafiki!
Ashley atatajirika sasa maana wataandika vitabu, watatengeneza na sinema kuhusu maisha yake na jinsi alivyomwangusha Gavana wa New York!
Kusoma habari zaidi Bofya:
Ukitaka kusoma Juices zote bofya hapa:

11 comments:

Anonymous said...

Huyu dada ni karibu umri wa binti zake. Lazima aone haya huyo!

Anonymous said...

Lakini ule msemo wa kiswahili ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona, huyo bwana Gavana hapo kautumia vilivyo, hata kama angekuwa mume wangu ningesema kweli bwana hapo ulishikwa! Hata akienda mahakamani hakimu mwenyewe na juries wakimuona huyo kimwana naona watasema mhuu huu mtihani!

Simon Kitururu said...

Sijui kwanini nikimuangalia huyu binti nahisi kuwa mke wa gavana alikuwa anaonekana hivyo alivyokuwa kijana.Inawezekana Gavana alikuwa anafantasaizi tu kuwa yuko na mke wake kama alivyokuwa kijana. Hivi kumuita huyu dada malaya sio kumtusi?

Anonymous said...

malaya lakini mzuri

Anonymous said...

Kumbe tunatofautiana sana kuhusu matumizi ya neno "mzuri". Mie mwanamke kama huyo inabidi yeye ndio anilipe hela nimlale!

Anonymous said...

Hivi huyo gavana hatumii madawa ya kulevya?

Anonymous said...

Huyo dada watu wanamwita malaya kwa kuwa alikuwa anauza ngono na mnunuzi wa ngono naye tumwiteje, maana kwenye biashara hii naona anayepewa jina baya ni muuzaji tu mbona mnunuzi hana jina baya? Kwani biashara yoyote ni makubaliano kati ya muuzaji na mnunuzi.

Anonymous said...

Dada Chemi,
Sio sawa ukisema "Huyu ndiye aliyemwangusha Gov" Huyu Gavana kajiangusha mwenyewe....
Nakuomba ubadilishe kichwa cha habari..
Aksante

Anonymous said...

Napingana na anony wa 5:22PM. Huyu dada ndiye kamwangusha Gavana kwa vile skandali inahusu alivyomlipia safari na kakutana naye Mayflower Hoteli chumban namba 871.

Anonymous said...

ni binti kwelikweli(malaya ni neno tu)

hata wife wa gavana lawama zake zainatakiwa kuwa selective kwani huyu she ni mrembo!!

Anonymous said...

Hawa ndio viongozi wanaojiita wajuaji wa demokrasia,halafu wakati huo-huo wanapigania na kutetea haki za wanawake duniani,Hizi sio kashfa kwa viongozi wa marekani,bali ni FAKHARI NA SHAHADA ZA JUU ZA ADABU NA HESHIMA,wakisha fikia urais watatufundisha ni nini haki na usawa!!!.Mapaka wanaofugwa nyumbani wana heshima na HAYA na adabu ya hali ya juu kuliko baadhi ya viongozi wa Marekani,kama huyo Gavana anaejiita Mr.Clean!!!.